Elections 2010 TAKUKURU yamkamata Magreth Sitta Tabora; Aachiwa kwa dhamana

Majasho

JF-Expert Member
Aug 4, 2009
413
220
871.jpg


Waziri Sitta amekamatwa kwa tuhuma ya kutaka kutoa rushwa na TAKUKURU mkoani Tabora. Sitta amekamatwa na fedha zaidi ya millioni moja na bahasha za kaki 140 na simu za mkononi aina ya Nokia. Sitta ameachiwa kwa dhamana.

Habari zaidi nikizipata
 
hayo ni mambo yao. Na ukizingatia huko ndio mkoani kwa fisadi papa wala usishangae mzee. habari ndio hizo kumkwaza mzee 6
 
Waziri Sitta amekamatwa kwa tuhuma ya kutaka kutoa rushwa na TAKUKURU mkoani Tabora. Sitta amekamatwa na fedha zaidi ya millioni moja na bahasha za kaki 140 na simu za mkononi aina ya Nokia. Sitta ameachiwa kwa zamana. Habari zaidi nikizipata

Watakamatwa wengi na kampeni hizi!...
 
Inawezekana ni kweli au ndo mbinu za kuondoa mzee six ulingoni asirudi kabisa mjengoni. Mambo yao hao. Mwaka huu ni nomaa ngoja nichukue modem kabisa ili 24 hours nafuatilia michezo michafu hii.
 
TBC imetangaza kwenye taarifa yao ya habari kuwa mke wa Spika Mama Magreth Sitta amekamatwa akitoa rushwa huko Tabora. Inavyoelekea TBC wameshabikia habari hiyo na kuzungumza moja kwa moja na Kaimu mkuu wa TAKA-KURU wa mkoa huo wakimdhihaki na kumhukumu kuwa ametoa rushwa.
Mbona hawa Takukuru hawaendi igunga ambapo yule muiran anachagiliwa tu kwa mlungula????
sijui nchi inaendaje
 
watoa taarifa ni wale wale wa kadi elfu kumi, hiyo mnayoitikisa ni mibuyu haiangushwi kwa upepo mwanana yanayoanguka ni majani tu hata matunda yake hayatikiswi sembuse shina, kalagabaho mtachonga sana mwaka huu na mwisho wenu umefika ni J'3 tu nitawatafuta.
 
TBC imetangaza kwenye taarifa yao ya habari kuwa mke wa Spika Mama Magreth Sitta amekamatwa akitoa rushwa huko Tabora. Inavyoelekea TBC wameshabikia habari hiyo na kuzungumza moja kwa moja na Kaimu mkuu wa TAKA-KURU wa mkoa huo wakimdhihaki na kumhukumu kuwa ametoa rushwa.
Mbona hawa Takukuru hawaendi igunga ambapo yule muiran anachagiliwa tu kwa mlungula????
sijui nchi inaendaje
.

Jamani,
Hapo ndipo mnapotuchanganya sasa.
Taarifa inasema amekamatwa akitaka kutoa rushwa.Sasa kelele zote hizo za nini?.Si kuna mahakama na atakwenda kujitetea huko?Ushabiki gani huu wa kutotumia akili.
 
Mama Sita kama kakamatwa na rushwa anapaswa kuwajibika kama raia mwingine yeyote anayekamatwa na rushwa. Sijasikia wala kuona hiyo taarifa, ila naipokea kama taarifa zingine tunavyozisikia, tukianza kuweka hayo ni kama tunataka kusema wengine wako juu ya sheria. TAKUKURU wanapaswa kuwatreat watuhumiwa wote kwa uzito ule ule, si kwa sababu ni mke wa Sita au waziri.
 
hizi ni njama za ROSTAM NA HOSEA za kumpunguza nguvu SPIKA tu kwasababu aliwashugulikia bungeni mbona wabunge,wadiwani wengi tu wanakamatwa lakini haitangazwi???yaani MAGRET ndo wa kwanza kutoa rushwa????SPIKA hili lisikuvunje moyo tena ukirudi mjengoni washugulikie ipasavyo
 
Ni kosa kuwa katika nyumba ya kulala wageni?
Ni kosa kuwa na bahasha za kaki?
Ni kosa kuwa na simu mpya zaidi ya moja?
Ni kosa kutembea na shilingi milioni moja?

Hii yote sanaa tu..........!
 
nyie mnacheza nani apelekwe mahakamani watu wamekamatwa na pesa za EPA wakasamehewa wakaambiwa warushe taratibu siku wakipata sijui lini.
 
Hizi Rushwa za uchaguzi, mbona wanatajwa na kukamatwa wanaotoa tu!! kwani ile sheria ya Rushwa inasemaje?
 
Mama Sita kama kakamatwa na rushwa anapaswa kuwajibika kama raia mwingine yeyote anayekamatwa na rushwa. Sijasikia wala kuona hiyo taarifa, ila naipokea kama taarifa zingine tunavyozisikia, tukianza kuweka hayo ni kama tunataka kusema wengine wako juu ya sheria. TAKUKURU wanapaswa kuwatreat watuhumiwa wote kwa uzito ule ule, si kwa sababu ni mke wa Sita au waziri.

Hosea analipiza kisasi kuonekana na Bunge liliongozwa na Sitta kuhusika na rushwa ya Richmond.

Na wale watuhumiwa wa ufisadi 11 aliowataja Dr Slaa pale mwembe yanga serikali imewachulia hatua gani?, Hosea hakuwemo kweli?
1.Rostam
2. Mkapa
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Nisiadieni wengine nimewasahau tuwataje wote kwa majina.

Takururu inafanya siasa za maji taka kwa Sitta kwa vile Hosea alihusishwa na Bunge kwenye kashfa ya Richmond
 
Mimi siamini kwamba tangu hizi mbio zakura ya maoni zianze hakuna mbunge yoyote ambae hajakamatwa na takukuru,lazima wapo lakini hatujawahi kutangaziwa,wanatutangazia madiwani tu..Hili la kumtangaza waziri SITTA si bure lina mkono wa ROSTAM NA HOSEA,hawa watu wawili wana uhasama na SPIKA jinsi alivyowasugulikia bungeni..na Rostam yupo tabora aiendelea na kampeni zake..SPIKA sita hizi habari zisikuvunje oyo badala yake ongeza bidii na bunge lijalo uwashugulikie haswa..sasa hv wabaya wote wa SPIKA(ROSTAM,LOWASA....)watakuwa wanafurahi sana
 
22. The following persons shall be deemed to commit
unconscionable funding within the meaning of this Act:
(a) every person who corruptly, by himself or by
any other person, on his behalf, either before,
during or after the nomination process or
election directly or indirectly gives, or provides,
or pays, wholly or in part, the expense of giving
or providing food, drink, entertainment or
provisions to or for any person, for the purpose
of influencing that person, or any other person,
to vote or to refrain from voting at such
nomination process or election; and
(b) every person who corruptly accepts or takes any
such food, drink, entertainment or provision.

so habari ndiyo hiyo
 
Sasa hii imekaaje kwa hawa TAKUKURU mbona wanamoyo sana kukamata
au wamehaidiwa kitu manake ghafla wamefufuka kila siku sasa tunawasikia
mara huyu mara yule sijui hii imekaaje wadau naomba msaada.
 
Back
Top Bottom