Tamko la Baraza la Maaskofu juu ya hali ya Zanzibar na mgomo wa madaktari

Status
Not open for further replies.
Busara hizi zitaongoza amani kamwe,tunawaheshimu sana maaskofu wa kikatoliki.kati ya viongozi wasomi waliojaa busara basi ni hawa.nasisitiza tena kuwa hawa sio vihiyo.hawa wameacha kuoa,kuwa na familia ili kufikiri sawa sawa.sasa hawa wamesema.walisema muswada wa katiba ufutwe serikali ikakataa lakini baadaye iliuondoa.
Katika hili hakuna ubishi wala objection hapa.serikali mara moja tekeleza hili!!
 
Kama huna digree huwezi kuwa kiongozi wa kanisa katoliki, hakika huku ndo kuna vichwa!

Jana nikiwa kwenye ibada St. Peters church alikuja Padre mgeni akijatambulisha akasema yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa tano chuo kikuu cha Ardhi akimalizia degree yake ya Architecture. Yaani hawa mapadre nawa admire sana.
Nalipenda sana kanisa katoliki wengine wapige porojo sisi twasonga mbele.
 
Tamko la maaskofu halivuki MAJI, znz ni nchi inayojitegemea na haiendeshwi na kanisa.
Pole sana! Hoja kuhusu amani, usalama, upendo na kuheshimiana kwa watanzania wote bila kujali itikadi ya mtu si kitu kwako? Kwa hiyo ndiyo kusema Zanzibar inajitegemea kwa mauaji na kuchoma makanisa? Bado kuna safari ndefu!!!!
 
Lengo la Mkutano huu lilikuwa kutathmini shughuli na kazi zetu za Kichungaji na za huduma za jamii kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita (2009-2012) na vile vile kupanga mikakati ya kuboresha shughuli hizo za Kichungaji na za huduma za Jamii katika Nyanja za Afya, Elimu, Maji, misaada kwa wasiojiweza, utetezi na ushawishi, kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo (2012-2015).

Jibu: Mngebakia kuzungumzia haya na kuwaeleza wananchi kwa ujumla pesa za umma mlizopokea through MoU na misamaha ya kodi mlizitumiaje kwa miaka mitatu iliyopita...

Pamoja na kufanya tathmini ya kina ya utendaji wa Baraza letu katika kipindi hicho kilichopita, na kupanga mipango kabambe kwa ajili ya utendaji wa Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, Mkutano wetu Mkuu umekuwa fursa ya kujadiliana na kushirikishana baadhi ya matukio/mambo ambayo, kwa hakika, yameitikisa jamii yetu ya Watanzania na kuidhalilisha mbele ya Jumuiya ya kimataifa.

Jibu: Naona tamko lenu limekazia matukio kuliko shughuli zenu za kila, hili la matukio linashughulikiwa na vyombo husika vya serikali nyinyi kama wananchi na waumini wa kawaida msubiri vyombo huru vifanye kazi??? who are you??

Ili kuepuka hali hiyo isitokee, kwa moyo wa unyenyekevu kabisa, tunapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:-
Sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania tutaendelea kusali ili kuiombea nchi yetu amani. Licha ya sala na maombi ya kawaida kwa ajili ya lengo hilo, Mkutano Mkuu umeamua kwamba, tutakuwa na siku moja ya kusali kitaifa kwa ajili ya kuomba amani;

Jibu: Naam Amin
Tutaendelea kutumia sauti yetu ya kinabii kuonya, kukemea na kukaripia vitendo vyote vile vinavyoashiria kueneza chuki miongoni mwa watu wa dini mbali mbali;

Jibu: Hapa hamjasema kitu

Kwa kutumia Tume na Idara zetu, tutaendelea kujenga na kueneza mazungumzano na Waamini wa dini mbali mbali tukiheshimu tofauti zilizopo. Hii ni kwa sababu tunaamini kwamba, suala la dini ni wito na hiari ya mtu na hakuna mtu yeyote aliye na haki ya kumlazimisha mwingine ajiunge na dini yake.

Jibu: Amani ipo Tanzania si kwasababu yenu wala mazungumzo yenu kwasababu ya serikali na vyombo vinavyotoa haki

Mihadhara, makongamano na mikutano yenye lengo la kutoa kashfa na kuchochea chuki miongoni mwa dini mbalimbali ipigwe marufuku;

Jibu: Hapa mmeanza kupotea kabisa; nini maana ya kashfa, nini maana ya kuchochea; kama mmeshindwa kueneza dini yenu msikataze watu kufanya debates kuhusu comperative religiuos debates...lazima pasemwa dini feki ni ipi? kama hutaki kusikiliza kalale usiombe msaada kwa serikali.

Vyombo vya habari vinavyoeneza uzushi, kashfa na uchochezi vidhibitiwe kwa kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungiwa;

Jibu: Too general and hypothetical..vitaje vyombo hivyo na useme uzushi gani na uchochezi gani wamefanya; acheni unafiki wasomi wa kweli hawmumunyi maneno

Uzushi na uongo unaoenezwa na vyombo vya habari na watu wenye lengo la kuwachonganisha Watanzania na waamini wa dini mbali mbali utolewe ufafanuzi mara moja na Wizara na vyombo vingine vinavyohusika;

Jibu: Hapa hamjasema kitu

Kuweko na mpango kabambe wa kutoa elimu ya uraia yenye kina na upana katika nafasi zote, itakayowawezesha vijana wetu kuwa wazalendo kwa nchi yao na kuepuka propaganda za kuwagawa Watanzania kwa misingi ya kidini;

Jibu: Naona mnaanza siasa kama zile za 2010; sijaona mkiongelea huduma zenu tena
Suala la ukosefu wa ajira, hasa miongoni mwa vijana, liangaliwe kwa makini kwani linaweza kuwa moja ya sababu zinazowafanya vijana wengi kujiingiza katika vikundi vya kidini vinavyojenga chuki na kutoa matumaini ya uongo;

Jibu: Haya mambo ya serikali naona mnaongea kama Lowassa vile

Lakini, zaidi ya yote, iwapo Serikali yetu na mamlaka husika inataka kuwa na imani mbele ya jamii kwamba ina nia thabiti ya kuhakikisha kwamba vurugu za kidini hazipati nafasi katika Nchi yetu, wale wote wanaohusika na vurugu hizo wachukuliwe hatua za kisheria mara moja! Ni vigumu kuamini kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 2001 mpaka sasa, Makanisa 25 yamekwisha chomwa moto Visiwani Zanzibar lakini hakuna aliyekamatwa na kuchuliwa hatua za kisheria!

Jibu: Naaam uchunguzi unaendelea


Tunaiasa Serikali yetu ikae tena pamoja na madaktari na kuchambua hoja zitakazowekwa mbele yao. Uwazi na ukweli vikitawala hakuna pande itakayokataa kuridhia eti kwa sababu ya kukataa tu bila hoja. Taifa letu limejipatia aibu mbele ya macho ya ulimwengu ya jinsi tunavyoshindwa kuishi kile tunachosema kwenye majukwaa.

Jibu: Hii vilevile inatokana na serikali kupeleka pesa kwenye miradi ya kanisa bila ukaguzi; hivi hata bugando na kcmc wanataka kuboreshewa mazingira yao na serikali siyo nyinyi tena?? mbona hapo kimyaaaaaaaaaa
 
Jana nikiwa kwenye ibada St. Peters church alikuja Padre mgeni akijatambulisha akasema yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa tano chuo kikuu cha Ardhi akimalizia degree yake ya Architecture. Yaani hawa mapadre nawa admire sana.
Nalipenda sana kanisa katoliki wengine wapige porojo sisi twasonga mbele.

Aisee, lakini waache kuiba pesa za umma; kusoma ili kuiba kuna faida gani
 
Kwa hiyo wawaache muendelee kuchoma makanisa?

Wamechoma wenyewe wakatoliki ili kupata sympthy na kuwanyamzisha uamsho..

Inawezekana vilvile kuna financial motives, kwasababu yalikuwa magofu hakuna waumini walitaka insurance compensation

ndio maana hawajashikwa hata moja leo
 
Maaskofu wameandika waraka mzuri kabisa. Nasikia huwa wanaongozwa na roho mtakatifu kwa hiyo waraka huu wamesaidiwa na roho mtakatifu. Mimi nakubaliana nao kabisa kwasababu haina haja kuwa na fujo za kidinikatika nchi hii. na serikali lazima ihakikishe usawa unafanyika. Sababu ya fujo la zanzibar sio udini bali ni siasa na wale wahusika kwenye fujo hilo wanajulikana na viongozi wetu wanawajua vizuri tu. Zile ni fitina za kutaka kuwagawa wananchi kitabaka. Tunapoona jambo hasa hapa tanzania linatakiwa kuangaliwa kwa makini sana venginevo linaweza kuleta shida sana. Maaskofu waendelee kueneza ukweli na wakiona mapungufu katika uongozi wasiwache kusema. Ukweli ndio utakao tuvusha.
 
Nimeishi kitume na watawa hawa kwa miaka mingi....nina msingi mzuri wa kitawa uliojengwa vema na mzazi wangu tangu utotoni.....matamko kama haya huwa si ya kubeza.....ukityumia busara za kawaida kabisa unaona kuna ukweli na wahusika wanapaswa kuchukua hatua za haraka sana.....

Ndo hivyo tena...mwenye macho haambiwi ona. Tunasahau kupambana na mambo ya msingi yanayoisumbua jamii yetu tunaleta hoja za udini...lakini mficha maradhi kifo kitamuumbua. Ndo maana sasa hivi yale matatizo ya kweli yanafumuka karibu kila upande.
 
Imekaa kichochezi zaidi.TWAMBIENI KWANINI MAHOSPITAL YENU YANAGOMA HUKU MKIPEWA PESA NA SEREKALI ISIYONADINI?
 
juu ya kanisa hili linishawahi kusema tofauti yao na hawa wengine....
 
Safi sana kwa kuwaambia maana hawa wenzetu sijui niseme ni wavivu wa kufikiria inakuwaje watu wanapinga muungano then wanachoma makanisa? Kama wao ni wababe basi wakachome ikulu, ukweli ni kwamba hii serikali yetu ipo kama haipo manake lile suala sio la kunyamazia kabisa
 
je, umepata amani baada ya kutoa kashfa zako hizo? nina amini kwa 100% bado utakuwa na mahangaiko moyoni...lakini sisi unotukashfu hatuna shida bana, tunasonga mbele na imani yetu kwa amani tele...!
 
je, umepata amani baada ya kutoa kashfa zako hizo? nina amini kwa 100% bado utakuwa na mahangaiko moyoni...lakini sisi unotukashfu hatuna shida bana, tunasonga mbele na imani yetu kwa amani tele...!

Mbona viongozi wako wanaiomba serikali ipige marufuku mihadhara (debates)???

Wameshindwa kuitetea dini yao (inapupukutika) wanaomba msaada wa serikali?

Serikali inawahusu nini mihadhara ya dini "comperative religious debates"
 
Huyo Bakhresa so far amewasaidia vipi waislam kuondokana na ombwe la ujinga na umaskini. mbona hatujasikia amejenga shule? anogopa kutoa fedha zake kwa vilaza wanaotumia fedha kuanzisha redio na tv za uchochezi nonsense.

Safari hii redio iman imewashika vibaya..hadi mnaomba serikali iwasaidie wtf

Mkishindwa kuwajibu hoja redio iman (kwasababu ya VILAZA wenu) msiwachonganishe waislam na serikali,..

come on and debates siyo kila siku kulialia "waislam wana kashifu my foot"

Nendeni kwenye debates ikiwa kweli nyie siyo VILAZA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom