Sio bure nadhani kuna kipapai tumepigwa ama la tumemkosea Muumba wetu ama mizimu yetu! Vyovyote iwavyo kuna mahali tumekosea ama kupungukiwa na kitu kikubwa sana!
Maumivu ya bando wala hayaumi tena, bei za bidhaa na vyakula kupaa wala sio habari ya kuumiza kichwa tena.. Maji kudra zimeokoa jahazi
Sasa haya mengine haya hizo fafanuzi zake kama ukiamua kuziweka kwenye jarida moja unaweza kutengeneza bonge la comedy show ama ukapata homa ya vipindi
Fafanuzi za umeme usio imara
Fafanuzi za mikopo ya matrilion
Fafanuzi za deni la taifa
Fafanuzi za miradi iliyojaa vinguzumkuti na upigaji wa kufa mtu
Kiboko msheli ni fafanuzi za treni ya umeme, mabehewa ya SGR, gharama zake, aina zake nknk
Kuna nini Mungu baba wa mbinguni!?
Wafafanuzi sio wamoja
Wafafanuzi hawaelewani kila mmoja anatoa kioja chake kisha anapotea.. Taifa linaumwa!
Huko chawala wanasagiana kunguni, huko ndiko wamechanganyikiwa kabisa.. Hotuba zao zilizochafua hali ya hewa nazo zimekodishiwa wafafanuzi...wakifafanua sasa unaweza ukavua nguo ukimbie.. Ni mahututi wanahudumia wagonjwa[emoji2827]
Ukikaa pembeni na kupiga taswira haya matukio yote ni kama vile taifa liko kwenye wodi ya wanaougua uchizi.. Inauma sana!
Tukiona humu kila uchao watu wanatangaza kutaka kujiua basi tambua taifa linaumwa na limechanganyikiwa kabisa...![emoji1544][emoji2827]