Elections 2010 TAKUKURU yamkamata Magreth Sitta Tabora; Aachiwa kwa dhamana

Nahisi niwakati muafaka Jk anaitaji kujua ni jeshi la mawaziri la aina gani alillokuwa nalo miaka 5 iliopita na kuwahadaa wananchi yuko na baraza lililo imara...nahisi vitendo vya rushwa vya kuwakamata watu ni mfano wa kujua ni wapi alipo na wapi anaelekea

kitendo cha kukamatwa mama magreth sitta ambae ni waziri kinatuonyesha nini kinaendelea na tutarajie baraza gani 2011

Kazi kwako mtanzania mpiga kura
 
wanaokamatwa na rushwa CCM wala hamna anayewachomekeaa..ukiwafuatilia tuu bila hata mbinu za PCCB unawakamataaa...

bila rushwa hakuna UHAI WA CCM...Hapo sasa WAGOMBEA WATAPATAJE ULAJI CCM BILA RUSHWAAA.....
 
Hivi kweli watanzania tuko chjeap namna hiyo? Yaani kura zetu zinanunuliwa kwa bei rahisi ya simu ya Nokia ambayo thamani yake ni sawa na allowance ya siku moja ya mbunge, eti tunakubali?
 
Mheshimiwa Magreth 6 ni mtuhumiwa tu na hatimaye vyombo vya sheria vitathibitisha hizo tuhuma na tutajua ukweli. Kwa sasa ninaamini iko nguvu ya ufisadi nitendayo kazi ndani ya TAKUKURU na hivyo lolote lawezekana. Kama TAKUKURU wameanza kuwa mawakala wa ufisadi historia itakuja kuwaumbua. Iko siku Hosea. IKO SIKU!
 
Naombeni kamera yenye resolution nzuri. Kuna baa moja jamaa wanakutana na kugawana hela, ila simu yangu ndo hivyo tena, imeharibika kamera.
 
Takukuru inalinda wengine na wengine ni wa kukamatwa sivyo? Huu si kaule mchezo wa kukamata wabunge wa Arusha?

Sina shaka ni kumbeep mzee sita, kuvuruga kiakili.

Je ni kosa kwa kuwa na bahasha au pesa? Au kuna muda maalum wa mtu kutembea kipindi hiki? Huyu mama kuwa na simu sita kama jina lao ni kosa? Kwa wajibu wake na kazi zake hizo simu ni chache.

Siungi mkono rushwa lakini natambua mikono ya mafisadi papa na walinzi wao. Hawa mafisadi wanalindwa na TAKUKURU ili yao ipenye vizuri zaidi.

VOTE THEM OUT THIS TIME
 
Huko Kasulu Kamanda wa TAKUKURU amehamishwa na kutelemshu cheo Vipi? Tabora atafukuzwa kazi kamanda Mkuu
 
Mheshimiwa Magreth 6 ni mtuhumiwa tu na hatimaye vyombo vya sheria vitathibitisha hizo tuhuma na tutajua ukweli. Kwa sasa ninaamini iko nguvu ya ufisadi nitendayo kazi ndani ya TAKUKURU na hivyo lolote lawezekana. Kama TAKUKURU wameanza kuwa mawakala wa ufisadi historia itakuja kuwaumbua. Iko siku Hosea. IKO SIKU!

TAKUKURU haina credibility tena tokea waliposafisha kashfa ya richmond. Katika nchi zinazofahamu nini maana ya chombo cha umma kuwa na public trust, ni dhahiri kuwa Hoseah alikuwa amekosa sifa za kuiongoza TAKUKURU na hivyo alitakiwa amaa akae pembeni au akalishwe pembeni. Yoote yanayotokea hivi sasa yanayofanywa na TAKUKURU yanabakia kuwa yaleyale ya kulipiziana visasi na hivyo kuondoa credibility ya TAKUKURU kufanya kazi kwa uhuru bila watu kuhisi wameonewa. Ila Tanzania inaongozwa kisanii tu.
 
Yees...I knew it! Soon enough to note no PCCB in zenji, are they so clean in the isles or their tentacles are locked by the so called laws?
 
Watu hapa wanaongozwa emotional si mchezo! Habari hizi za kukamatwa wamekamatwa wengi tu? Leo hii Bi Sitta yupo mnalalamika kaonewa? Kuna watu wanasema mbona wengine wanatoa hawajakamatwa? Two wrong can't make it right!
 
Watu hapa wanaongozwa emotional si mchezo! Habari hizi za kukamatwa wamekamatwa wengi tu? Leo hii Bi Sitta yupo mnalalamika kaonewa? Kuna watu wanasema mbona wengine wanatoa hawajakamatwa? Two wrong can't make it right!

... Mkuu, hayo ndiyo ya kujiuliza hapa, kama wamekamata wengi kwa tuhuma za rushwa mbona hatuoni au kusikia hata mmoja akifungwa?? Wanakamata kwa ajili ya maigizo, au?!

... Kwa Mama Sitta kama habari inavyojieleza, walishindwa nini kusubiria na kumkamata akitoa rushwa badala ya kuhisi kuwa analengo la kutoa rushwa? Kwanini mbinu zao ziko so bogus kiasi kwamba kila anayekamatwa anaishia kuachiwa huru, hali ukweli ni kwamba ni waharifu?

Na hapa ndipo watu wanaposema, haya maigizo ya Takukuru ya kukamata watu "kisiasa siasa" tumeyachoka sasa!
 
Back
Top Bottom