Take Care People!!!Men at Work.

Ambitious

JF-Expert Member
Dec 26, 2011
2,144
875
Leo majira ya saa 8 mchana nimeshuhudia mwanamume mtu mzima(kama miaka 30 hivi) akiwa amekaa kitako kwenye mchanga huku akimwaga machozi kama vile mtoto mdogo aliyekosa kutimiziwa ahadi ya kununuliwa pipi na wazazi wake.
Baada ya kusogea kidogo na kuuliza nini kimemsibu nikasikia akitamka kwa majonzi kwamba ''laptop ya kazini(akionyesha begi tupu),simu yangu na pesa taslimu Tsh.600,000 vyote vimekwenda na matapeli'' huku akisisitiza:''Jamaa wameniharibia kazi,jamaa wameniharibia kazi'', akirejelea laptop ya kazini ndiyo inayomtia mawazo zaidi.
Kabla sijatafakari vizuri walinzi wa Supermarket ya TSN pale kona ya kuingia hospitali kuu ya Mhimbili wakanionyesha mabaki ya vitu vyenye mng'ao kama wa dhahabu huku wakiniambia kwamba jamaa ameingizwa mjini na wajanja wa mjini kwa kuuziwa kanyaboya.
Lakini baada ya kumuuliza vizuri yule mtu aliyetapeliwa akijitambulisha kwa jina moja tu 'Josiah' na anafanya kazi kama Tax Consultant kwenye firm fulani mjini na akasema hakumbuki chochote kuhusu majadiliano yoyote ya kuuziana mali yoyote bali anachokumbuka ni kushikwa bega na kuitwa na sauti iliyosema:''Oya mkuu nakuomba tuongee kidogo'' kisha akaingia kwenye gari na kukuta vijana wawili na msichana mmoja waliovalia vizuri kisha wakamwambia ''Tuna dhahabu hapa tunaiuza kwa bei poa'' baada ya hapo hakumbuki kitu zaidi ya kujikuta hapo alipo bila ya vitu tajwa hapo juu.Jasho lilikuwa likimtoka sana huku ameinamisha kichwa kwa masikitiko baada ya kumaliza kujieleza.
Baada ya muda kidogo kwa tukio zuri gari ya polisi ikakatiza na ikabidi tuisimamishe ili jamaa aliyetapeliwa akatoe maelezo polisi na pia tukamchangia kama Tsh.10,000 ya kwenda kokote atakapoelekea baada ya kutoka kituo cha polisi pale Mhimbili.
Tahadhari kwa wote tuwe makini katika kuongea na watu tusio wafahamu kwa kuwa hili jambo la utapeli wa kiajabu-ajabu limeshamiri sana sehemu za katikati ya mji.Nadhani watu wameongeza speed ya kazi baada ya kusomewa bajeti ya 2012-2013.Men at work people..Watch Out!!
 
asante kwa taharifa,zamani matapeli walikuwa wanavaa vibaya siku hizi wanapiga bling bling uwezi jua adi wadada warembo
 
Hakuna cha sababu za kumcheka!hawa jamb ni noma siku hiz wanatumia mazingambwe....
 
Tena akiwepo mdada unaweza kupata imani kidogo ukidhani hamna baya, kumbe inawezekana ndiye mkuu wa kikosi.
 
Hakuna cha sababu za kumcheka!hawa jamb ni noma siku hiz wanatumia mazingambwe....

Mkuu hajachekwa mtu hapo imetumika lugha ya kitamathali katika kueleza hali aliyo kuwa nayo huyo mtu aliyetapeliwa...
 
Leo majira ya saa 8 mchana nimeshuhudia mwanamume mtu mzima(kama miaka 30 hivi) akiwa amekaa kitako kwenye mchanga huku akimwaga machozi kama vile mtoto mdogo aliyekosa kutimiziwa ahadi ya kununuliwa pipi na wazazi wake.
Baada ya kusogea kidogo na kuuliza nini kimemsibu nikasikia akitamka kwa majonzi kwamba ''laptop ya kazini(akionyesha begi tupu),simu yangu na pesa taslimu Tsh.600,000 vyote vimekwenda na matapeli'' huku akisisitiza:''Jamaa wameniharibia kazi,jamaa wameniharibia kazi'', akirejelea laptop ya kazini ndiyo inayomtia mawazo zaidi.
Kabla sijatafakari vizuri walinzi wa Supermarket ya TSN pale kona ya kuingia hospitali kuu ya Mhimbili wakanionyesha mabaki ya vitu vyenye mng'ao kama wa dhahabu huku wakiniambia kwamba jamaa ameingizwa mjini na wajanja wa mjini kwa kuuziwa kanyaboya.
Lakini baada ya kumuuliza vizuri yule mtu aliyetapeliwa akijitambulisha kwa jina moja tu 'Josiah' na anafanya kazi kama Tax Consultant kwenye firm fulani mjini na akasema hakumbuki chochote kuhusu majadiliano yoyote ya kuuziana mali yoyote bali anachokumbuka ni kushikwa bega na kuitwa na sauti iliyosema:''Oya mkuu nakuomba tuongee kidogo'' kisha akaingia kwenye gari na kukuta vijana wawili na msichana mmoja waliovalia vizuri kisha wakamwambia ''Tuna dhahabu hapa tunaiuza kwa bei poa'' baada ya hapo hakumbuki kitu zaidi ya kujikuta hapo alipo bila ya vitu tajwa hapo juu.Jasho lilikuwa likimtoka sana huku ameinamisha kichwa kwa masikitiko baada ya kumaliza kujieleza.
Baada ya muda kidogo kwa tukio zuri gari ya polisi ikakatiza na ikabidi tuisimamishe ili jamaa aliyetapeliwa akatoe maelezo polisi na pia tukamchangia kama Tsh.10,000 ya kwenda kokote atakapoelekea baada ya kutoka kituo cha polisi pale Mhimbili.
Tahadhari kwa wote tuwe makini katika kuongea na watu tusio wafahamu kwa kuwa hili jambo la utapeli wa kiajabu-ajabu limeshamiri sana sehemu za katikati ya mji.Nadhani watu wameongeza speed ya kazi baada ya kusomewa bajeti ya 2012-2013.Men at work people..Watch Out!!

Kweli mjini mipango ukizubaa kidogo watu wanafanya uwekezaji kwenye mfuko wako.
 
DUH......
sasa na vilaptop vyetu hivi used mbona mwaka huu kazi ipo?? mpaka mwaka huu wa bajeti uishe tutakua tushakimbia mjini..
 
Back
Top Bottom