Talaka Haijakatazwa



Kwanza hongera kwa kuchangia. Nikirudi kwenye hoja zako. Je hiyo nukuu ni kutoka kitabu cha torati au injil?. Hujui tufouti ya Torati na injili Mkuu?

3. Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
Mkuu nimekoleza neno kwa kila sababu iliujue msingi wa swali la mafarisayo. Mkuu si kila sababu inayomfanya mtu kutoa talaka, talaka haitolewi eti kisa mtu kaamua bali ikiwa kuna uvunjifu mkubwa wa sheria za maadili. ndio maana nikasema hapo mwanzo, bikra ilikuwa moja ya vigezo vinavyoweza mfanya mtu atoe talaka. kwani mwanamke asiye na bikra moja kwa moja huhusishwa na uasherati yaani alishazini. Sio mwanamke kakosea kupika ndio umfukuze, hapana hili ni kosa. ndio maana swali la mafarisayo lilijikita kuuliza kila sababu.
 


Mkuu ishu inayozungumziwa pale ni kuona neno Ovu yaani ikiwa utagundua mke wako amecheat unaweza kutoa talaka.
 
Tunatetea talaka kwakuwa tumejiandaa kutenda maovu.


Hatutetei Talaka kwa kutenda Maovu Mkuu. Talaka ni kitu rasmi kabisa. Kama ni suala la kuoa wake wawili au watatu mbona liko wazi kabisa.
 
Hapa talaka imeruhusiwa ila kwa kosa la uzinzi. The problem is, je ni uzinzi wa wote au wa mke tu?

Mwanaume yeye anaruhusa kuoa wake wawili na zaidi hivyo akizini ni uzembe wake. Kwani sheria zipo na zinamruhusu kufanya hivyo
 
Naona talaka uiongeleayo ipo upande mmoja wa wanaume! Kwa maelezo yako na mwanamke anaruhusiwa talaka iwapo mumewe yupo kinyume nae!


Kwa msingi wa Biblia Mwanamke hana Mamlaka ya kutoa talaka. Unajua maana ya Talaka lakini Mkuu?

Talaka inavigezo vyake ambavyo ni:
1. Kutoa mahari
2. Kuoa

Huwezi toa Talaka ikiwa hujatoa Mahari wala hujaoa. Sasa jiulize kati ya mwanaume na mwanamke nani anatoa Mahari na nani anaoa?
 


Nipe andiko Mkuu linalosema Mume mmoja na mke mmoja kwa watu wa kawaida isipokuwa Askofu, wachungaji na Makuhani. Ukinipa hilo andiko nafuta mada nzima. Wapo watu wanaweza kuoa mke mmoja, wapo wengine wawili, watatu mpaka ishirini. Ila wapo watu ambao hata mke mmoja tuu anamsumbua.

Maandiko yanasema Mwanamke aliumbwa kwaajili ya mwanaume.
 


Manabii wakubwa karibu wote walikuwa na Wake wawili sasa wewe unayesema hivyo sijui umeyatoa wapi hayo maneno.
Ibrahimu Wake watatu Sarah, Hajiri, Ketura
Yakobo/Israel Wake wawili, Rahel na Lea Dada yake. Na vijakazi wao wawili
Suleiman wake Mia saba, masuria 300
Daudi wake wengi ila hamfikii mwanae Suleiman
Lameck wake wawili
 
Unakaribishaje povu wakati wewe ndo unatoa povu kwa niaba ya ule...!!
 
Hapa talaka imeruhusiwa ila kwa kosa la uzinzi. The problem is, je ni uzinzi wa wote au wa mke tu?
philosopher do not philosophize everything...you will be too busy in this world!
 
Naona kila kukucha ukweli unazidi kujiweka wazi na uongo kutoweka kidogo kidogo. Ahsante kwa bandiko lako mkuu, tatizo ni je! Watakubali?
 
Naona kila kukucha ukweli unazidi kujiweka wazi na uongo kutoweka kidogo kidogo. Ahsante kwa bandiki lako mkuu, tatizo ni je! Watakubali?

Nani asikubali.

Ikiwa Mungu mwenyewe hajafunga pingu za maisha na wewe sembuse mtu. Mtu akivunja miiko basi awajibike tuu
 
Nani asikubali.

Ikiwa Mungu mwenyewe hajafunga pingu za maisha na wewe sembuse mtu. Mtu akivunja miiko basi awajibike tuu
Tatzo watu washakalilishwa, kwamba mwenye uwezo wa kuvunja ndoa pale inapolazimika labda ni papa tu. Sasa hayo maandiko yako kwa mtu mwenye imani ya mapokeo inakua ngumu kukuelewa mkuu.
 
Tatzo watu washakalilishwa, kwamba mwenye uwezo wa kuvunja ndoa pale inapolazimika labda ni papa tu. Sasa hayo maandiko yako kwa mtu mwenye imani ya mapokeo inakua ngumu kukuelewa mkuu.


Imani pasipo akili ni upumbavu
 
uko sahihi kabisa.......huwezi ishi na mtu ukiwa huna furaha hata kdg.....unampa kibali cha kuolewa tena asonge mbele.
 
uko sahihi kabisa.......huwezi ishi na mtu ukiwa huna furaha hata kdg.....unampa kibali cha kuolewa tena asonge mbele.


Wengi wanaelewa hii kimya kimya, sema mdomoni wanapinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…