Taja kazi/ biashara unayofanya ili upate connection

Taja kazi/ biashara unayofanya ili upate connection

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,009
Reaction score
61,260
Wakuu kwanini tunaogopana Sana humu ndani wakati sisi ni wananchi wa kawaida kabisa kama wasiojulikana nao wapo humu ndani basi ni wachache hawawezi kutufuatilia watu wote hivyo mnaonaje ukiitumia hii fursa ya uzi huu kusema kazi yako au biashara yako huenda watu tukahitaji huduma yako ikawa faida kwako.

Kama unaogopa kusema wewe ni daktari basi taja hata hospital uliyopo ili tukiugua tuje kutibiwa kwenu kwa hisani yako..Kama uko bank basi taja tu bank fulan tawi fulan ili tuje au Kama mfanyabiashara taja duka lenu linaitwaje au kama uko kwenye kampuni flan itaje hata Kama NI TCC au TBL sema sisi tutazidi kuvuta sigara na kunywa pombe kwa ajili yako tu lengo ni mpate maslahi.

Kama ni mwalimu sema basi hata shule ulioajiriwa huenda tukaguswa kusomesha shuleni kwenu mwalimu.kama ni mpishi sema me niko jikoni hotel flan uone jinsi mtakavyopata wateja wengi msisahauWilaya husika unapofanyia kazi.
 
Walevi ndiyo wenye dili zote kokote pale.
Ukiwa na shida au swala linakusumbua, we nenda baa lazima upate ufumbuzi.
 
Natafuta kazi ya graphic designer au kufanya kazi stationary ,dodoma au arusha. Pia kama unatangazo natengeneza poster za mitanadaoni,vipeperushi,logo,mambango ,rebo za bidhaa n.k kwa bei nafuu kabisaa karibuni 0744412607.
 
Walevi ndiyo wenye dili zote kokote pale.
Ukiwa na shida au swala linakusumbua, we nenda baa lazima upate ufumbuzi.
Baba mdogo ni prisoner officer aliandikiwa masharti na daktari kuwa asinywe pombe. Hapo nimemaliza A level akawa ananichukua twende wote bar kwa vile sinywi pombe.

Nilikuwa namshangaa kwa nini mpaka aliponambia dili zote muhimu, magari, mashamba na viwanja alivitoa bar. Hawezi acha kwenda maana work mates wake anajua mishe zao hawana jipya la kumwambia kazini
 
Back
Top Bottom