TAMISEMI: Uhamisho utaruhusiwa lini? Mnakera Sana!

TAMISEMI: Uhamisho utaruhusiwa lini? Mnakera Sana!

7 ELEVEN

Member
Joined
May 29, 2017
Posts
74
Reaction score
138
Wandugu,

Nipeni pole,

Hawa TAMISEMI hivi uhamisho watatoa lini? Mbona wafanyakazi wa umma tunateseka hivi jamani? Yale maahadi yote ya Magufuli, Mama yetu mpendwa mama Samia na ile ya PM kuwa uhamisho ni HAKI ya kila mfanyakazi na watu watahama tu bila shida, sasa mtatekeleza lini?

Huku kitaa jamani maisha magumu, mshahara wenyewe kidoncho na huo huo kugawana mara kule mara huku, watoto shule ada, hivi huko kazini kweli nitakuwa na moyo wa kutekeleza kauli mbiu yenu ya [HASHTAG]#HAPAKAZI[/HASHTAG] Tu?

Muwe watu wa huruma jamani, tupeni uhamisho wetu, maana tulitegemea hii juni mnatoa majina lakini hadi leo holaaaa, yaani ngachoka kabisa jamani dah. Na mshahara wenyewe huu mbuzi toka alivyouacha JK hadi leo hii, hivi Magu huna huruma jamani? Kwanini mambo mengine ya kawaida lakini unaleta urasimu usio na tija halafu mwisho wa siku wafanyakazi wanakata tamaa? Au unadhani kuwatisha wafanyakazi na kauli tata ndio zitaleta tija katika uchumi wa viwanda?

HAPANA BABA BADILIKA, SISI WAFANYAKAZI TUNAOMBA HAKI YETU. SAWA TUNYIME TU KUTUONGEZEA MSHAHARA LAKINI ACHIA UHAMISHO; TUTAJIHAMISHA NA STRESS KAZINI ZITAPUNGUA, na morali wa kazi utaongezeka Rais wetu.

Simbachawene najua huu uzi utasoma tu na mwenzio Kailuki sijui kahiruki na uhakiki wake usioishaaa jamani tumechokaaaaa! MAJALIWA hebu tusaidieni jamani au wafanyakazi wa umma nchi hii tumewakosea nini?

WAKURUGENZI NYIE HUKO TAMISEMI si mnasoma huu uzi jamani? basi mpelekeeni taarifa bosi wenu mwambieni ukweli kuwa watu wamechoka wanataka uhamisho wao utoke na tupo tayari kujihamisha bila shida yeyote na wala hatutaki mia yenu ya uhamisho.

Nawashukuru kwa kunisoma na kunielewa, hivyo Mungu awabariki kwa kusikia kilio chetu sisi wafanyakazi wa Umma.

#ASANTE_MAGUFULI
#ASANTE_MAMA_SAMIA
#ASANTE_PM_MAJALIWA
#ASANTE_SIMBACHAWENE
#ASANTE_ANGELA_KAILUKI
#ASANTE_WAKURUGENZI_TAMISEMI
 
HIVI NI SEKTA GANI HAPA TANZANIA INAENDESHWA KWA USAWA??
 
Labda tusubiri wiki ya kwanza ya July maana ndio muda mwafaka ambao majina huwa yanatolewa
 
uhamisho ulio ruhusiwa ni wa ndani ya mkoa, japo umeruhusiwa bado makatibu tawala wako slow sana kutoa vibali, kazi mnayo watumishi
 
Samahani kama nitatumia maneno Makali.

1. Mtu anayependa Nyumba ndogo hawezi kupenda kukaa na mkewe / mumewe na hawezi ona umuhimu wa mtu mwingine kuwa karibu na mke / mume wake.

2. Mtu yeyote ambaye hajawahi kukaa au hapendi kukaa na familia yake hawezi kuona umuhimu wa mtu mwingine kuwa karibu na familia yake.
 
Watumishi wa umma hii sio serikali yetu haijawai kusikiliza lolote toka kwetu,nawashauri kuangalia style ya kumwaga ugali maana wao wamemwaga mboga kama hapo ofisini hakuna cha kuiba basi jaribu kuwaibia muda ukafanye mambo yako.
 
Nafkr anaskia waziri wa UHAKIKI, Kazi yake kuhakiki tu hata aibu hana, eti serikali makn lakn ifanye UHAKIKI serikali zilizopta zilikua serikali za hovyo?

Kazi yao kutoa matamko tu kujinenepea! Wanataka kupongezwa na kuombewa tu!

Wanauz mpaka to maximum point!
 
"Tuko katika hatua za mwisho za mchakato wa kuruhusu uhamisho wa watumishi, hivyo tunaomba watumishi walioomba uhamisho na wale watakaohitaji uhamisho kuwa wavumilivu. Na mwezi Julai zoezi litaanza rasmi"(In Suleiman Jaffo's voice).
Mwafwaaaaaaaa.
Hili siri *****kali bwana usitegemee kitu kizuri.
 
Da wengi tunaumia na hii issue....hakika ingelikuwa mi ndo nataka nimfuate mke wangu hakika leo nisingekuwa kwenye huo utumishi...but mpango ni mke anifuate as kuna uwekezaji tayari umefanyika
 
f1d54dfddff6ad3bb65ced95c4377b54.jpg

mkuu hukufanikiwa kuiona hii
 
ww jamaa uhamisho umefungulia toka wiki iliyopita na vibali vimeanza kutoka onana na Afisa utumishi wako aku update
 
Back
Top Bottom