Takwimu za Deni la Taifa kwa sasa

Takwimu za Deni la Taifa kwa sasa

Tuna wakati mgumu sana kama Taifa. Na hapa tulipofika ni hatari zaidi katika nchi hii ambayo watu wake wengi ni Wakulima na Wafanyakazi.
Ninajiuliza ikiwa kiasi hicho ni cha miaka minne tu, je, Rais huyu akipewa awamu ya pili tutaangukia wapi?

Mimi nnaulizia Matokeo (Faida) ya ukopwaji huu mkubwa Pesa ambazo nntakuja kuzilipa ,ni kitu gani tumepata kama Taifa !!?
Kununua watu ndani ya nchi,kuua upinzani nk
 
Weka takwimu za madeni ya Taifa ya Marekani na Japan tuone na ufanye analysis pia.

Halafu sijui kama unafahamu tofauti kati ya Deni la Taifa na Deni la Serikali kwa kuwa naona unapuyanga tu!
Lakini pia kwani pesa zinazokopwa Mh Rais anazitumia kunywea pombe au anawekeza kwenye miradi kwa ajili Taifa na wananchi wake?
Haya ya kuhomola hela bila utaratibu kwa kushirikiana na mtoto wa dada nayo huyajui ? Lwajabe kajinyonga mkuranga , hilo nalo hujasikia ?
 
Tumrudishe Mkapa mtumie angelo hai ndiye rais peke aliejenga uchumi imara
 
Deni linatoka wapi jamani na wakati tunaambiwa tunatumia fedha zetu za ndani yaani sisi ni dona kantri.
Samahani ndugu yangu hivi una akili sawa sawa? Hello za kuwapa madiwani wa Arumeru ili waunge juhudi ulimpatia wewe mkuu wa Wilaya Mnyeti? Hivi hushangai kwa Nini Ndugai alitibiwa kwa billion 27 ugonjwa usiojulikana mpaka akamnunia CAG. Hayo Ni kwa uchache
 
Vizazi tunavyoviachia haya madeni tunavyoviachia pia elimu bora ya kupambana na changamoto za kesho? Umeme wa uhakika pamoja na mabadiliko ya tabia hewa? Watakuwa na shirika la ndege na SGR vinavyo function?
 
Samahani ndugu yangu hivi una akili sawa sawa? Hello za kuwapa madiwani wa Arumeru ili waunge juhudi ulimpatia wewe mkuu wa Wilaya Mnyeti? Hivi hushangai kwa Nini Ndugai alitibiwa kwa billion 27 ugonjwa usiojulikana mpaka akamnunia CAG. Hayo Ni kwa uchache
Bila samahani ndugu yangu nina akili sawasawa..je na wewe una akili sawasawa? Nimeuliza swali kutokana na tunavyoaminishwa na rais kwamba tunatumia fedha zetu nikauliza..deni linatoka wapi sasa..maswala uliyonitajia hata hayahusiki na nilichouliza acha upopoma
 
Acha kutulosha ujinga weee mbwiga kila mtu arafanya maamuzi kwa utashi wake
Nikulishe ujinga mara ngapi na wakati hapo ulipo umeshakuwa mjinga tayari..anyway sikushangai mapopoma kama wewe Tanzania mpo wengi sana..
 
Bila samahani ndugu yangu nina akili sawasawa..je na wewe una akili sawasawa? Nimeuliza swali kutokana na tunavyoaminishwa na rais kwamba tunatumia fedha zetu nikauliza..deni linatoka wapi sasa..maswala uliyonitajia hata hayahusiki na nilichouliza acha upopoma
Hukunielewa kusudio langu,nilikuwa naku support halafu huko nakushangaaa ili nifikishe ujumbe wangu nilio kusudia kwa walengwa. Tuko pamoja
 
Nyie watu hamjui mnataka nini
2015 mlikua mnapiga kelele mkapa kaua uchumi kauza mashirika yenye nguvu kwa bei ya kutupa kama NBC,SIGARA NA TBL,mkaenda mbali zaidi kutaka afungwe kwa kujimilikisha mgodi wa kiwira kwa shilingi milioni 70,leo umekuja na ugunduzi mpya kuwa mkapa alikua mpiganaji uchumi!!
Yooote haya kutafuta kumfanya Magufuli aonekane si lolote mpaka mnasahau maandishi yenu yapo humu ukibisha nakutolea thread zako ulizokua ukisema mkapa fisadi
Kwani kuna kilichobalika? Sio kweli kwamba hakuua na kuuza mashirika kwa bei chee!!!? Ila hii haiondoi hoja kwamba katika kipindi chake deni la taifa lilipungua, sababu zikiwa nyingi mojawapo ikiwa ni kusamehewa kwa madeni kwa nchi masikini. Sasa huyu wetu leo nahisi angepata hiyo fursa angeyaongeza zaidi na kuzidi aliyosamehewa.
 
KWA TAKWIMU HIZI ZA DENI LA TAIFA HAKIKA TUNAANGAMIA.

01. Awamu ya kwanza chini ya Mwl. Nyerere alieongoza kwa miaka zaidi ya miaka 20.
-Deni la Taifa lilipotoka mwaka 1979 mara tu baada ya vita ya Kagera lilikuwa Trilioni 3.

02. Awamu ya pili chini ya Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza kwa miaka 10.
-Deni la Taifa lilipanda kutoka Trilioni 3 hadi kufikia Trilioni 18. Hii inamaana kuwa, Mzee Mwinyi alikopa fedha kiasi cha Trilioni 15 pekee ndani ya awamu zote mbili.

03. Awamu ya tatu ya Mhe. Benjamin Mkapa aliyeongoza kwa miaka 10.
-Mzee Mkapa alipoingia alikuta deni ni Trilioni 18. Mzee Mkapa akafanya jitihada za kupunguza deni hilo na kufanikiwa kulipunguza hadi kufikia Trilioni 10.
Mpaka anaondoka madarakani uchumi ulikuwa unakuwa kwa 6.7%
Kwa neno moja tu tunaweza kusema, Mzee Mkapa alikuwa ni "Mpiganaji wa uchumi".

04. Awamu ya nne chini Mhe. Jakaya Kikwete alieongoza miaka 10.
-Ameingi amekuta deni la Taifa ni Trillion 10. Lakini katika kukopa kwake mpaka anamaliza muda wake wa uongozi (awamu zote mbili) ameacha deni la Trilioni 35. Maana yake kwa miaka yote 10 amekopa kiasi cha Trilioni 25.

05. Awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ambae mpaka sasa ana miaka minne (4) ya uongozi wake ikiwa hajakamilisha hata awamu moja ya miaka mitano.
-Ameingia madarakani amekuta deni la Taifa lililoachwa ni Mzee Kikwete ni Trilioni 35.
-Mpaka kufikia mwezi huu wa January mwaka 2019, deni la Taifa limefika Trilioni 61.8
*Kwa lugha rahisi ni kwamba Rais Magufuli amekopa Trilioni 26 ndani ya miaka minne (4) tu.*
Hivyo basi, ni dhahiri kusema kuwa, Rais Magufuli ndiye Rais pekee kati ya marais wote waliopita, aliyekopa pesa nyingi sana kwa muda mfupi sana.

Tuna wakati mgumu sana kama Taifa. Na hapa tulipofika ni hatari zaidi katika nchi hii ambayo watu wake wengi ni Wakulima na Wafanyakazi.
Ninajiuliza ikiwa kiasi hicho ni cha miaka minne tu, je, Rais huyu akipewa awamu ya pili tutaangukia wapi?

View attachment 1192870
Hata afikishe Trillion kupita awamu zote lakini ni Serikali hiihii ya awamu ya tano chini ya Commander In Chief Magufuli itakayokuwa na uwezo wa kulipa madeni yake yote kwa muda mfupi kutokana na utekelezaji na ukamilishaji wa miradi yake yote mikubwa iliyoikuta na iliyoianzisha.

Kuna haja ya kusudi kabisa Magufuli apewe kipindi chake cha pili wakati miradi aliyoifanyia kazi inaporudisha faida tuanze kufaidika pamoja nae!
 
Hatuwezi kuwa na deni hilo wakati tunajenga miradi mikubwa kama SGR, Stigula goji, ndege tumenunua kwa cash yote hiyo ni kwa pesa yetu ya ndani tuliyoibana toka kwa nafisadi. Rais haendi nje tumebana matumizi sana. Sasa deni linaongezeka kutokana na nini?! Tafadhali rais itisha mkutano ikulu TBC live kukanusha uongo wa mabeberu hawa
Subutu!, wewe wewe ,najaribu kama yeye ni mkweli,mimi nitachukua kadi na ya chama chake hadharani na kushawishi jamaa zanzgu wote wampe kura.
 
Nadhani pamoja na deni kuwa kubwa kipindi cha Dr Magufuli lakini matokeo ya pesa iliyo kopwa tunayaona, Kwenye miundombinu, Vituo vya afya kila kata, Ndege, elimu bure. haina shida tutalipa tu maaana rasilimali zetu zina value kubwa kuliko hilo deni na anazisimamia vizuri .Viva My president
 
Back
Top Bottom