Kwa mara nyingine malalamiko yametolewa dhidi ya Mmiliki wa vyombo vya habari vya IPP Bw. Reginald Mengi. Huko nyuma amewahi kulalamikiwa na Mbunge wa Mkuranga Mhe. Adam Malima na muda si mrefu uliopita amelalamikiwa na mfanyabiashara mwingine Bw. Yusuph Manji.
Hata hivyo safari hii analalamikiwa na chombo cha TAJA (Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania). Katika barua ifuatayo ambayo nakala yake ametumiwa Rais Kikwete watu wataja wanatoa madai mazito na yenye utata dhidi ya mzee Mengi. Hata hivyo kwa yeyote atakayesoma kwa macho huru ataona kitu kingine kilichofichika.
Amueni wenyewe uzito, ukweli, na mantiki ya madai haya.
TAJA, hawaonekani popote kwenye maslahi ya waandishi wa habari, kimekua kikundi cha watu wachache kwa maslahi binafsi, si chombo cha waandishi wa habari. Angalia TAMWA (Ananilea Nkya), MISA-Tan (Ayubu Rioba) ambavyo vimekua mstari wa mbele kupambana na serikali na ukiukwaji wowote wa maslahi ya wanahabari... JF tusikubali kutumika. Kama kweli ni wana habari mbona hawajafanya Press Conference? Wanahabari wana vyombo vya habari kwanini waje JF? ama kwa sababu wanaona hakuna Editor? nadhani Invisible ni editor, ondoa huu uchafu
duh..!! kilichonishinda mimi ni hiyo lugha iliyotumika. Yaani, kama hawa ndio waandishi na ndio wanajaribu kujenga hoja basi tumekwisha. Zaidi ya yote, kwanini ni wao walalamike? Kama kuna unfair treatment ni serikali ya Zanzibar ndio wangekuwa na sababu ya kulalamika? Je, vyombo vya Zanzibar vinawataja vipi viongozi wa muungano au watu maarufu? Je vyombo vingine vya habari viliripoti kwa kina kiasi gani suala la Shamuhuna?
Wao wenyewe wanaituhumu MCT kuwa ni maswahiba wa Mengi, sasa kwanini wanapeleka malalamiko yao kwake? Hivi wakikataliwa si watasema "tulijua" na wakikubaliwa watasema "tumeogopwa"?
Sidhani kama kuna sababu ya kuondoa; lakinin ni vizuri watu waone na wapime kwa sababu hatuwezi kujua mawazo ya kijinga tusipoyaona.
Na hilo ndilo ninalolitaka kujua. I have a big doubt over these allegations. Hawa wanatumiwa? Na nani? Maswala yepi ya kitaifa wamekuwa kifua mbele kutetea? Nadhani TAJA kwa uandishi wa namna hii mmejichanganya! Pamoja na kuwa Mengi si Hero kwangu bado mmenifanya niamini huyu bwana mnamwandama kwa kutumiwa. Kwa kutumia taaluma zenu za kiuandishi angalia tuhuma zilivyo na mfikirie kwanini abebe Mengi! Mnampa "shavu" bure...Viongozi wa TAJA ni wakina nani? Wanataaluma gani? na wafanyakazi vyombo vipi vya habari?
Isije ikawa ni chama cha waandishi wa habari makanjanja Tanzania
Asha
Nadhani inachekesha,,, pale wanapomtaja, Manji, Basalehe na Malima, wanasahau Edward Lowassa, Andrew Chenge, Basil Mramba, Daudi Ballali, wote hao ni waislamu? Aibu tupu mheshimiwa Hamza KOndo kama kweli ni wewe, ila jamani huu naona ni Mkenge wa kuiondoa JF katika hoja za msingi.... Kondo kama unataka demu karibu