Uchaguzi 2020 TAKUKURU yamshikilia mgombea wa ubunge kupitia CHADEMA jimbo la Mtama kwa tuhuma za kutoa rushwa ili atangazwe kuwa mshindi

Jinga wewe kama wamesema watamfikisha mahakamani ni kwanini sasa umedai Takukuru wamethibitisha hilo kosa kutendeka? Ona ulivyo mpumbavu? Matukio mangapi Takukuru wamekamata watu lakini leo wapo tu uraiani? Acha upumbav
Kule mtera jimboni kwa Livingston Lusinde kibajaji rafiki wa ndungai na mtukufu alishikwa na cash mkononi na picha video live zikionyesha lakini Takukuruccm hawakufanya chochote
 
Kumbe yawezekana kweli mzee wasira walimhongea akashindwa na bulaya, kwa hili la mtama tumefumbua macho tuko chonjo sana
Umejifumbua macho kwa lipi? Ebu tumia hata Akili yako ndogo ya kufulia chupi yako, kesi za kutengeneza kesi za kuwabambikia wapinzani kwa kushirikiana na Takukuruccm ndipo zikufungue macho wewe kipofu?
 
Haiwezi kuingia akilini hata kidogo.
Ni tuhuma ambazo hazina mantiki kabisa.

Yaani mgombea wa chama cha Upinzani (CHADEMA) aende kumhonga DED (msimamizi wa uchaguzi aliyeletwa kuja kuhakikisha CCM inashinda), tena vimilioni vichache, wakati hata fomu ya kugombea alikuwa bado hajarudisha.

Ni tuhuma za kiuwendawazimu kwa 100%
CCM hutengeneza kesi za kuwabambikia wapinzani pasipo kutafakari kabla na huwa hawajui kuwa kuna mungu pia na ataweza kufunua mbinu zao chafu za kishetani kushirikiana na Takukuruccm kuwabambikia kesi wapinzani ni kitendo kibaya sana Nape Tutaenda kukushitakia kwa baba yako mzee mwandosya
 
Hao wanaitwa majasiri. Yani hata kampeni bado unaweka mazingira salama. Kama ni kweli basi huyo ni mkali.
Kesi ya kubambikiwa hiyo Hakuna cha Rushwa wala nini bali Takukuruccm wamejitoa fahamu kufanya uonevu
 
Takukuruccm muogopeni mungu acheni kufanya kazi kwa mujibu wa watumishi wa CCM, fanyeni kazi kwa mujibu wa katiba na Sheria na endapo mtaendelea kuwabambikia kesi wapinzani mjiandae kusomewa Albadiri kwani hakuna mabaya yasiyo na mwisho.
 
Dah huu ssa ndo unaitwa upofu. Yaani mtu katoa rushwa kabisa na imethibitika, lakini eti bado anatetewa. CCM ndo inayoonekana imemfanyia mchezo, basi inaonekana huko CDM watu wote ni malaika hakuna binadamu.
CCM hata mje na utetezi gani hakuna wa kuwaamini hizo Tabia zenu za kuwabambikia kesi wapinzani zipo Nchi nzima hilo hakuna ubishi
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Lindi imemkamata na inamshikilia mgombea ubunge wa jimbo la Mtama kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Seleman Luwongo kwa tuhuma ya kutaka kumpa rushwa ofisa uchaguzi wa halmashauri ya Mtama.

Leo akizungumza na waandishi wa habari mjini Lindi, mkuu wa TAKUKURU wa mkoa wa Lindi, Steven Chami alisema taasisi hiyo inatarajia kumfikisha mahakamani Luwongo kwa tuhuma ya kutaka kumpa rushwa ya shilingi 1,540,000 ofisa uchaguzi wa jimbola Lindi ili atangazwe ameshinda wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Mkuu Chami alisema Luwongo alikamatwa jana jioni majira ya saa 12 huko Mtama. Akibainisha kwamba kiasi hicho cha fedha ni sehemu ya shilingi 10,000,000 za kuwahonga ofisa uchaguzi huyo na msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri ya Mtama ili atangazwe kuwa mshindi wa nafasi hiyo ya ubunge.

''Mtuhumiwa alikamatwa kufuatia taarifa iliyopokelewa ikieleza kuwa tarehe 21.08.2020 majira ya saa tano asubuhi alikwenda katika ofisi ya uchaguzi pamoja na msimamizi wa uchaguzi, na lengo la maongezi yake ni kutaka asaidiwe kutangazwa mshindi wa kura za ubunge jimbo la Mtama,'' Chami alisisitiza.

Alibainisha kwamba Luwongo ili kutimiza lengo lake la kutangazwa mshindi aliandaa shilingi 10.00 milioni ili awape wote wawili( ofisa na msimamizi wa uchaguzi). Nakwamba alihaidi kutoa fedha za utangulizi siku ya kurejesha fomu.

Chami ambaye alikuwa sambamba na mkuu wa TAKUKURU wa mkoa wa Mtwara, Enock Ngailo alisema baada ya uchunguzi TAKUKURU ilibaini pasipo nashaka kitendo kilichofanywa na Luwongo ni kushawishi kutoa rushwa.

Ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007. Kwahiyo ofisi ya TAKUKURU ya mkoa wa Lindi kwa kushirikiana na ofisi ya TAKUKURU ya mkoa wa Mtwara iliweka mtego uliomnasa Luwongo.

Chami alimaliza mazungumzo yake kwa kusema baada ya kukamilisha uchunguzi inatarajia kumfikisha mahamani leo ili akajibu tuhuma inayomkabili kwa mujibu wa kifungu cha 15(1) (b) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.


Muungwana
Kura hazijapigwa eti rushwa itolewe ili atangazwe mshindi ! Takukuru sikilizeni , hata kama watanzania ni mabwege lakini si wa kudanganywa kijinga namna hiyo
 
Hivi si ni hii hii ile TAKUKURU iliyokabidhi vyesi vyote vya rushwa ccm vishughulikiwe huko tena wapo kwa chadema. Kesi ya kutengeneza haina mashiko
 
Wakristo huamini kwamba Mungu akitaka kukudondosha hukutia kwanza upofu, unakuwa unafikiri unaona kumbe huoni! Ndicho kinatokea sasa kwa CCM. Kama ulivyoandika hapa, huyu mtu ambaye hata hajathibishwa na NEC ampatie rushwa DED kwa ajili ya kumtangaza kushinda?


Ukifikiri vizuri unaona kabisaa Ni mbinu ya kitoto imetumika.
 
Dah huu ssa ndo unaitwa upofu. Yaani mtu katoa rushwa kabisa na imethibitika, lakini eti bado anatetewa. CCM ndo inayoonekana imemfanyia mchezo, basi inaonekana huko CDM watu wote ni malaika hakuna binadamu.
Hapo mtama kuna figisu za kutosha kutoka kwa NAPE , huyu mgombea amekamatwa akiwa anahakiki fomu zake ofisi ya tume, kwahiyo hakukabidhi fomu.

Mgombea wa ACT alirejesha fomu alirejesha fomu tar 25 .08.2020 lakini ofisi zilifungwa toka asubuhi hadi jioni kwahiyo hakukabidhi fomu.

Ni njama za kujinga na kihuni
 
Hapo mtama kuna figisu za kutosha kutoka kwa NAPE , huyu mgombea amekamatwa akiwa anahakiki fomu zake ofisi ya tume, kwahiyo hakukabidhi fomu.

Mgombea wa ACT alirejesha fomu alirejesha fomu tar 25 .08.2020 lakini ofisi zilifungwa toka asubuhi hadi jioni kwahiyo hakukabidhi fomu.

Ni njama za kujinga na kihuni
Dah! Kumbe ilivyokua?! Mbona Suleiman Methew hakusema hayo?
 
Nadhani anataka akiwa kapata Kura nyingi wasimwekee figisu na wamtangaze tuu.. alikua anajaribu kufanya booking ya haki yake.
 
Wakristo huamini kwamba Mungu akitaka kukudondosha hukutia kwanza upofu, unakuwa unafikiri unaona kumbe huoni! Ndicho kinatokea sasa kwa CCM. Kama ulivyoandika hapa, huyu mtu ambaye hata hajathibishwa na NEC ampatie rushwa DED kwa ajili ya kumtangaza kushinda?
Usikimbilie tu kuweka comment...tathimini kuhusu maelezo ya tukio lenyewe..
 
Back
Top Bottom