Uraibu si kwa madawa ya kulevya pekee

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,883
2,765
Habari wakuu

Kuna hii dhana kwamba kuwa teja hadi uwe unatumia madawa ya kulevya pekee. Tena madawa yenyewe bangi haipo kivile. Uwe unatumia cocaine, heroine na mengine ya jamii hiyo ndio utaitwa teja pale ambapo yamekuzidia na huwezi fanya jambo bila kujidunga hayo.

Huo ni uongo. Mateja wapo wengi sana katika sekta na viburudisho mbalimbLi.

Siku hizi kuna hizi energy drinks. Mtu kwa siku lazima anywe. Wengine mbili na zaidi na bila ya hivyo hajisikii vyema. Tena mtu huyu hujisifia waziwazi. Huyu ni teja. Najua mko wengi

Wapo wale wa soda. Mwingine anasema nikokosa p***i asubuhi kazi haziendi. Natetemeka mwili, tena anajisifia. Huyu nae teja. Anajiandalia mazingira ya kisukari tu

Mwingine pombe. Kwenye pombe wako wengi na tunawaona. Mbaya zaidi zipo pombe za kienyeji zenye kuuzwa kwa bei chee na zenye kilevi asilimia kubwa sana. Tunaona mikoani huko vijana wanateketea. Hawazalishi mali wala hawazalishi wanawake. Kwisha kabisa. Kwenye maafisa usafirishaji nako janga maana ni vijana na wananunua pombe za bei chee zilizohalalishwa kisha wanapanda boda zao kuingia kazini. Hao wote ni mateja.

Wapo mashoga na wasagaji. Huku usiseme. Hawa wako kundi moja na wale wa madawa ya kulevya. Uraibu wao ni wa kificho kificho japo kwa sasa wanatengenezewa majukwaa ya kuradimisha jambo lao. Bado kwa vyovyote ni uraibu maana wapo wanaotaka kuacha na wanashindwa kwa utashi wao. Nao ni mateja

Wapo wapenda ngono; wanawake kwa wanaume. Tofauti hapa mwanaume ataitwa kipanga na mwanamke ataitwa malaya. Mtu hawezi kaa wiki moja bila ngono na yuko radhi kujichua kukidhi haja. Hawa nao ni mateja.

Yapo mazingira mengi sana yanayopelekea watu kuwa waraibu katika jambo fulani. Mengine mtaongezea. Hoja yangu ni kwamba, tusithubutu kuwanyooshea vidole vya kejeli hawa watu. Mtu yoyote na kwa wakati wowote anaweza kuangukia kwenye uraibu wa aina fulani. Tena asijisifu kuwa uraibu wangu si sawa na wa yule. Wewe ni teja tu

Muhimu ni serikali na jamii kutazama kile kinachowezekana na kutafuta tiba, ziwe za muda mfupi au nrefu

Mathalani kwenye unywaji pombe uliopitiliza na unaoatbiri vijana kwa wingi. Pandisha kodi ya hatari sana bei ya hizo pombe iwe juu. Mbona walipandisha bei ya mafuta ya taa kulingana na dizeli na petroli ili kunusuru uchakachuaji. Wanasbindwa nini kunusuru vijana?

Pia kupeleka miradi maeneo husika. Maeneo kama Kilimanjaro vijijini walikuwa wa ategemea kahawa na ndizi. Sasa kabawa ikapotea (sasa naona wanarudisha) hivyo vinana wengi wakawa iddle, na mbaya zaidi wakapelekewa hizo pombe za bei chee zinazowamaliza.

Niishie hapa kwa sasa
 
Walikataza pombe za kwenye viroba, watu wakazalisha zaidi hizi za kwenye makopo.

Ukiongeza kodi utawahamisha kutoka hizo za viwandani mpaka za kienyeji, japo itasaidia kwa wachache ila sio kwa vijijini.
 
Hivi kula kula mara kwa mara nako kunaweza kuwa uraibu? Unakuta watu wanapenda kula chips wasipokula wanajisikia vibaya
 
Kuna wadau kwenye uzi wangu huko wa kuhusu picha za utotoni wametupia koment fupi fupi za nongwa sana kwa kuwa wanapenda vitu vyepesi. Nawakaribisha na huku kutoa michango yao myepesi myepesi as usual
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom