Tai hapigani na nyoka ardhini

Tai hapigani na nyoka ardhini

Atamchukua juu angani na kubadilisha uwanja wa vita, na kisha atamwachilia nyoka angani.

Nyoka hana stamina, hana nguvu na hana usawa hewani. Hivyo kushindwa mapigano ni hakika kwa asilimia 100

lakini haina maana kwamba nyoka ni mdhaifu la hasha. Udhaifu wake unatokana na uwanja wa vita usio wake tofauti na ardhini ambapo ana nguvu ya kujeruhi kuumiza na hata kusababisha mauti.

Chukua vita yako katika ulimwengu wa roho kwa kuomba na ukiwa katika ulimwengu wa roho Mungu anachukua vita vyako.

Usipigane na adui katika eneo lake la faraja, badilisha uwanja wa vita kama Tai na Mungu akusimamie kwa maombi yako ya bidii na ya dhati ya moyo wako.

Utakuwa na uhakika wa ushindi safi!

View attachment 2790189

Sent using Jamii Forums mobile app
Mshana Jr. leo umeongea kitu cha maana mno, nadhani wokovu umeshafika nyumbani kwako kama ulivyofika kwa zakayo. infact, hakuna aliyewahi kumshinda shetani akienda kimwili, na ili shetani ashinde mwanadamu huwa either anamsogeza kwenye ulimwengu wake wa giza, au anamwendea kimwili ili mwanadamu aingie king kupambana kimwili na anashinda asubuhi kabisa. mwanadamu chali. ila ukimwendea shetani kiroho kwa Nguvu za Mungu, hana nguvu hata chembe, anakimbia. ndio maana kushindana kwetu si kwa damu na nyama, ni kwa roho, katika ulimwengu wa roho. huko ndiko tunapigana na wakuu wa anga, wakuu wa giza, falme na mamlaka na majeshi ya pepo wabaya,yapo kibao huko ukienda kichwakichwa bila Nguvu za Mungu au ukienda kimwili, yana nguvu balaa.
 
Back
Top Bottom