Talaka umetoa wivu wa nini?

Talaka umetoa wivu wa nini?

jembe afrika

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
7,602
Reaction score
3,783
Wakuu nafikiri mko poa kabisa,kuna kitu huwa najiuliza mpaka nimeamua kulileta kwenu.

Kuna rafiki yangu wa siku nyingi sana ana mke na amedumu nae kwenye ndoa zaid ya miaka kumi.

Wamekua na migogoro ya hapa na pale isiyoisha ikafikia mwisho jamaa katoa talaka.

Baada ya miezi minne jamaa kamkuta mke mtalaka wake kakumbatiwa na kidume kingine akaanzisha fujo

Na kumjeruhi huyo jamaa,sheria ikachukua mkondo wake jamaa kafungwa miaka kumi.

Swali langu wivu unatoka wapi wakati mmeachana kwa hiari yenu?
 
Inategemea yawezekana mwanamke ndiyo chanzo cha talaka kwahyo alitaka kulipa kisasi while is not fair!!
 
Huyo ndio wale staki nataka,wanakurupuka kuwacha mke au mke kudai talaka kumbe hajiwezi matokeo yake fedheha,kuchunguza anatoka nanani amerejeshwa nanani....
 
Munkari

unamaana maji hayasahau baridi hata ukiyachemsha vp lazima yapoe?
 
Last edited by a moderator:
WALIMWEUSI

kosa la jinai hilo.kapunguziwa huwa hadi 40
 
Last edited by a moderator:
sheria ya nchi mkuu

Hii ndio Sheria ya Nchi kwa Makosa ya Jinai yanayohusu kujeruhi:

Sheria . Na. 5 ya 1961 kif;8 (228)

Mtu yeyote ambaye
(a) isivyo halali anamjeruhi mwingine ; au
(b) isivyo halali, na kwa kusudi la kumjeruhi au kumuudhi mtu yeyote, anasababisha sumu yeyote au kitu kingine chenye kudhuru kupewe mtu mwingine au kuliwa na mtu mwingine atakuwa anatenda kosa na atahukumiwa kifungo cha miaka mitatu.
 
CHEZEA jembe afrika WW
 
mi ndo habarinilizozikuta kwenye familia yake mkuu
 
Hilo ndilo tatizo la kukimbilia talaka. Mnaposhindwanahatua ya kianzia kuchukua ni kutengana. Hii ina maana hamuendi mahakamani kutafuta talaka bali mume kutoa kibali cha mandishi cha kumruhusu mke arudi na kuishi kwa wazazi hadi mgogoro wao utakapotatuliwa. Hili laweza kufanyika hata kwenye ofisi ya mwenyekiti wa mtaa tu. Hatua hii inawapa fursa ya kuchanganua natatizo yenu na ikibidi kukubaliana kurudiana.
 
Back
Top Bottom