TAMISEMI, pesa za fidia ya ada idara ya sekondari hazitoshi; elimu ya bajeti ya mwaka kwa kila shule inahitajika

Kijana ushe2

Senior Member
Apr 6, 2017
176
122
Wanajamvi habari za leo,

Poleni kwa majukumu na mihangaiko ya kulipambania taifa letu pendwa la Tanzania. Mnaomba niende moja kwa moja kwenye lengo la kuandaa huu uzi kuhusu elimu katika sekondari. Naomba wizara zinazohusika ziweke mikakati imara ili waweze kuzidhibiti shule za serikali:

Moja, kila shule iwe na bajeti kamili ya mwaka wa masomo na so kuangalia idadi ya wanafunzi tu maana kuna shule zina bajeti bubu yani husubiri pesa na kuzitumia bila kujali mpaka zinamaliza mwaka kwa madeni(mikopo) kitu ambacho ni cha ajabu sana na hapa lazima ubadhirifu wa mali za umma uwepo.

Naomba wizara husika hapa ziwe macho sana na zisisitize bajeti iwepo kabla ya Matumizi. Wao wanakupatia mapato na matumizi ya mwaka wa fedha kitu ambacho ni virahisi mtu kutengeneza.

Pili, naomba serikali iweze kusambaza umeme kwa shule zote nchini na pia zitafute wafadhili wazisaidie hizi shule kununua mashine za kuchapishia mitihani ya shule na kazi zingine za taasisi.

Tatu, serikali izifuatilie shule hizi changa kwa undani zaidi zinahangaika mno ikiwezekana wawe wanapewa walimu motisha kwa kuangalia mazingira na mahali shule ilipo!

Kwa leo ni hayo tu

Mtaaluma anaeipenda nchi yake

Karibuni MOYOWOSI!
 
Hivi gharama za ada, chakula na malazi kwa hawa watoto wetu waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya kati badala ya kidato cha tano zitabebwa na mzazi au serikali?
Mfano mimi mwanangu amechaguliwa CBE Dodoma
 
Back
Top Bottom