Soma tamko la Jukwaa la Wahariri (mada) na pia soma 'post' yangu vizuri
Kunguru Jasiri
Nimekusoma vizuri.
Umesema "kila mmiliki wa chombo cha habari ana haki ya kuamua habari ipi aitoe.........."
Nimekuuliza bunge letu la Tanzania limekuwa "chombo cha habari" kama ilivyo ITV, TBC nk?
Mimi nadhani "Bunge" ni chombo cha uwakilishi wa wananchi.
Wanapokusanyika pamoja kama ilivyo sasa huko Dodoma, ni "mkutano wa bunge". Na hukusanyika na kufanya mkutano kwa ajili ya kujadili na kupitisha mambo mbalimbali yanayowahusu wananchi wanaowawakilisha k.v bajeti ya serikali,mipango ya maendeleo nk
Kilichofanyika ambacho nilitegemea uniambie hivyo ni kwamba, idara ya mawsiliano ndani ya chombo hiki imeanzisha utaratibu na yenyewe kurusha matangazo ya mikutano yote ya chombo hiki. Nadhani ni TV na Radio
Kwa kuwa wameanzisha TV na Radio yao, hawawezi kujipa haki miliki ya kurusha matangazo ya mikutano yote ya bunge na kuzuia vyombo vingine vya habari kama walivyo wao kusikiliza na kuchukua kwa njia aidha ya kuyaonesha moja kwa moja (live) au kuyarekodi na baadaye kutumia kama reference!!.
Bunge ni chombo cha wananchi kwa kila eneo kupeleka mwakilishi kufanya kwa niaba ya watu wa eneo husika. Kamwe wawakilishi wa wananchi hawawezi kufanyia mijadala yao gizani!!... Wanakuwa wanaogopa na kuficha nini eti??
Na kwamba kama media zingine zinahitaji chochote kilichojadiliwa ndani ya chombo hiki i.e bunge, watapewa na media ya bunge iitwayo "Bunge TV" au "Bunge Radio!". Tell me umeshawahi kuona wapi hii!??
Hii ndiyo hoja ya TEF, kwamba hili halipo popote duniani