FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 40,530
- 46,614
Maisha hayana formula, nimekuta mtu kaniibia pesa nikapandwa na hasira, kwahiyo nikae kimya kisa wewe umesema nikiwa na hasira nikae kimya? Pathetic absurdity!
Kwahiyo huwa mnashindana kupata like nyingi?Kuna watu wamenizidi mkuu
Kwahiyo huwa mnashindana kupata like nyingi?
asante sana. Hasa namba 11 ni ya kuzingatia sana.Habarini wanaJamii.
kuna msemo wa unesema "silence is the best answer too" tafasiri "ukimya ni jibu sahihi pia" basi twendeni moja kwa moja kwenye hoja ili uweze kutambua muda wa kukaa kimya kwajili ya kujilindia heshima yako ,kulinda heshima za watu wengine na kuepusha mikwazano .
1. kaa kimya ukiona umepandwa na hasira.
2. kaa kimya kama hauna vielelezo(facts) vilivokamilika kuhusu unachotaka uzungumze.
3. kaa kimya kama hujathibitisha stori au kitu unachotaka uzungumze.
4. kaa kimya kama maneno yako yatamvunja moyo mtu aliedhaifu.
5. kaa kimya kama ni muda wa kusikiliza unachoambiwa au kinachoongelewa.
6. kaa kimya kama utaona maneno yako yatadharau vitu vitakatifu kama imani au dini ya mtu.
7. kaa kimya kama utashawishika kuleta utani uliojaa dhambi au usio na maadili mema.
8.kaa kimya kama maneno yako yatakufanya udharaulike baadae au mbeleni.
9.kaa kimya kama maneno yako yataleta maana tofauti kwa mtu au watu unaoongea nao.
10. kaa kimya kama habari au jambo halikuhusu.
11. kaa kimya kama maneno yako yatakua na uongo ndani yake au unashawishika kusema uongo.
12. kaa kimya kama maneno yako yatashusha heshima ya mtu mwingine.
13. kaa kimya kama maneno yako yatapelekea kuvunjika kwa urafiki au undugu.
14. kaa kimya kama upo kwnye hali mbaya hasa kimawazo au kama hujui unachotaka kukisema.
15. kaa kimya kama huwezi ongea kitu bila kupayuka kwa sauti kubwa au kwa ustaarabu.
16. kaa kimya kama maneno yako hayataleta picha nzuri kwa Mungu wako,marafiki zako na familia yako.
17.kaa kimya kama baadae utaona ni sahihi usingeongea ulichokiongea.
18. kaa kimya kama umeshasema kuhusu hicho kitu zaidi ya mara moja.
19. kaa kimya kama unaona maneno yako yatamtibua mtu mkorofi asie na adabu na mpumbavu.
20. kaa kimya kama ukiwa unafanyia kazi unachotaka kukisema.
"yoyote atakae chunga ulimi na mdomo wake atajiepusha na balaa" -zaburi 21:23.
yaap kama huna ushahid bora unyamaze kama una ushahid na vielelezo vyotr paza sautYawezekana huu ni utanzania zaidi. Ndo maana sehemu nyingi tunapigwa eg madini,escrow nk. Woga,woga,woga. Mfano kuna mtu alisema, Tanzania itaanza kuikopesha Ulaya hivi karibuni! So, kwa vile hujui ni kweli au uongo,basi tuwe kimya?
unaongea lkn ucwashushie heshimaLeo nilikuwa sehemu... nimekaa nasubir simu yangu ipate moto ili maisha yaendelee nilikaa na mapolisi wanaongea upuuzi kuhusu uchaguzi wa kinondoni ningekaa kimyaa.hapana niliwapa elimu ya iraiya. Nipo na ndugu mmoja ofisini anaongea ujinga nimwache
una uhakika kaiba pesa kama una uhakika unaweza ongea kama hunahisi tu nyamazaMaisha hayana formula, nimekuta mtu kaniibia pesa nikapandwa na hasira, kwahiyo nikae kimya kisa wewe umesema nikiwa na hasira nikae kimya? Pathetic absurdity!
asante sana mkuuNimekuelewa Sana Mleta Mada
asante sana mheshimiwaUbarikiwe.
hahahaKwa hayo ya hapo juu utaongea muda gani sasa?