Tamko la CHADEMA asili

Tamko la CHADEMA asili

Hivi hiki chama cha "Chadema Asili" kimesajiliwa na msajili mkuu wa vyama....?
Makao makuu yao yako wapi?
Mwenyekiti & Katibu wao ni nani?
Hawa ndo kindakindaki kweli Chadema. Kwasababu hawana mpunga ndo tatizo
 
watani wangu kwa hili nawaonea huruma mtu anawaweka kwenye bus la chama halafu analiuza huku lina watu ndani ila bei ni ile ile account itune wengine mtajijua
 
Mimi ninalolipinga kwa nguvu zote ni kitendo cha kupokea mafisadi na kuanzia kuwasafisha.
Chama chetu hakina tofauti na ile CCM ya Kikwete iliyofuga na kutetea ufisadi.
Ni wazi kwamba Magufuli akichukua CCM tutapotezwa muelekeo kama chama.
Lowassa asipoondolewa na kumuomba msamaha dokta Slaa tutaishia kufanya maigizo yasiyo na kichwa wala miguu.
 
Umeona hiloo!
 
Hivi hiki chama cha "Chadema Asili" kimesajiliwa na msajili mkuu wa vyama....?
Makao makuu yao yako wapi?
Mwenyekiti & Katibu wao ni nani?
kamanda unauliza majibu kwa nini ??? siku zooote huulizi unakuja kuuliza leo! ! umechelewa sana
 
Ndugu wana jf,
CHADEMA asili tuliosalia kuipigania demokrasia ya kweli na kuupiga vita ufisadi unaofanywa na viongozi waliopo CCM na walioondoka,
Tunajua nchi ipo katika kipindi cha vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa kisera na kiuchumi,sisi CHADEMA asili tunafuatilia yale yote yanayo endelea na yanayofanywa na serikali mpya ya rais magufuli,

Labda tuseme yapo tunayompongeza na yapo tusiompongeza,
Tunayompongeza ni kama vile utendaji kazi wake wa utumbuaji majipu na kurudisha nidhamu maofisini,
pia labda tuchukue fursa hii kumpa pongezi kupewa uenyekiti,

CHADEMA asili haturidhishwi na mambo yanavyokwenda kwenye chama chetu,hivi sasa kila mmoja ni msemaji wa chama,chama kimekuwa na watu waoga kupita kiasi,tunajua sisi ni watu wa maandamano na kupigwa,

Hatuungi mkono mkono wabunge wa upinzani kutoka nje kwenye vikao vya bunge utamaduni ni kupambana kwa hoja ikishindikana maandamano,
Mpaka sasa chama kimetupa hoja yake kuu ya chama kupambana na ufisadi ambayo kipindi cha nyuma tulikua tukitembea kifua mbele,

labda tumpongeze mwenyekiti kwa kuendelea kuwepo katika harakati japo kuna watu wanataka kumzidi nguvu,
pia ombi letu mwenyekiti turudishie ile list ya mwembe yanga pale kwenye tovuti ya chama na pia sloogan ya kupambana na ufisadi lazima kila kiongozi mjumbe aimbe hilo na pia chama kufeli kwenye kuhitimu turudi kwenye harakati,

pia tunalaani chama kutumia pesa nyingi kwenye media kujaribu kusafisha watu walioamua kujifunika matope kwa utashi wao.
ni hayo kwa leo ila yapo mengi kwa baadae!

CHADEMA vyema sum sum kazi ngumu
hatupigi ila tunaua,kwanini kwa sera.

Imetolewa na CHADEMA asili
Msisahau kushiriki kwenye kura ya ndiooo...oo kwa wafadhili wenu
 
Ukawa Siyo chama Bali ni muungano wa vyama vilivyoungana kupambana chama cha Mafisadi kuliko chama chochote Tanzania.
hivi ni chama ni kwa sasa ambacho hakina mafisadi. naomba jibu. manake unaongea as if huku kwingine kuna malaika. Mbowe alisema "Ni nani kati yetu anayeweza kutoa boriti kwenye jicho la mwenzake "? tafakali
 
chadema asili wako wengi tu.wengi wamehama ccm wanaona angalau ccm ya magufuli inataka kukata kiu yao ya mabadiliko.chadema ya sahvi haieleweki kabisa inasimamia nn
Kwa hiyo wanahama CCM, basi mkakutane Dodoma.
 
hivi ni chama ni kwa sasa ambacho hakina mafisadi. naomba jibu. manake unaongea as if huku kwingine kuna malaika. Mbowe alisema "Ni nani kati yetu anayeweza kutoa boriti kwenye jicho la mwenzake "? tafakali
Basi kwa maneno hayo tu,ndio yaliweza kutulainisha!
 
Tunahitaji chadema asili iliyoundwa ktk misingi imara ya demokrasia
 
Back
Top Bottom