Tamaa za maisha zinavyowapoteza mapunda wa madawa ya kulevya

Toxic Concotion

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
5,667
20,360
Inasikitisha kuwa vijana hawajifunzi kila siku kupelekea kurudia makosa hayo hayo.

Imekuwa mtindo sasa vijana kuwekwa rehani kwa suppliers wa madawa ya kulevya Pakistan na Iran na 'matajiri' kuchukua mzigo kwa mali kauli.
Mwisho wa siku waliowekwa rehani wanatalekezwa, waliochukua mali maisha yao yanaendelea kwa raha uraiani.

Kuna haja serikali ikawa strict zaidi hasa kwa hao wanaoweka wenzao rehani na kuwatelekeza. Wakigundulikana wachukuliwe kama wauaji tu.

View attachment 2482381
View attachment 2482382
Tamaa mbele Mauti nyuma!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Ukute walitamani maisha ya wauza unga wakaaminishwa kuwa wakiwekwa rehani na wao watakuwa ma don kutokujua ma don wanatajirika kupitia majuha kama wao.

Leo wananing'inizwa kama mbuzi machinjioni na pengine wakiachiwa wasipewe hata mia.
Na hamna kingine hapo Mkuu zaidi ya hilo kujua wakitoka hapo na wao wametusua.

Sema nini kutokana na hizi video wa kujifunza watajifunza.
 
Hi vita ni nzito tofauti na tunavyodhani.
Mtandao wa wauzaji ni mkubwa sana na unanguvu kubwa pia wengi wanashawishika na malipo wanayoahidiwa. Tuwalee watoto wetu katika njia ya kumhofia mwenyezi Mungu
 
Hilo la malezi ndio la muhimu.
Kuna haja kila mzazi kumfunza mwanae kuwa hakuna fedheha katika umaskini.

Tatizo kubwa tunaaminisha watoto zetu kuwa utajiri ndio kila kitu kutokuanisha njia za kupata utajiri huo.

Pia wazazi tunachangia madhila ya waoto wetu kwanza kwa kuwawekea matarajio makubwa ya kutoka kimaisha na pili kutokuhoji pale panapokuwa na mabadiliko ya kiuchumi kwa watoto wetu.

Baba akipewa pesa kidogo na mwanae anaona ni sawa kutokuangalia chanzo cha mabadiliko ya ghafla ya kipato cha mtoto wake.
 
Back
Top Bottom