Mungu alituletea JK kwa maana kamili, Akatuletea Mzee Makamba sasa anakamilisha kazi ya Ukombozi kutuletea Mwigulu Nchemba na Nape ukombozi umekaribia na njia ni nyeupe.
Utendaji wa hawa tajwa umeidhihirisha CCM na madudu yake, ukosefu wa utu, unyama na matumizi mabovu ya kupindukia ya vyombo vya usalama. Mauaji ya raia na mateso kwa watanzania. ninawaomba tufanye na uchunguzi wa matukio yote ya halaiki kuanzia kumwagiwa tindikali sheikh, kuchomwa kisu sheikh, kuchinjwa mchungaji na kupigwa risasi mapadre inawezekana hili genge liko nyuma ya haya yote ili kuvuruga amani ya nchi yetu.
Fujo zote na uchomaji wa nyumba za ibada inawezekana kana kabisa hawa watu wanamkono wao huku ni muhimu uchunguzi wa kina ukafanyika ili kuweza kubaini kila janga ambalo lilikuwa kwa ajili ya kupaka matope ama dini, chama cha siasa, kabila, nk.
Mungu ni mwema sana, huwa hawaachi wema wateseke siku zote. Sasa tutashuhudia mitambo ya simu ikitetereka, tutawahi sattelite najua bado tunatumia za wazungu. Wakati umefika kila raia mwenye mapenzi mema na nchi yake atoae taarifa yeyote pale alipo anachokiona na kinachofanywa na hawa majangili wa demokrasia. Tunajua wapo wengi wema TISS, wapo wengi wema polisi, wapo wengi kwenye kampuni za simu na ikulu. Wakati umefika kuitumikia nchi kwa uadilifu badala ya tumbo. Kama leo wameweza kuuwa ili wabaki Ikulu kesho wanaweza kukuuwa wewe usiwachekee hata kidogo toa taarifa mapema ili ushindi uwe wetu wote.
Mungu yupo nasi daima.
Daima zilizomwagika, walioko jela na wanaoteswa hakika haitapotea kamwe.