Talaka, ni suluhu ya migogoro ya ndoa?

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Wapendwa,

Nimeiona mada hii ikiendelea kwenye mtandao wa Fikrapevu nikaona si vibaya na sisi pia tukaileta hapa na kuidadavua kwa maslahi ya wana MMU wote.
Je utoaje wa talaka (kwa wanaume)/kuomba talaka (kwa wanawake) kwa wenye ndoa wenye migogoro ni suluhu ya migogoro hiyo?

Maoni yako, pliz.
 
Talaka yaweza kuwa suluhu kwa yale matatizo ambayo yanaondoa mantiki nzima ya ndoa.
Angalizo: ukianza kutoa talaka utaona suluhu ya kila tatizo ni talaka ndani ya ndoa...usiwe mwepesi wa kutoa talaka na kama ikitokea jitahidi hali hiyo isijirudie.
 
inategemea na aina ya matatizo.kama makubwa mno,talaka is the best option.mfano mume au mke imegundulika anataka kumuua mwenzake,mfano umeweka sumu kwenye chakula,au mume kutembea na mtoto wake{kwa upande wangu mimi,hilo halivumiliki}nitamuamini vipi huyo mume tena?au unapigwa kila siku,ukiendelea kukaa mwisho utakuwa kilema.ila matatizo madomadogo unajitahidi kukomaa nayo
 
Hiyo haijakaa sawa hata kidogo (kama kweli hivyo ni ndivyo ilivyo).

Kwa nini mwanaume atoe na mwanamke aombe?
 
Talaka ni kitu kibay Yet sio jibu au suluhu ya migogoro ya kindoa

Matatizo ya ndoa ili yapate majibu ya kweli ni wahusika kukaa na kushughulikia tofauti zao wakimshirikisha Mungu ili shetani asipate nafasi ya kuwapa mafundisho ya uongo kuona kuachana ndio majibu

Hahitajiki mtu wa tatu ktk matatizo ya ndoa

Ni Mungu na WAWILI wahusika
 
Very good.
 
Hata kama mmoja wa hao wanandoa ananyanyaswa? Aendelee tu kuwa kwenye hiyo ndoa hadi atakapopoteza maisha yake au kupata kilema cha maisha?
 
Wapendwa,

Nimeiona mada hii ikiendelea kwenye mtandao wa Fikrapevu nikaona si vibaya na sisi pia tukaileta hapa na kuidadavua kwa maslahi ya wana MMU wote.
Je utoaje wa talaka (kwa wanaume)/kuomba talaka (kwa wanawake) kwa wenye ndoa wenye migogoro ni suluhu ya migogoro hiyo?

Maoni yako, pliz.

Ni last olternative baada ya kutumia njia zote za kusuluhisha na kushikana
 
Ni suluhisho ndio iwapo njia zote zimefail ila kuna kitu kinashangaza, wapo wanawake wanaendelea kuwepo kwenye ndoa yenye mateso kisa wanaume wanagoma kutoa talaka.
 
Hiyo haijakaa sawa hata kidogo (kama kweli hivyo ni ndivyo ilivyo).

Kwa nini mwanaume atoe na mwanamke aombe?

haijakaa sawa kweli, inabidi na wanawake wakiona mambo hayaendi sawa wawape talaka wanaume zao.
 
Talaka ni suluhisho
Talaka ni shule
Talaka ni uhuru
Talaka ni upumbavu

Hayo hapo juu yote ni majibu. Inategemea talaka imetolewa katika mazingira gani.
 
Talaka yaweza kuwa suluhu kwa yale matatizo ambayo yanaondoa mantiki nzima ya ndoa.
Angalizo: ukianza kutoa talaka utaona suluhu ya kila tatizo ni talaka ndani ya ndoa...usiwe mwepesi wa kutoa talaka na kama ikitokea jitahidi hali hiyo isijirudie.

yan hii ni kweli kabisa.kuna mfano hai wa lijanaume limoja ambalo lilifikiri kumwacha mkewe ni suluhisho,yan ss hivi ameacha wanawake hata 20 wamefika.na mbaya zaidi watt wameathirika na kwasasa limefulia mbaya.yan hata hela ya kula ni taabu!
 
As much as TALAKA sio kitu kizuri, Sometimes ni suluhisho..... Kuna vitu havivumiliki jamani.... Kuna vitu vinauma Mno!!!

naomba nikusapoti walau kwa asilimia 51, binafsi natamani kurudi kuwa mtoto.
 
Back
Top Bottom