Tambua muda wa kukaa kimya

Tambua muda wa kukaa kimya

Kwa akina sisi kuongea ndo tiba.... Eti unikere nikae kimya mpaka hasira ziishe Hapana..... Nitaongea mpaka .

No 20 ,18 Sawa 15 nitapasuka.... 14 sijui 13 bora uvunjike kuliko kuletewa ujinga... 12 ndo -sawa napenda ili ajifunze siku nyingine ...11,10,9 Sawa..... 8 inategemea...
Yani hapo wawili. Nikae kimya au nilie. Ila siwezi kukaa kimya nitakupa linalokustahili tu
 
hapo zinategemeana ukiwa na hasira ukitaka kuonngea bas ongea ktu ambacho bdae hutojutia kukiongea
 
Sawa

Are u a good samaritan yule wa kwenye bible?

Sijui kama ntakua kama huyo Msamaria wa kwenye Biblia ila siku zote haya ndio maombi yangu..

“Uniondolee ubatili na uongo, Usinipe umasikini wala utajiri, Unilishe chakula kilicho kadri yangu, Nisije nikashiba, nikakukana, Nikasema Bwana ni nani? wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Bwana Mungu wangu.”

Mit. 30:8-9
 
Maneno mazuri. Yafanyie kazi hakika utabarikiwa
 
Yani hapo wawili. Nikae kimya au nilie. Ila siwezi kukaa kimya nitakupa linalokustahili tu

Hapo tu ndio unaponiangusha, ukae kimya au ulie, ila hauwezi kukaa kimya, inamaana hapo nilazima uteme nyongo. Ila unaweza kujifunza kumpa mtu linalomstahili kistaarab, wachache sana wanaweza kufanya hilo wakiwa na hasira. Tunaendelea kujifunza lakini, sio jambo rahisi. Hii mada imenikumbusha mambo mengi sana ya muhimu
 
Mi nalitemaga kistaarabu ila litakuchoma. Kwanza mara nyingi nagombana na bf wangu sasa yeye ndo nampaga maneno hadi akikaa ananiambia ila beb ulinipa maneno makali hadi nikajishtukia.
 
Kama unatema nyongo kistaarab sio mbaya, maneno yanaumiza na kuchoma sana. Kuna mambo unaweza kuambiwa kila ukiyakumbuka unachukia kila kitu. Usimchokoze sana mgombea mwenza, mpe maneno kistaarabu!
 
Yeye ndo anakua ananichoza. Nikiongea anasema sina dogo.
 
Habarini wanaJamii.

kuna msemo wa unesema "silence is the best answer too" tafasiri "ukimya ni jibu sahihi pia" basi twendeni moja kwa moja kwenye hoja ili uweze kutambua muda wa kukaa kimya kwajili ya kujilindia heshima yako ,kulinda heshima za watu wengine na kuepusha mikwazano .

1. kaa kimya ukiona umepandwa na hasira.

2. kaa kimya kama hauna vielelezo(facts) vilivokamilika kuhusu unachotaka uzungumze.

3. kaa kimya kama hujathibitisha stori au kitu unachotaka uzungumze.

4. kaa kimya kama maneno yako yatamvunja moyo mtu aliedhaifu.

5. kaa kimya kama ni muda wa kusikiliza unachoambiwa au kinachoongelewa.

6. kaa kimya kama utaona maneno yako yatadharau vitu vitakatifu kama imani au dini ya mtu.

7. kaa kimya kama utashawishika kuleta utani uliojaa dhambi au usio na maadili mema.

8.kaa kimya kama maneno yako yatakufanya udharaulike baadae au mbeleni.

9.kaa kimya kama maneno yako yataleta maana tofauti kwa mtu au watu unaoongea nao.

10. kaa kimya kama habari au jambo halikuhusu.

11. kaa kimya kama maneno yako yatakua na uongo ndani yake au unashawishika kusema uongo.

12. kaa kimya kama maneno yako yatashusha heshima ya mtu mwingine.

13. kaa kimya kama maneno yako yatapelekea kuvunjika kwa urafiki au undugu.

14. kaa kimya kama upo kwnye hali mbaya hasa kimawazo au kama hujui unachotaka kukisema.

15. kaa kimya kama huwezi ongea kitu bila kupayuka kwa sauti kubwa au kwa ustaarabu.

16. kaa kimya kama maneno yako hayataleta picha nzuri kwa Mungu wako,marafiki zako na familia yako.

17.kaa kimya kama baadae utaona ni sahihi usingeongea ulichokiongea.

18. kaa kimya kama umeshasema kuhusu hicho kitu zaidi ya mara moja.

19. kaa kimya kama unaona maneno yako yatamtibua mtu mkorofi asie na adabu na mpumbavu.

20. kaa kimya kama ukiwa unafanyia kazi unachotaka kukisema.

"yoyote atakae chunga ulimi na mdomo wake atajiepusha na balaa" -zaburi 21:23.
Yawezekana huu ni utanzania zaidi. Ndo maana sehemu nyingi tunapigwa eg madini,escrow nk. Woga,woga,woga. Mfano kuna mtu alisema, Tanzania itaanza kuikopesha Ulaya hivi karibuni! So, kwa vile hujui ni kweli au uongo,basi tuwe kimya?
 
Habarini wanaJamii.

kuna msemo wa unesema "silence is the best answer too" tafasiri "ukimya ni jibu sahihi pia" basi twendeni moja kwa moja kwenye hoja ili uweze kutambua muda wa kukaa kimya kwajili ya kujilindia heshima yako ,kulinda heshima za watu wengine na kuepusha mikwazano .

1. kaa kimya ukiona umepandwa na hasira.

2. kaa kimya kama hauna vielelezo(facts) vilivokamilika kuhusu unachotaka uzungumze.

3. kaa kimya kama hujathibitisha stori au kitu unachotaka uzungumze.

4. kaa kimya kama maneno yako yatamvunja moyo mtu aliedhaifu.

5. kaa kimya kama ni muda wa kusikiliza unachoambiwa au kinachoongelewa.

6. kaa kimya kama utaona maneno yako yatadharau vitu vitakatifu kama imani au dini ya mtu.

7. kaa kimya kama utashawishika kuleta utani uliojaa dhambi au usio na maadili mema.

8.kaa kimya kama maneno yako yatakufanya udharaulike baadae au mbeleni.

9.kaa kimya kama maneno yako yataleta maana tofauti kwa mtu au watu unaoongea nao.

10. kaa kimya kama habari au jambo halikuhusu.

11. kaa kimya kama maneno yako yatakua na uongo ndani yake au unashawishika kusema uongo.

12. kaa kimya kama maneno yako yatashusha heshima ya mtu mwingine.

13. kaa kimya kama maneno yako yatapelekea kuvunjika kwa urafiki au undugu.

14. kaa kimya kama upo kwnye hali mbaya hasa kimawazo au kama hujui unachotaka kukisema.

15. kaa kimya kama huwezi ongea kitu bila kupayuka kwa sauti kubwa au kwa ustaarabu.

16. kaa kimya kama maneno yako hayataleta picha nzuri kwa Mungu wako,marafiki zako na familia yako.

17.kaa kimya kama baadae utaona ni sahihi usingeongea ulichokiongea.

18. kaa kimya kama umeshasema kuhusu hicho kitu zaidi ya mara moja.

19. kaa kimya kama unaona maneno yako yatamtibua mtu mkorofi asie na adabu na mpumbavu.

20. kaa kimya kama ukiwa unafanyia kazi unachotaka kukisema.

"yoyote atakae chunga ulimi na mdomo wake atajiepusha na balaa" -zaburi 21:23.
Leo nilikuwa sehemu... nimekaa nasubir simu yangu ipate moto ili maisha yaendelee nilikaa na mapolisi wanaongea upuuzi kuhusu uchaguzi wa kinondoni ningekaa kimyaa.hapana niliwapa elimu ya iraiya. Nipo na ndugu mmoja ofisini anaongea ujinga nimwache
 
Back
Top Bottom