Tamisemi lipeni mishahara ya walimu jamani!

Komando tamimy

Senior Member
Nov 18, 2020
108
121
Kumekuwa kuna mambo mengi yanafichwa fichwa lakini madhara yake ni makubwa na miongoni mwa mambo ambayo mhe: Rais wetu aliyoyaongea alisema wizara hazi-communicate.

Unajua kila kitu kikimsubiri rais ndo aje afanye maamuzi kuna hakuna haja ya kuweka mawaziri kwani kazi yao kubwa imekuwa ni kusifia tu mpaka wewe ambaye unamsikiliza unaona aibu. Juzi nimeskia mhe jafo kwenye uzinduzi wa daraja la kijazi. Daaahh nikaisi sasa IQ yetu ina matatizo. Nakumbuka tulimsema sana JK hapa jukwaaani lkn tulikuwa tumeshau kumbe yeye ndo alikuwa amembeba akili za mawaziri wake.Unapokuwa waziri unatakiwa uwe mbunifu na ufanye kazi kwa weledi na si kazi ya kusifia tuu mpaka unatia kinyaaa.

Mimi nilidhani baada ya ushindi wetu wa kishindo na kuwashinda wale waliotuchelewesha kwenye maendeleo sasa Nchi itakimbia na mambo yatakuwa pouwa.Nimasikitiko makubwa mno waalimu walioingiaa kazini tangu tarehe mosi mwezi 12 hawajalipwa mshahara wa mwezi wa 12, 1 na wa2. Hivi Tamisemi kuna shida gani? Kwanini inashindwa kuwasiliana wizara ya fedha (hazina) ili waalimu hawa waingizwe kwenye mfumo wa malipo ya mishahara(payroll).

Nimejaribu kulifuatilia hili mpaka tamisemi zaidi mara 5 majibu unayojibiwa ni kwamba mara waziri wa mambo ya fedha ni mgonjwa naye ndio authorizing officer.

Mara ya pili tunahakiki TIN kwa walimu walioko kazini majibu ya mara pili.

Mara ya tatu nilijibiwa tunaondoa waalimu waliodanganya masomo katika uombaji wa ajira.

Jibu la nne ambalo lilinikatisha tamaaa kabisa ni nilijibiwa wanaajiri walimu wengine 5000 ili wakianza kulipa mishahara walipe kwa pamoja.

Niliwaambia kitu ki1 kwamba hebu na wewe fikiria kama ndo ungekuwa wewe uko kazini unafanya halafu hupewi mshahara ingekuwaje,? Ungeishije?! Rais kila siku anawazungumzia wanyonge, wanyonge wakubwa ni hawa au mpaka yafike kwa raisi?walipeni waalimu mishahara yao.Waalimu ni watu muhimu katika jamii wasidharauliwe.

Mzee Hasanali
Kada mkongwe
Kwa sasa niko KATAVI -MPIMBWE
 
Huo ni mwanzo tu. Mkianza kulipwa kila mwezi, mjiandae pia kwa makato ya 15% kutoka Bodi, 2% kutoka CWT! Halafu Bayport na Platinum watakuwa wana wamendea kwa mbaali ili wawaingize kwenye mikopo yao yenye riba 300%!

Kiufupi tu kazi ya ualimu ni ngumu sana! Utaandika lesson plan isiyo na tija wala umuhimu wowote ule kwa miaka yote ya utumishi wako, madaraja yatapanda kwa kusua sua iwapo huyu mzee atamuiga rafiki yake PK au Mu7 kutawala milele,nk!!
 
Walimu ni lazima wapigwe! IQ yao IPO near to madness. Let's them die alone. Siwezi kumsikitkia mwalimu aliyehujumu uchaguzi
 
Walimu ni lazima wapigwe! IQ yao IPO near to madness. Let's them die alone. Siwezi kumsikitkia mwalimu aliyehujumu uchaguzi
#THE LOST na unaroho mbaya kama jina lako. Hawa hawakuhusika kwenye uchaguzi tunsongelea waalimu walioanza kazi
 
Hao wanaolia ni wapuuzi sana, wasubirie serikali bado inajipanga, au kama vipi wakiona hali ngumu wanaweza kuacha kazi tu.
 
Back
Top Bottom