Tamko la CHADEMA asili

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
15,046
17,658
Ndugu wana jf,
CHADEMA asili tuliosalia kuipigania demokrasia ya kweli na kuupiga vita ufisadi unaofanywa na viongozi waliopo CCM na walioondoka,
Tunajua nchi ipo katika kipindi cha vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa kisera na kiuchumi,sisi CHADEMA asili tunafuatilia yale yote yanayo endelea na yanayofanywa na serikali mpya ya rais magufuli,

Labda tuseme yapo tunayompongeza na yapo tusiompongeza,
Tunayompongeza ni kama vile utendaji kazi wake wa utumbuaji majipu na kurudisha nidhamu maofisini,
pia labda tuchukue fursa hii kumpa pongezi kupewa uenyekiti,

CHADEMA asili haturidhishwi na mambo yanavyokwenda kwenye chama chetu,hivi sasa kila mmoja ni msemaji wa chama,chama kimekuwa na watu waoga kupita kiasi,tunajua sisi ni watu wa maandamano na kupigwa,

Hatuungi mkono mkono wabunge wa upinzani kutoka nje kwenye vikao vya bunge utamaduni ni kupambana kwa hoja ikishindikana maandamano,
Mpaka sasa chama kimetupa hoja yake kuu ya chama kupambana na ufisadi ambayo kipindi cha nyuma tulikua tukitembea kifua mbele,

labda tumpongeze mwenyekiti kwa kuendelea kuwepo katika harakati japo kuna watu wanataka kumzidi nguvu,
pia ombi letu mwenyekiti turudishie ile list ya mwembe yanga pale kwenye tovuti ya chama na pia sloogan ya kupambana na ufisadi lazima kila kiongozi mjumbe aimbe hilo na pia chama kufeli kwenye kuhitimu turudi kwenye harakati,

pia tunalaani chama kutumia pesa nyingi kwenye media kujaribu kusafisha watu walioamua kujifunika matope kwa utashi wao.
ni hayo kwa leo ila yapo mengi kwa baadae!

CHADEMA vyema sum sum kazi ngumu
hatupigi ila tunaua,kwanini kwa sera.

Imetolewa na CHADEMA asili
 
Kwa hali ya kawaida, utawala mpya huja na maono mapya, itikadi mpya na style mpya ya uongozi..wengi tuliochukizwa na huu utawala mpya hatukuwa na option bali kuondoka na kuhamia kule kwenye mabadiliko ya kweli..usipoteze energy kubadili chama wakati kipo chama kilichozaliwa upya na kinachoendana na ideology/itikadi unazoamini
 
Hivi hiki chama cha "Chadema Asili" kimesajiliwa na msajili mkuu wa vyama....?
Makao makuu yao yako wapi?
Mwenyekiti & Katibu wao ni nani?
 
Kwa hali ya kawaida, utawala mpya huja na maono mapya, itikadi mpya na style mpya ya uongozi..wengi tuliochukizwa na huu utawala mpya hatukuwa na option bali kuondoka na kuhamia kule kwenye mabadiliko ya kweli..usipoteze energy kubadili chama wakati kipo chama kilichozaliwa upya na kinachoendana na ideology/itikadi unazoamini
Haiwezekani mwenyeji kukimbia mgeni
 
Ndugu wana jf,
chadema asili tuliosalia kuipigania demokrasia ya kweli na kuupiga vita ufisadi unaofanywa na viongozi waliopo ccm na walioondoka,

Tunajua nchi ipo katika kipindi cha vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa kisera na kiuchumi,sisi chadema asili tunafuatilia yale yote yanayo endelea na yanayofanywa na serikali mpya ya rais magufuli,

labda tuseme yapo tunayo mpongeza na yapo tusio mpongeza,

Tunayompongeza ni kama vile utendaji kazi wake wa utumbuaji majipu na kurudisha nidhamu maofisini,

pia labda tuchukue fursa hii kumpa pongezi kupewa uenyekiti,

Chadema asili haturidhishwi na mambo yanavyokwenda kwenye chama chetu,hivi sasa kila mmoja ni msemaji wa chama,chama kimekuwa na watu waoga kupita kiasi,tunajua sisi ni watu wa maandamano na kupigwa,

Hatuungi mkono mkono wabunge wa upinzani kutoka nje kwenye vikao vya bunge utamaduni ni kupambana kwa hoja ikishindikana maandamano,

Mpaka sasa chama kimetupa hoja yake kuu ya chama kupambana na ufisadi ambayo kipindi cha nyuma tulikua tukitembea kifua mbele,

labda tumpongeze mwenyekiti kwa kuendelea kuwepo katika harakati japo kuna watu wanataka kumzidi nguvu,

pia ombi letu mwenyekiti turudishie ile list ya mwembe yanga pale kwenye tovuti ya chama na pia sloogan ya kupambana na ufisadi lazima kila kiongozi mjumbe aimbe hilo na pia chama kufeli kwenye kuhitimu turudi kwenye harakati,

pia tunalaani chama kutumia pesa nyingi kwenye media kujaribu kusafisha watu walioamua kujifunika matope kwa utashi wao.

ni hayo kwa leo ila yapo mengi kwa baadae!

Chadema vyema sum sum kazi ngumu
hatupigi ila tunaua,kwanini kwa sera.

Imetolewa na chadema asili

Hakuna chama cha siasa nchini kinachojulikana kama chadema asili....
 
Tamko hili mlilitolea wapi na waandishi gani walihudhuria?
Tamko ili liwe tamko ni lazima litolewe ktk muktadha maalumu, watu maalumu na wakati maalumu.

Poleni sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom