KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 696
Nakubaliana na wanaosema talaka ni suluhisho la "last resort". Njia nyingine zikishindwa, badala ya kuendelea kuishi katika hali ya kutegana; akikosea nammaliza; basi talaka ndo njia inayopendekezwa na wataalam wengi. Talaka haiepukiki kwenye mahusiano yaliyokwisha haribika na talaka ni suluhu haswaa.
Tatizo wengi wanatoa au kuomba talaka kama fimbo ya kuwachapia wenzao hasa pale wanapoona wenzao hawana kipato cha kuwakidhi pindi ndoa inapovunjika. Haya ni matumizi mabaya. Ila kwa kutatua migogoro iliyoshindikana ni afadhali talaka.