"talaka kwenye ndoa ni haki" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"talaka kwenye ndoa ni haki"

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Dec 17, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Swali walilouliza!

  Wakajikuta swali lao limekosewa! Ni kweli zogo (controversy) au hekaheka kubwa inayowagawa watu katika makundi mawili kuhusu talaka inapatikana katika injili ya Mathayo 5:32 na 19:9
  Kumbuka Injili ya Luka na Marko pia imeripoti tukio la Mathayo 19:9 Yesu alipotegwa swali na Mafarisayo isipokuwa ni Mathayo peke yake ameandika kuhusu exception ya kutoa talaka ambayo ni kosa la uasherati (tutaangalia baadae kwa nini ni mathayo peke yake ameripoti hivyo).

  Kabla ya kufika huko ni Muhimu sana kufahamu mazingira (geography) iliyopelekea Yesu kuulizwa swali na Mafarisayo.
  Tukumbuke kwamba Yesu alikuwa Galilaya na alikuwa amemaliza huduma yake na sasa alikuwa anasafiri kupitia eneo la Perea ili kurudi Yerusalemu kwa ajili ya pasaka (yaani kifo chake).

  Mafarisayo waligundua kiwamba Yesu atapita hilo eneo ambalo kwa wakati huo lilikuwa chini ya himaya ya Herodi.
  Hivyo mafarisayo walijua ni wakati muafaka wa kumuuliza swali (trick question) ili ajichanganye na wapate sababu ya kumuua.
  (kumbuka mafarisayo walikuwa wanamfafuta sana Yesu wamuue ila walikosa sababu au shitaka Mathayo 12:14, Marko 3:6)
  Kwa hiyo mafarisayo walimuuliza Yesu swali ambalo lengo ni kumtega yeye (test) na si kutaka kujua.

  Kumbuka miaka 2 iliyopita Yohana mbatizaji ambaye alimtangulia Yesu alikuwa amefungwa Jela kwa sababu aliongelea suala la talaka ya Herode Antipas ambaye alioa mke wa mdogo wake Filipo ambaye mke wake alitoa talaka kwa mume wake Filipo na kwenda kuolewa na Herodi Antipas (kaka mtu) Soma Mathayo 14:1-12.

  Yohana mbatizaji hakubabaika au kujisikia vibaya kumkemea Herodi na dhambi yake hata kama ni ikulu (Math 14:4) matokeo yake akawa arrested na kutupwa jela na baadae kukatwa kichwa.

  Kwa kuwa Yesu alikuwa anapita maeneo ambayo ni himaya ya herodi Antipas, mafarisayo walijua fika kwamba Yesu atajichanganya tu na jibu la swali watakaloulizwa na atajimaliza kwa kumtaja Herode na dhambi yake ya kuoa mke wa mdogo wake na kama Yohana mbatizaji kwa kutamka tu aliuawa Yesu Je ambaye anapita kwenye himaya yake?

  Swali aliloulizwa Yesu lilikuwa:
  Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote?’

  Kumbuka wakati Yesu yupo duniani talaka ilikuwa inakubalika kutokana na Musa alivyoamuru hata hivyo kulikuwa na gumzo na utata wa sababu ipi hasa mume anaweza kutoa talaka kwa mke au sababu ipi hasa inaweza kupelekea mume kutoa talaka kwa mke wake na kumbuka pia wayahudi walikuwa hawaruhusu mwanamke kutoa talaka bali mwanaume tu.

  Ndipo kukawa na makundi matatu yanayopingana

  KUNDI LA KWANZA – SHAMMAI
  Wao walikubaliana kwamba sababu inayoweza kumfanya mume kutoa talaka ilikuwa ni uzinzi (adultery)

  KUNDI LA PILI – HILLEL
  Wao walikubaliana kwamba sababu inayoweza kumfanya mume kutoa talaka ni pale mke akipika chakula kisichoiiva au kibaya au ovyo.

  KUNDI LA TATU – RABBI
  Wao walikubalkiana kwamba hata mume akikutana na mwanamke mzuri zaidi ya Yule anaye nyumbani basi anaweza kutoa talaka

  Sasa swali kwa Yesu lilikuwa wewe upo upande gani?
  SHAMMAI, HILLEL AU RABBI?

  Yesu alifahamu fika mioyo ya mafarisayo inawaza kitu gani na akawajibu kwa swali (counter attack) kwa kuwauliza tangu mwanzo Mungu alifanya kitu gani kwa ajili ya mke na mume.

  Mafarisayo wakajikuta swali lao limekosewa na kwamba wamekosa point kwani wao walitaka ajibu Kumbukumbu la Torati 24:1-4) na Yeye akajibu Mwanzo 2:24.

  Ikabidi wamrukie kwa swali kuhusu Musa kuruhusu talaka ndipo wakajibiwa kwamba Musa aliruhusu talaka kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao na kukataa kwao design ya ndoa tangu mwanzo na ndipo Yesu akazusha mambo 4 muhimu kabisa

  JAMBO LA KWANZA
  Hapo mwanzo Mungu aliumuumba mwanaume mmoja kwa ajili ya mwanamke mmoja, kama angetaka Adamu awe na wanawake wengi basi angewaumba akina Sandra, Joan, Jane, Linda wakutosha na si Eva peke yake.
  (mwanzo 1:27, 5:2, Marko 10:16)

  JAMBO LA PILI
  Yesu anatia mkazo kwamba ndoa ndicho kifungo (strongest bond) duniani hivyo kabla ya kuingia kwenye ndoa ni muhimu sana anayehusika kufahamu kwamba anaingia kwenye kitu ambacho huwezi kutoka labda kifo kitokee kati ya wawili.
  (Mwanzo 2:24, Marko 10:7)

  JAMBO LA TATU
  Katika ndoa wawili huwa mtu mmoja, mwili mmoja (one flesh)
  (Mwanzo 2:24, Marko 10:8)

  JAMBO LA NNE
  Yesu alithibitisha kwamba Mungu ndiye huwaunganisha wawili wanaooana na kwamba kile Mungu amekitenganisha binadamu asikitenganishe.

  Hivyo swali la mafarisayo
  Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote?’
  Jibu la Yesu ni HAPANA KUBWA
  Na kwamba Yesu hakuwa kwenye kundi lolote iwe SHAMMAI AU HILLEL AU RABBI.

  Yesu alielezea kudumu (permanency) na kutovunjika (inviolability) ya ndoa hadi wanafunzi wakaendelea kumuuliza jioni yake huku wakipendeleza kwamba kama masuala ya ndoa ni hivyo basi ni busara sana mwanaume asioe kabisa.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Ni ngumu sana!

  Kwa wayahudi ni mwanaume tu aliruhusiwa kutoa talaka na si vinginevyo!Suala la talaka ni issue ngumu sana katika nyakati mbali mbali ambazo binadamu amekuwa chini ya uso wa dunia.
  Suala la talaka lilikuwa gumu sana wakati wa Musa.
  Likawa gumu sana kwa mafarisayo hata wakaamua kumuuliza Yesu ingawa wao swali lao lilijikita katika kumtega Yesu na si kuelewa issue nzima ya talaka.

  Suala la talaka ni gumu zaidi leo hadi limepelekea hata watu waliopo kanisani (Christians) kujikuta wamejigawa katika makundi mawili wale wanaokubali na (liberal Christian) wale wanaokataa (conservative Christian) na kila kundi (school) lina maandiko ambayo linasimamia kutoka katika Biblia.

  Issue inakuwa ngumu zaidi kwa kuwa hata tafsiri (translation nyingi mpya za Biblia sasa nimebadilisha baadhi ya maneno ya msingi hata yale yanayohusiana talaka.
  Kwa mfano Mathayo 19:9

  Kiswahili Biblia inasema:
  Mimi nawaambia, ye yote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini." Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini."

  Matthew 19:9 (King James Version)
  And I say unto you, Whosoever shall put away his wife, except it be for fornication, and shall marry another, committeth adultery: and whoso marrieth her which is put away doth commit adultery.

  Matthew 19:9 (New International Version)
  I tell you that anyone who divorces his wife, except for marital unfaithfulness, and marries another woman commits adultery."

  Matthew 19:9 (Contemporary English Version)
  I say that if your wife has not committed some terrible sexual sin, [a] you must not divorce her to marry someone else. If you do, you are unfaithful

  Matthew 19:9 (Worldwide English (New Testament))
  But I tell you this. No man may send his wife away unless she has committed adultery. If he does, and if he marries another woman, he commits adultery. And if a man marries a woman who has been sent away by her husband, he commits adultery.'

  Kutokana na translations za hapo ikitokea kila mmoja akawa na Biblia yake likija suala la talaka (divorce) hawa watu 5 hawatakubaliana kwani Kiswahili tunajua Uasherati(fornication) ni tofauti na uzinzi (adultery) na hata siku moja huwezi kuita zinaa (sexual immorarity au marital unfaithful) au uzinzi (adultery) ni uasherati bali uasherati ni aina ya zinaa.
  Uasherati ni kwa wale ambao hawajaoana na uzinzi ni kwa wale ambao wameoana.

  Kutofahamu maana au tofauti na uasherati na uzinzi husababisha kutoelewa nini Yesu aliongea katika Mathayo 19: 1-10.

  Hata hivyo suala la talaka linaweza kupewa majibu kibiblia na Biblia ipo wazi na inaeleweka kabisa na Yesu mwenyewe alieleweka kabisa kwamba ukishaolewa hakuna kitu kinaitwa talaka isipokuwa kifo
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Wednesday, December 2, 2009
  Maafa ya talaka!

  Talaka ikitolewa huathiri wote hata wale tusiowaona!Mahusiano ni kazi (hardwork), migogoro hujitokeza, msongo wa mawazo haukosekani, matarajio huyeyuka hata hivyo kila mmoja ana ufahamu na uwezo tofauti wa kukabiliana na hizi challenges.
  Jambo moja la msingi ni kwamba matatizo yote ya ndoa huweza kuwa fixed na talaka huweza kuzuilika kama wawili wakiamua.

  Hata hivyo ni muhimu kujua maafa ya uamuzi wa kupeana talaka ili kama unawaza talaka ni muhimu kufahamu ili uweze kubadilisha mtazamo wako ambao unaudanganyifu uliokithiri.
  Moja:
  TALAKA HUVUNJA NYUMBA
  Familia iliyoanzishwa na wawili walioana huharibiwa muda wote ambao wahusika wataishi chini ya jua.
  Kunakuwa na kovu (scar) ambalo huambatana na wahusika na kamwe haliwezi kufutika.
  Talaka huvunja nyumba familia ambayo ingekuwa Baraka kwa mama, baba na watoto/mtoto.

  Mbili:
  TALAKA HUSABABISHA MIOYO KUTOA DAMU (ngeu)
  Talaka haiathiri wahusika tu (yaani mke na mume) bali huathiri familia, ndugu, jamii na taifa kwa ujumla.
  Talaka husababisha marafiki na ndugu kuomboleza kwa machozi ya damu bila kusema lolote.

  Tatu:
  TALAKA HUATHIRI WATOTO
  Watoto huchanganyikiwa na kitendo cha wazazi kuachana na hakuna mtu duniani anayeweza kufahamu ugumu na uchungu ambao huwakuta watoto katika mioyo na akili zao.
  Kila mtoto anaufahamu wa kwamba anahitaji kupata upendo wa baba na mama pamoja na anaona hata kwa watoto wenzake.
  Mtoto huchanganyikiwa mno pale wazazi wakitalikiana.

  Nne:
  TALAKA HUHARIBU USHUHUDA
  Kila anayepewa talaka au kutoa talaka hujiwekea alama (mark/label) katika maisha yake na watu huisoma hiyo alama kwamba "Huyu ni failure" na huweza kusababisha kukosa acceptance kwa watu wengine bila sababu ya msingi, kisa talaka!

  Tano:
  TALAKA NI KUKANA KIAPO
  Wakati wa kufunga ndoa wahusika walitoa ahadi zao (vows) kukubali na kuahidi kwamba wataishi pamoja katika afya na uzima, raha na shida hadi kifo kitakapowatenganisha.
  Walitoa ahadi mbele za Mungu na mashahidi.
  Je, walikuwa hawamaanishi?
  Je, kichwani akili zilihama?
  Je, walikuwa wanatania?
  Je, ilikuwa kweli au uwongo?
  Talaka ni kukana kiapo na pia kuikana Biblia
   
 4. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mamamia, naona leo uko fiti sana kwa mambo ya "ndani ya nyumba" mimi huko ndio fani yangu, natoka kidogo nikapate bia, nikirudi nakujibu kuhusu masuala ya talaka na jinsi Yesu alivyo fundisha. nisemem mapema kuwa naunga mkono talaka japo mimi mwenyewe nimekuwa nikishauri watu wengi kutoyoa talak kwa watu wengine. muhimu ujue kuwa naunga mkono talaka katika mazingira fulaniflani tu. nitafafanua nikirudi,

  usiondoke tafadhari
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  yuko fiti kwa kukopi na kupesti!
  mwambie akupe linksi na wewe uwe unatujazia seva hapa:D

  kinyume na hilo naweza sema unatafuta DHAMANA
   
 6. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli geof. Inaonekana mama 100 ana chukua mahali tena bila ku-digest!

  Nitampa brief:
  Watu wanahimiza sehemu ya pili ya kauli ya yesu isemayo: (mwanadamu asikitenganishe) wanasahau au wanapuuzia sehmu ya kwanza (alichokiunganisha mungu) ili kuhalalisha upinzani wao juu ya talaka. Nasema hapa kuwa, talaka ilizuiwa kwa kile tu "alicounganisha mungu" sasa kama watu wamedanganyana huko (na mungu hafungamani na udanganyifu wala maovu yoyote) au wamepeana mimba chini ya kiapo halafu wakaoana hapo ni sawa na waliotapeliana! (mungu hakai kwenye utapeli). Kwa watu kama hao talaka ni ruksa endapo hawatakuwa tayari kuishi kwa amani a mungu. Lakini wakisameheana na kurudiana kwa mapenzi mapya ya kweli na haki, mungu ni mwema, huamrisha malaika zake kufurahi na kushangilia kwa ajili yao!!!!!!

  Kwa msingi huu (na ni huu tu) naunga mkono talaka, vinginevyo siungi mkono
   
Loading...