Uchaguzi 2020 TAKUKURU yamshikilia mgombea wa ubunge kupitia CHADEMA jimbo la Mtama kwa tuhuma za kutoa rushwa ili atangazwe kuwa mshindi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Lindi imemkamata na inamshikilia mgombea ubunge wa jimbo la Mtama kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Seleman Luwongo kwa tuhuma ya kutaka kumpa rushwa ofisa uchaguzi wa halmashauri ya Mtama.

Leo akizungumza na waandishi wa habari mjini Lindi, mkuu wa TAKUKURU wa mkoa wa Lindi, Steven Chami alisema taasisi hiyo inatarajia kumfikisha mahakamani Luwongo kwa tuhuma ya kutaka kumpa rushwa ya shilingi 1,540,000 ofisa uchaguzi wa jimbola Lindi ili atangazwe ameshinda wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Mkuu Chami alisema Luwongo alikamatwa jana jioni majira ya saa 12 huko Mtama. Akibainisha kwamba kiasi hicho cha fedha ni sehemu ya shilingi 10,000,000 za kuwahonga ofisa uchaguzi huyo na msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri ya Mtama ili atangazwe kuwa mshindi wa nafasi hiyo ya ubunge.

''Mtuhumiwa alikamatwa kufuatia taarifa iliyopokelewa ikieleza kuwa tarehe 21.08.2020 majira ya saa tano asubuhi alikwenda katika ofisi ya uchaguzi pamoja na msimamizi wa uchaguzi, na lengo la maongezi yake ni kutaka asaidiwe kutangazwa mshindi wa kura za ubunge jimbo la Mtama,'' Chami alisisitiza.

Alibainisha kwamba Luwongo ili kutimiza lengo lake la kutangazwa mshindi aliandaa shilingi 10.00 milioni ili awape wote wawili( ofisa na msimamizi wa uchaguzi). Nakwamba alihaidi kutoa fedha za utangulizi siku ya kurejesha fomu.

Chami ambaye alikuwa sambamba na mkuu wa TAKUKURU wa mkoa wa Mtwara, Enock Ngailo alisema baada ya uchunguzi TAKUKURU ilibaini pasipo nashaka kitendo kilichofanywa na Luwongo ni kushawishi kutoa rushwa.

Ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007. Kwahiyo ofisi ya TAKUKURU ya mkoa wa Lindi kwa kushirikiana na ofisi ya TAKUKURU ya mkoa wa Mtwara iliweka mtego uliomnasa Luwongo.

Chami alimaliza mazungumzo yake kwa kusema baada ya kukamilisha uchunguzi inatarajia kumfikisha mahamani leo ili akajibu tuhuma inayomkabili kwa mujibu wa kifungu cha 15(1) (b) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Muungwana
Kati ya taasisis ya Kwanza kuundwa upya baada ya TL ukuingia ikulu Ni Takukuru.Takukuru Ni tawi la ccm
 
It is too stupid to be true!
 
Hata uchaguzi bado,kampeni bado,anahongaje ili atangazwe kushindwa?!!

Hizi mbinu za kummaliza asigombee tena!!
Hakuna kitu hapo. Pesa hiyo ni ya CCM. Kasingiziwa huyo. Walimkamata wakati anamuhonga msimamizi? Au msimamizi ndiye aliyesema kwa TAKUKURU kuwa kahongwa? Waache utoto.
 
Chami ambaye alikuwa sambamba na mkuu wa TAKUKURU wa mkoa wa Mtwara, Enock Ngailo
Huyu ndugu yangu ananiaibisha....eti nayeye ANATHIBITISHA🙄
 
Back
Top Bottom