Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,914
- 16,528
"Kuna tuhuma ya wizi wa kutisha kwenye mikopo ya serikali ambapo kwa miaka mitano iliyopita deni la serikali limeongezeka kutoka trilioni 60.7 Machi 2022 hadi trilioni 115.2 Februari 2026, sawa na ongezeko la trilioni 54.3. Deni limeongezeka kutoka ukuaji wa wa asilimia 7 hadi ukuaji wa asilimia 19."
"Sasa, lakini kwa sehemu kubwa mikopo hii imechukuliwa kwa siri nje ya bajeti, na imepita kwenye na haijapita kwenye mfuko mkuu wa serikali. Na maana yake kama haikupita kwenye mfuko mkuu wa serikali imepita kwenye akaunti za watu binafsi. Jambo hili haliruhusiwi, ni kinyume na ibara ya 135 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."