PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Tamko rasmi la Baraza la Vijana Chadema Taifa (BAVICHA) kuunga mkono maandamano ya vijana wa Gen Z, kesho Oktoba 29,2025.
==
Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) limeundwa kwa mujibu wa ibara ya 7.8.2 (a) ya katiba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya mwaka 2006 toleo la 2019 likiwa na lengo kuu la kuhakikisha vijana wanatoa mchango thabiti katika kukuza na kuendeleza madhumuni ya Chama kwa maslai na ustawi wa Taifa la Tanzania kwa mujibu wa mwongozo wa BAVICHA Na.3.1 toleo la 2019.
Tunafahamu msimamo wa Chama chetu wa kuhusu uchaguzi mkuu 2025 ulikuwa ni NO REFORMS NO ELECTION. Pia, tunafahamu vijana na umma wa Watanzania wapenda haki na mabadiliko ndani ya Taifa letu kuwa wametangaza kuwepo kwa maandamano tarehe 29.10.2025 kudai haki za msingi ikiwemo uchaguzi HURU na HAKI na wenye KUAMINIKA, sambamba na kupinga ufujaji wa rasilimali za Taifa.
BAVICHA katika kuunga mkono msimamo wa Chama chetu na kuunga Taifa mkono vuguvugu la vijana wa kizazi kipya (Gen Z) wanaokabiliwa na changamoto za ukosefu mkubwa wa ajira, kuuwawa, kutekwa na kupotezwa. Hatuna budi kuwaunga mkono vijana wenzetu walioamua kupaza sauti kwa njia ya maandamano ya amani Oktoba 29.2025.
Siku zote vijana wa CHADEMA tunapaswa kuongozwa kwa na maneno ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuwa, Tunataka kuona katika Taifa hili vijana jeuri na wenye kujiamini, si vijana waoga akina ndio bwana mkubwa, vijana wanaohoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyosha-bihiana na matakwa na matajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa.
Kwa uzito wa maneno haya ya Mwalimu ambayo vijana tumejiapiza kuyaishi, na kwa kuwa watawala wamepuuza maoni ya wananchi. Natoa WITO kwa vijana wa CHADEMA nchi nzima kuwa sehemu ya historia hii muhimu kwa Taifa letu kwa sababu lugha ya MAANDAMANO ndiyo ludha pekee ambayo watawala wanaweza kuielewa kwa sasa.
Maono ya Mwalimu yakawe ni taa na DIRA katika kulinda miiko na tunu za Taifa letu zenye lengo la kulinda UTU, UHANI na DEMOKRASIA YA KWELI nchini.
Tunawatakia vijana wote kila la kheri katika mapambano ya kudai haki, uhuru na maendeleo ya watu ndani ya Taifa letu.
VIJANA NI NGUVU YA MABADILIKO.
MUNGU IBARIKI CHADEMA. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Imetolewa Na;
BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA (BAVICHA - TAIFA)