Vesper-valens
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 5,380
- 7,572
- Thread starter
- #61
Ni upuuzi wa kiwango cha SGRTamaduni wabadilike kifikra. Kuendelea kung'ang'ania muziki ambao hauhitajiki sokoni ndo anguko lao. Hata wanamuziki wa Congo baada ya kuona wanapotea wameamua kubadilika.. zamani walikuwa wanatoa nyimbo ndefu za hadi dakika 10 ila siku hizi na wao wanatoa nyimbo za dakika 3 hadi 4. Na yale masebene wamepunguza. Kina Pepe Kale wakifufuka watashangaa sana kuona Werrason katoa wimbo wenye verse ya Hiphop. Wacongo pia walikuwa ni wabishi mno kupiga bila vyombo lakini siku hizi nao kuna matamasha wanapiga bila vyombo ili mradi mkono uende kinywani. Kimsingi muziki una mabadiliko dunia nzima. Tamaduni wao wakubali kubadilika na kuacha UJEURI. Kujifanya unasimamia misingi ya Hiphop huku unazidi kutumbukia kwenye umaskini ni upuuzi mtupu.