TAMISEMI: Mwanafunzi mmoja atatumia kitabu kimoja

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu imesema imetenga Shilingi Bilioni 50 kwenye Bajeti ya mwaka 2021/22 kwa ajili ya kununua Vitabu vya Kiada kwa wanafunzi wote wa msingi na Sekondari Nchini.
.
Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo alipokua akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bugumbikiso Kata ya Chifunfu Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema walipolalamikia uhaba wa vitabu shuleni hapo, ambapo amesema kupatikana kwa vitabu hivyo kutasaidia kila mwanafunzi kupata kitabu chake mwenyewe sawa na muongozo unavyotaka wa kitabu kimoja kwa Mwanafunzi mmoja yaani 1:1.
 
Inabidi waongeze na walimu sasa.
Kuna shule huku vijijjini ndanindani zina walimu wachache,nyingine wawili,watatu wanne,na wakati mtaani Kuna kontena la walimu hawana ajira.
 
Ngoja tusubiri tuone.

Hivi Angela Kairuki siku hizi yuko wapi yule mama alikuwa na kamba nyingi.
 
Kwa Tz hy kitu haitokaa itokee, ni bora hizo pesa wawekeze kwenye miundombinu ya shule mfano ujenzi wa madarasa, madawati nk
 
Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Ummy Mwalimu imesema imetenga Shilingi Bilioni 50 kwenye Bajeti ya mwaka 2021/22 kwa ajili ya kununua Vitabu vya Kiada kwa wanafunzi wote wa msingi na Sekondari Nchini.
.
Mhe.Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo alipokua akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bugumbikiso Kata ya Chifunfu Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema walipolalamikia uhaba wa vitabu shuleni hapo, ambapo amesema kupatikana kwa vitabu hivyo kutasaidia kila mwanafunzi kupata kitabu chake mwenyewe sawa na muongozo unavyotaka wa kitabu kimoja kwa Mwanafunzi mmoja yaani 1:1.
Kwani hamuwezi kununua kabisa afu ndo mnakuja kutuambia, pumbavu ninyi ni lini mmeteleleza ahadi.
Mlisema mnalipa malimbikizo tunayowadai kabla ya julai wapi mmetekeleza..
Mkasema kuna punguzo la kodi kwa watumishi 1% mmeongeza 2500.
Mnapenda sana sifa nyie
 
Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu imesema imetenga Shilingi Bilioni 50 kwenye Bajeti ya mwaka 2021/22 kwa ajili ya kununua Vitabu vya Kiada kwa wanafunzi wote wa msingi na Sekondari Nchini.
.
Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo alipokua akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bugumbikiso Kata ya Chifunfu Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema walipolalamikia uhaba wa vitabu shuleni hapo, ambapo amesema kupatikana kwa vitabu hivyo kutasaidia kila mwanafunzi kupata kitabu chake mwenyewe sawa na muongozo unavyotaka wa kitabu kimoja kwa Mwanafunzi mmoja yaani 1:1.
Joining Instruction zote za F5 2021 moja kati ya mahtaji ya shule ni vitabu vya kiada. Hiyo bajeti itaanza kutumika lini?
 
Back
Top Bottom