Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 2,343
- 3,521
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ilitoa fursa kwa wahitimu wa kidato cha nne wa mwaka 2023 kubadilisha machaguo yao ya masomo wanayotarajia kusoma wanapoendelea na elimu ya juu baada ya kuongeza tahasusi 49.
Mabadiliko hayo yatagusa tahasusi 'kombinesheni' za kidato cha tano na kozi za vyuo vya ualimu, vyuo vya kati na elimu ya ufundi kwenye mfumo wa kieletroniki ili kufanya marekebisho ya machaguo kulingana na ufaulu walioupata. Waziri Mchengerwa alidai kuwa,”mchakato huu utaanza Machi 20, 2024 utahitimishwa Aprili 30, 2024 utatoa fursa ya wanafunzi kufanya mabadiliko ya machaguo, tahususi au kozi kwa njia mtandao. Kitaalamu mpango wenu umedumu kwa muda wa miezi minne tu kabla ya wenyewe kudai kuwa kuna changamoto katika Utekelezaji.
Mabadiliko ya sera ya elimu ya mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 na mitaala ya elimu kwa kidato cha tano yameanza kutekelezwa ikiwamo uanzishwaji wa tahasusi mpya 49 kutoka 16 zilizokuwapo awali. Serkali mmewahi kwenda kwenye shule na kuzungumza na wanafunzi kuwauliza je kuna haja ya kuongeza combination mpya za ajabu ajabu, eti kuna French, Arabic na Chinese hii combination ina manufaa yapi kwa mtoto wa Mtanzania abaye anatoka Nayumbu anakuja Nsumba kusoma kidato cha tano? Elimu imekuwa sandakalawe, walio na elimu ndo wanatuvuruga barabara ni kama chuki kuwa tusifike alipo yeye. Nchi ina maprofesa na wataalamu ila wote wameziba masikio kama hawaoni mambo yanayoendelea.
Tamisemi ilitoa fursa hiyo ikiwa imezingatia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la mwaka 2023 na mitalaa ya elimu kwa kidato cha tano, inayoelekeza kuanza utekelezaji wa mafunzo ya elimu ya amali. Je mlifanya upembuzi yakinifu kama ya kuanza kutumia rasimili mali za umma kupoteza muda? Waziri wa Tamisemi, Mohamed Mchengerwa alitangaza fursa hiyo leo Machi 20, 2024 amesema, "utekelezaji huo umehusisha uanzishaji wa tahasusi mpya 49, kutoka 16 zilizokuwepo awali hadi kufikia tahasusi 65." Tunatakiwa kuanza na huyu, kwanini atuongopee watanzania kwenye mpango kuhusu Maisha ya watoto wetu?
"Ukweli ni kwamba wakati wa ujazaji wa fomu za machaguo ya awali tahasusi mpya 49 hazikuwepo kwenye orodha ya machaguo na pia matokeo ya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne hayakuwa yametoka kumwezesha mwanafunzi kuwa na machaguo mazuri zaidi kulingana na ufaulu wake. Serious kabsa waziri unazungumza upupu kiasi hichi, eti kuna combination ya Economics, Business Studies and Islamic Knowledge (EBuI), yaani mtoto akasome Uchumi, biashara na elimu ya Kiislamu?! Mpo serious kabsa!? Kiswahili, Textile and Garment Construction and Fine Art (KTeFi), aisee, Tamisemi na Wizara ya Elimu mnawaletea watanzania hivi tu kwa kuwaaminisha vitakwenda safi kumbe ni uongo.
Juzi mnakuja na libarua lenu eti kuahirisha Utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa wa kidato cha tano mwaka wa masomo 2024/2025, Yaani nimesoma baru hiyo mpaka nimecheka kama mazuri, kipindi mnaanza kuwaaminiha watanzania wachache kuwa mpo na mango bora wmkiwa na hizi combination zaidi ya 60, kuna kundi la wadau Hodari waliwaambia kuwa muache kukurupuka na kupoteza rasilimali za wazazi kwa watoto wao, ila mkashupaza shingo, haya sasa mmevunjika kwa aibu. Richard Mabala alizungumzia hili suala kuwa je mmejiandaa, ila mkakaa kimya kwa kuwa nyie wajuaji. Leo kiko wapi!?
Wakati mwingine fanyeni kuwa wapole na kusikiliza wadau kwa unyenyekevu nyie ni viongozi sio watawala, Benjamin Franklin aliwahi kusema 'If you fail to plan, you are planning to fail'. Shirikianeni na wengine mpate mawazo mazuri.
SIO KWA UBAYA!