TAMISEMI: Kuna upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi, hisabati 17,354

TAMISEMI: Kuna upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi, hisabati 17,354

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
SERIKALI imesema mahitaji ya walimu wa masomo ya sayansi na Hisabati ni walimu 47,354, waliopo ni 30,044 na upungufu ni walimu 17,312.

Hayo yameelezwa leo bungeni Mei 29,2025 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Zainabu Katimba wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,Shally Raymond(CCM) ambaye alitaka kujua Je, kuna Walimu wangapi wa masomo ya Hisabati na Sayansi na kuna ziada au upungufu wa Walimu wangapi katika Shule za Msingi na Sekondari.

Akijibu Naibu Waziri Katimba amesema Serikali inatambua changamoto ya upungufu wa walimu katika shule za msingi na sekondari. Serikali imekuwa ikiajiri walimu wa kada mbalimbali ikiwemo walimu wa masomo ya sayansi kadiri ya upatikanaji wa fedha.

Amesema Mahitaji ya walimu wa masomo ya sayansi na Hisabati ni walimu 47,354, waliopo ni 30,044 na upungufu ni walimu 17,312.

Aidha kuhusu shule za msingi amesema amesema mahitaji ya walimu ni 298,687 waliopo ni 173,861 na upungufu 124,826 akisema serikali itaendelea kuajiri walimu ikiwemo wa masomo ya sayansi kadiri ya upatikanaji wa fedha.

 
waajiri tu yeyote!!! Hata hao wa masomo ya art, kibongobongo sayansi wanaweza fundisha!!! Waache janja janja👿
 
Back
Top Bottom