Taifa limechanganyikiwa?

Taifa limechanganyikiwa?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
370,591
Reaction score
858,064
Sio bure nadhani kuna kipapai tumepigwa ama la tumemkosea Muumba wetu ama mizimu yetu! Vyovyote iwavyo kuna mahali tumekosea ama kupungukiwa na kitu kikubwa sana!

Maumivu ya bando wala hayaumi tena, bei za bidhaa na vyakula kupaa wala sio habari ya kuumiza kichwa tena, maji kudra zimeokoa jahazi.

Sasa haya mengine hata hizo fafanuzi zake kama ukiamua kuziweka kwenye jarida moja unaweza kutengeneza bonge la comedy show ama ukapata homa ya vipindi.

Fafanuzi za umeme usio imara.
Fafanuzi za mikopo ya matrilion.
Fafanuzi za deni la taifa.
Fafanuzi za miradi iliyojaa vinguzumkuti na upigaji wa kufa mtu.
Kiboko msheli ni fafanuzi za treni ya umeme, mabehewa ya SGR, gharama zake, aina zake n.k.
Kuna nini Mungu baba wa mbinguni!?

Wafafanuzi siyo wamoja, wafafanuzi hawaelewani kila mmoja anatoa kioja chake kisha anapotea. Taifa linaumwa!

Huko chawala wanasagiana kunguni, huko ndiko wamechanganyikiwa kabisa. Hotuba zao zilizochafua hali ya hewa nazo zimekodishiwa wafafanuzi, wakifafanua sasa unaweza ukavua nguo ukimbie. Ni mahututi wanahudumia wagonjwa[emoji2827].

Ukikaa pembeni na kupiga taswira haya matukio yote ni kama vile taifa liko kwenye wodi ya wanaougua uchizi.. Inauma sana!

Tukiona humu kila uchao watu wanatangaza kutaka kujiua basi tambua taifa linaumwa na limechanganyikiwa kabisa...![emoji1544][emoji2827].
giphy.gif
 
Baada ya watu kubanwa na kuambiwa wazi ...Uhuru wao Una limit ...not to that extent..Kwa miaka 6...
Kinachotokea sasa ni too much freedom ya kulalamika na kulaumu...
Watu wanapata sehemu ya kuondoa machungu Yao tu..new freedom ina mambo yake
 
Baada ya watu kubanwa na kuambiwa wazi ...Uhuru wao Una limit ...not to that extent..Kwa miaka 6...
Kinachotokea sasa ni too much freedom ya kulalamika na kulaumu...
Watu wanapata sehemu ya kuondoa machungu Yao tu..new freedom ina mambo yake
Na hizi fafanuzi je?
 
Sio bure nadhani kuna kipapai tumepigwa ama la tumemkosea Muumba wetu ama mizimu yetu! Vyovyote iwavyo kuna mahali tumekosea ama kupungukiwa na kitu kikubwa sana!

Maumivu ya bando wala hayaumi tena, bei za bidhaa na vyakula kupaa wala sio habari ya kuumiza kichwa tena.. Maji kudra zimeokoa jahazi

Sasa haya mengine haya hizo fafanuzi zake kama ukiamua kuziweka kwenye jarida moja unaweza kutengeneza bonge la comedy show ama ukapata homa ya vipindi

Fafanuzi za umeme usio imara
Fafanuzi za mikopo ya matrilion
Fafanuzi za deni la taifa
Fafanuzi za miradi iliyojaa vinguzumkuti na upigaji wa kufa mtu
Kiboko msheli ni fafanuzi za treni ya umeme, mabehewa ya SGR, gharama zake, aina zake nknk
Kuna nini Mungu baba wa mbinguni!?

Wafafanuzi sio wamoja
Wafafanuzi hawaelewani kila mmoja anatoa kioja chake kisha anapotea.. Taifa linaumwa!

Huko chawala wanasagiana kunguni, huko ndiko wamechanganyikiwa kabisa.. Hotuba zao zilizochafua hali ya hewa nazo zimekodishiwa wafafanuzi...wakifafanua sasa unaweza ukavua nguo ukimbie.. Ni mahututi wanahudumia wagonjwa[emoji2827]

Ukikaa pembeni na kupiga taswira haya matukio yote ni kama vile taifa liko kwenye wodi ya wanaougua uchizi.. Inauma sana!

Tukiona humu kila uchao watu wanatangaza kutaka kujiua basi tambua taifa linaumwa na limechanganyikiwa kabisa...![emoji1544][emoji2827]
giphy.gif
Niliwahi soma ushuhuda wa Prof. Iyke Nathan Uzorma The grand master now in Christ.( Mkuu wa wachawi amrudia Kristo). Sikukumbuki ni part ya ngapi ila kwenye huo ushuhuda kuna sehemu alieleza kuwa kuna:-

1.Uchawi wa kuroga mtu mmoja,
2.Kuna uchawi wa kuroga familia,
3 Uchawi wa kuroga ukoo mzima na
4.Uchawi wa kuroga nchi nzima.

Watu wengi wanashangaa kwanini kuna nchi hazina rasilimali za kutosha lakini zimeendelea kuliko nchi zenye ardhi nzuri,maji,misitu,wanyama na madini ya kila aina?

Si bure Mshana tumerogwa akili ndio maana tunakuwa km mazombi tu. Haiwezekani mafuta juu,chakula juu,umeme hamna,maji hamna, deni la taifa juu na bado raia tupo kimya tu![emoji15][emoji15][emoji15].
 
Back
Top Bottom