Mi niko ndani we ni mlinzi, ingia kwenye gemu we ni mshindani mi ni mshindi/
Ukiniona sizi usinichukulie kipimbi, wakati kitaani master naheshimika kama dingi/
Mi ni mfanya kazi we ni kazi nakufanya, hazichaniki maana hauna hadhi ya kuchana/
Tahadhari changa rambi rambi na dhamana, yakua ukaishi kwenye kambi za lawama/
Kule siskiki sishawishiki, kusaliti we ni mwanafunzi mi ndo shule ya muziki/
We ni mume mbona mke halidhiki, unajiita mcee na bado uko nje ya msingi/
Mi kibaka we ndo shingo ya kabali, mi ndo driver we ndo konda au tingo kwenye gari/
We kapuku mi na' bingo la mistari, ogelea kote dizasta ndio kingo za bahari/
Mi ndo tungo shazi nazisuka kama jamvi, we ndo pusha zungusha mi ndo mzuka kwenye nyasi/
Najua ku rythms ma mcee wanajua nini, vilio kila masta navyotua kwenye scene/
Nina mama bora,mama nuru,mama funzo, we ni mtumwa kwenye soko niko huru kwenye tungo/
Tukirudi class we ni good mi ni better, mulize kingo kitaani mi ni babuu we ni sheta/
Wauza sura wana ghani tu majina, wao majini kama kabula mi ndo shetani la vina/
Mi nimenuna bwege cheka na hii vocal, beat tope na dizasta mi ndo mega mining volvo
Mi ndo folder, mi ndo hoja, mi ndo mada kwenye somo kwenye jeshi mi ni soldier
Mi ndo muosha naogesha midundo, niite dizasta wananiita profesa tungo