Tamko la Baraza la Maaskofu juu ya hali ya Zanzibar na mgomo wa madaktari

Status
Not open for further replies.

Nyetk

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
1,648
1,696
UJUMBE WA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA KWA WAAMINI WAKATOLIKI NA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA

Sisi Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania tumekutana katika Mkutano wetu Mkuu wa 65 wa kawaida tangu tarehe 23 – 30 Juni 2012 uliowajumuisha Wakuu wa Mashirika ya Kitawa, wakuu wa Idara, Tume na Taasisi za Baraza pamoja na wawakilishi Walei. Lengo la Mkutano huu lilikuwa kutathmini shughuli na kazi zetu za Kichungaji na za huduma za jamii kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita (2009-2012) na vile vile kupanga mikakati ya kuboresha shughuli hizo za Kichungaji na za huduma za Jamii katika Nyanja za Afya, Elimu, Maji, misaada kwa wasiojiweza, utetezi na ushawishi, kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo (2012-2015).

Pamoja na kufanya tathmini ya kina ya utendaji wa Baraza letu katika kipindi hicho kilichopita, na kupanga mipango kabambe kwa ajili ya utendaji wa Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, Mkutano wetu Mkuu umekuwa fursa ya kujadiliana na kushirikishana baadhi ya matukio/mambo ambayo, kwa hakika, yameitikisa jamii yetu ya Watanzania na kuidhalilisha mbele ya Jumuiya ya kimataifa.

Kwa namna ya pekee kabisa, tumetafakari juu ya vuguru za kidini za hivi karibuni zilizotokea katika Visiwa vya Zanzibar kuanzia 26-28 Mei, 2012 na kupelekea kuchomwa moto kwa baadhi ya Makanisa Visiwani humo pamoja na uharibifu mkubwa wa mali na uvunjifu wa amani. Bila kupenda kurudia matamko ya Wadau mbali mbali waliyoyatoa katika nyakati tofauti kulaani bila kusita hali hiyo ya kutisha na kusikitisha iliyojitokeza Visiwani humo, tunaunga mkono kwa nguvu zote kauli na jitihada za wale wote wenye mapenzi mema walioguswa na vitendo hivyo na hivyo kuvilaani. Tunatoa pole na kueleza mshikamano wetu wa kindugu kwa wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na vitendo hivyo vya vurugu ambavyo vimefanya sehemu ya jamii ya wakazi wa Visiwani humo, hasa Wakristo, kuishi kwa wasi wasi mkubwa kutokana na vitisho vinavyoendelea kutolewa na baadhi ya vikundi pamoja na hali ya kutopewa ulinzi wa kutosha na vyombo husika. Tunaendelea kuwaahidi Sala na mshikamano wetu katika kipindi hiki kigumu.

Pamoja na hayo, tunapenda kuwakumbusha Watanzania wenzetu, hasa mamlaka husika kutafakari na kuzingatia busara ya wahenga waliosema kwamba "mwanzo wa makubwa ni madogo" na kwamba "mdharau mwiba mguu huota tende". Kumbu kumbu zinatwambia kwamba, chuki za wazi za kidini zilianza kuinyemelea nchi yetu miaka ya 1990, pale mihadhara ya kashfa za kidini ilipoanza kuruhusiwa. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, kwa kuongozwa na busara ya kichungaji, kwa nyakati tofauti, liliandika barua kuziomba na kuzihimiza Mamlaka husika kuingilia kati na kuhakikisha kwamba mihadhara kama hiyo haipati nafasi ya kuendelea katika nchi yetu kwani kamwe haiwezi kuwa na tija isipokuwa kuamsha hisia kali za kidini, jazba na kujenga chuki miongoni mwa waamini wa dini tofauti. Kwa bahati mbaya, ushauri huo wa Baraza la Maaskofu ulipuuzwa na mamlaka husika.

Hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko kubwa la vyombo vya habari ambavyo vimeanzishwa na ambavyo badala ya kuzingatia malengo mazuri ya vyombo vya habari ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, vimeonyesha malengo ya wazi ya kueneza uzushi, kashfa, chuki na uchochezi. Bado kuna CD/DVD na Kanda chungu nzima zilizozagaa mitaani zenye malengo kama hayo ambapo, kwa mshangao mkubwa wa raia wema wa nchi hii, licha ya wahusika kufahamika na kuonekana wazi wazi, hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi yao. Tunachelea hata kudhani kwamba mamlaka za dola zinawakingia kifua wadau wa harakati hizo.

Mkusanyiko wa mambo yote haya ndio uliotufikisha hapa tulipo. Kwa upendo tulio nao kwa nchi yetu na kwa kuzingatia historia ya mlolongo wa matukio yaliyotufikisha hapa tulipo, tunahofu, lakini kwa uwazi tunapenda kuziambia mamlaka husika, watu wote wenye mapenzi mema na Watanzania wote kwa ujumla kwamba, iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa mara moja ili kurekebisha hali hii, baada ya miaka michache, hakika kwamba nchi yetu inaweza kuingia katika machafuko makubwa ya kidini. Ili kuepuka hali hiyo isitokee, kwa moyo wa unyenyekevu kabisa, tunapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:-

  • Sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania tutaendelea kusali ili kuiombea nchi yetu amani. Licha ya sala na maombi ya kawaida kwa ajili ya lengo hilo, Mkutano Mkuu umeamua kwamba, tutakuwa na siku moja ya kusali kitaifa kwa ajili ya kuomba amani;
  • Tutaendelea kutumia sauti yetu ya kinabii kuonya, kukemea na kukaripia vitendo vyote vile vinavyoashiria kueneza chuki miongoni mwa watu wa dini mbali mbali;
  • Kwa kutumia Tume na Idara zetu, tutaendelea kujenga na kueneza mazungumzano na Waamini wa dini mbali mbali tukiheshimu tofauti zilizopo. Hii ni kwa sababu tunaamini kwamba, suala la dini ni wito na hiari ya mtu na hakuna mtu yeyote aliye na haki ya kumlazimisha mwingine ajiunge na dini yake.

Kwa upande wa wadau wengine na hasa kwa Serikali yetu pamoja na vyombo vyake vya usalama tunapendekeza yafuatayo:-

  • Mihadhara, makongamano na mikutano yenye lengo la kutoa kashfa na kuchochea chuki miongoni mwa dini mbalimbali ipigwe marufuku;
  • Vyombo vya habari vinavyoeneza uzushi, kashfa na uchochezi vidhibitiwe kwa kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungiwa;
  • Uzushi na uongo unaoenezwa na vyombo vya habari na watu wenye lengo la kuwachonganisha Watanzania na waamini wa dini mbali mbali utolewe ufafanuzi mara moja na Wizara na vyombo vingine vinavyohusika;
  • Kuweko na mpango kabambe wa kutoa elimu ya uraia yenye kina na upana katika nafasi zote, itakayowawezesha vijana wetu kuwa wazalendo kwa nchi yao na kuepuka propaganda za kuwagawa Watanzania kwa misingi ya kidini;
  • Suala la ukosefu wa ajira, hasa miongoni mwa vijana, liangaliwe kwa makini kwani linaweza kuwa moja ya sababu zinazowafanya vijana wengi kujiingiza katika vikundi vya kidini vinavyojenga chuki na kutoa matumaini ya uongo;
  • Lakini, zaidi ya yote, iwapo Serikali yetu na mamlaka husika inataka kuwa na imani mbele ya jamii kwamba ina nia thabiti ya kuhakikisha kwamba vurugu za kidini hazipati nafasi katika Nchi yetu, wale wote wanaohusika na vurugu hizo wachukuliwe hatua za kisheria mara moja! Ni vigumu kuamini kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 2001 mpaka sasa, Makanisa 25 yamekwisha chomwa moto Visiwani Zanzibar lakini hakuna aliyekamatwa na kuchuliwa hatua za kisheria!

Tumefanya mkutano wetu katika mazingira ya kuwepo mvutano kati ya madaktari na serikali na kwa bahati mbaya sana, kama tulivyokwisha kutamka huko nyuma, mvutano huu unaleta athari kubwa kwa raia wasio na hatia, athari ambayo haiwezi kurudishwa. Uhai wa raia wa Tanzania unaangamia kwa kukosa ulinzi wa tiba. Katika hili tunapenda kukumbusha kuwa kila mmoja ni mdau. Hakuna hata mmoja anayeweza kulikwepa hili. Tunapenda kurudia himizo letu la awali kwamba ni bora ikapatikana njia nyingine iliyo mwafaka zaidi ya kudai haki na mazingira yanayofaa ya kazi bila kuleta madhara ya kupoteza uhai ambao ni haki msingi ya kila mwanadamu.

Tunaiasa Serikali yetu ikae tena pamoja na madaktari na kuchambua hoja zitakazowekwa mbele yao. Uwazi na ukweli vikitawala hakuna pande itakayokataa kuridhia eti kwa sababu ya kukataa tu bila hoja. Taifa letu limejipatia aibu mbele ya macho ya ulimwengu ya jinsi tunavyoshindwa kuishi kile tunachosema kwenye majukwaa.

Mwisho, tunaendelea kuwaalika Watanzania wenzetu, hasa viongozi wa dini mbalimbali kuwahamasisha waamini wao wawe raia wema wa nchi hii kwa kuungana pamoja kuhamasisha upendo, haki, amani na maridhiano miongoni mwa Watanzania wote. Licha ya tofauti zetu, tuzingatie hasa yale yanayotuunganisha: ubinadamu wetu na uraia wetu wa nchi yetu Tukufu ya Tanzania ambamo tutake tusitake, ni lazima wote tuishi! Tuepe ushindani ambao hauna tija isipokuwa kutupeleka katika kujenga chuki na hali ya kudhaniana vibaya miongoni mwa Waamini wetu. Iwapo kuna sababu ya kushindana, tushindane katika kubuni mbinu za kujenga Upendo na Amani miongoni mwa Watanzania katika kutafuta njia za kuwaletea maendeleo yatakayowatoa kutoka katika Umaskini, Ujinga na Maradhi ambao ndio adui wetu sote.

Tunaiombea Nchi yetu Amani na Usalama.



+Jude Thaddaeus Ruwai'chi
RAIS: BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA/
ASKOFU MKUU JIMBO LA MWANZA

Juni 30, 2012
 
Wasomi wa kikatoliki wakikaa ujue kuna jambo! Hawa ndo wasomi wametoa tamko! Yapasa serikali ichukue hatua dhidi ya wahusika. Hivi vichwa havikurupuki! Hujifungia ndani na kutoka na maneno ya busara.
 
Kama huna digree huwezi kuwa kiongozi wa kanisa katoliki, hakika huku ndo kuna vichwa!
 
tamko ni zuri na limejaa hekima na nia njema kwa taifa letu...je kuna mtu ansikiliza tamko hili? je kuna moyo unaotamani kutekeleza? Kama hakuna tutaangamia kama nchi
 
Kikwete ni mnafiki sana , kama alikuwa anasema ukweli au kama alikuwa na hoja za msingi kwa nini asisimame na madaktari wote pamoja watueleze kila mtu anasemaje hili tuone mwongo ni yupi . Yeye anakuja peke yake anabwabwaja anadhani wanasiasa wa nchi hii tunwaamini. Mwongo Mkubwa
 
Nimeishi kitume na watawa hawa kwa miaka mingi....nina msingi mzuri wa kitawa uliojengwa vema na mzazi wangu tangu utotoni.....matamko kama haya huwa si ya kubeza.....ukityumia busara za kawaida kabisa unaona kuna ukweli na wahusika wanapaswa kuchukua hatua za haraka sana.....
 
Kama huna digree huwezi kuwa kiongozi wa kanisa katoliki, hakika huku ndo kuna vichwa!

Sheria za Kanisa Katoliki yaan Canon Laws inasema kwamba ili uwe askofu lazima uwe walau na Phd au equivalent:

Can. 378(1){5}:
{To be a suitable candidate for the episcopate, a person must hold a doctorate or at least a licentiate in sacred Scripture, theology or canon law, from an institute of higher studies approved by the Apostolic See, or at least be well versed in these disciplines}
 
Asante mkuu Nyetk kutuletea huu ujumbe jamvini. Mimi nilisiki live jana redioni. Ni ujumbe uliosheheni ukweli, uko very balanced na umetolewa bila 'biace' yoyote. Natamani kungefanyika utaratibu wa kuunga mkono tamko hili kwa mstakabali wa nchi hii. Big-up sana wazee wetu.

NAUNGA MKONO TAMKO!
 
Last edited by a moderator:
Inachukua miaka 8 kuwa padre baada ya kumaliza form six na kati ya hiyo nane lazima usome philosophy ikusaidie kufikiria vizuri,Tunapaswa kuweka itikadi zetu pembeni na kusikiliza busara za hawa ndugu
 
Inachukua miaka 8 kuwa padre baada ya kumaliza form six na kati ya hiyo nane lazima usome philosophy ikusaidie kufikiria vizuri,Tunapaswa kuweka itikadi zetu pembeni na kusikiliza busara za hawa ndugu

Kwa miaka hiyo minane ya upadri ni sawa na degree ya miaka mitatu, ukaenda masters miaka miwili na PhD miaka mitatu.

Kwa padri wa kanisa katoliki ni equivalent na Phd ya huyu niliyemfananisha. Na huyo ujue ni padri wa Jimbo yaani diocesan. Padri wa Mashirika kama majesuit unaweza kufika hata miaka 45 unausotea!!
 
Kwa miaka hiyo minane ya upadri ni sawa na degree ya miaka mitatu, ukaenda masters miaka miwili na PhD miaka mitatu.

Kwa padri wa kanisa katoliki ni equivalent na Phd ya huyu niliyemfananisha. Na huyo ujue ni padri wa Jimbo yaani diocesan. Padri wa Mashirika kama majesuit unaweza kufika hata miaka 45 unausotea!!

Phd halafu unafanya usheraiti wtf
 
kanisa katoliki lina watu wenye akili sana....sio wale wenzetu wanaogomea sensa
 
Maaskofu hawana kauli kwa nchi yenye waislamu 99% hii kauli iishie Tanganyika.

Wanataka serikali ikataze waislamu wasihubiri dini yao...sasa kama wao wameshindwa kueneza dini yao wanataka serikali iwasaidie kwa kuwazuia wengine wasifanye mihadhara??

Eti vyombo vya habari vifutwe..wako kwenye enzi zile za st. nyerere; vifutwe kwanini unafikiri hizi ni zama za kusikiliza unachotaka..kila moja uko right kuwa maoni yake kama hutaki usisikilize redio hiyo.."SIYO UNALIA KWA Serikali" what a shame..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom