Taharuki!kiwanda cha A-Z chadaiwa kutiririsha maji yenye sumu ,watu na mifugo wako hatarini

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
228
250
Taharuki!kiwanda cha A -Z chadaiwa kutiririsha maji machafu yanayosababisha athari kwa watu na mifugo.

Katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya wananchi wa kata ya Ormoti jijini Arusha wamekilalamikia kiwanda cha A -Z kwa kutiririsha maji machafu yanayoleta athari kwa wananchi na mifugo.

Wananchi hao kwa nyakati tofauti wameeleza kwamba maji hayo ambayo hubadilika rangi yamekuwa yakitoka ndani ya kiwanda hicho na kuelekea mashmbani mwao na kupelekea mazao yao kuharibika.

Hatahivyo,uongozi wa mtaa huo umekiri kupokea kero hiyo kutoka kwa wananchi mbalimbali na kusisitiza kwamba wanayafanyia kazi.

Wananchi hao walikilalamikia kiwanda hicho kuwa kimekuwa na desturi ya kufungulia maji machafu yanayobadilika rangi jambo linaloleta kero mtaani kwao.

Walisema kwamba maji hayo hutoa harufu Kali ambapo baadhi ya mifugo yao imeshapata madhara na mingine kupoteza uhai baada ya kunywa maji hayo.

"Ng'ombe wetu wamekufa baada ya kunywa haya maji na hata mazao yameharibika maana haya maji yana kemikali ya ajabu serikali itusaidie" alisema mkazi wa eneo hiloHatahivyo,walidai kwamba hivi karibuni baadhi ya maofisa wa mazingira kutoka baraza la usimamizi wa mazingira nchini(Nemc) walifika katika eneo lao na kusikiliza kero hiyo na kuhaidi kuchukua hatua kuhusu hali hiyo lakini mpaka sasa hawajachukua yoyote.

"Baadhi ya maofisa wa Nemc walikuja hapa na kutusikiliza wakahaidi kurudi baada ya wiki mbili lakini mpaka sasa kimya yaani kila mtu anapoingia ndani ya kiwanda hicho hatoki salama maana tunahisi wanapewa chochote" alisema mkazi wa eneo hi


Mwenyekiti Wa Mtaa huo Charles Mollel sanjari na viongozi wa serikali ya mtaa walisema kwamba tayari wameshapokea malalamiko hayo kutoka kwa wananchi na kwa sasa wanayafanyia kazi.

Viongozi hao wamedai kwamba kero ya kiwanda hicho kutiririsha maji hayo ni ya muda mrefu katika eneo hilo lakini wao wamejipanga kukutana na pande zote ili kujua kiini cha malalamiko hayo kabla ya kufanya maamuzi.

Uongozi wa kiwanda cha A-Z Mara kwa Mara wametafutwa na waandishi wa habari ili kuzungumzia malalamiko hayo lakini wameshindwa kutoa ushirikiano juhudi za kuwatafuta bado zinaendelea.

Mwisho.
 

Attachments

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,199
2,000
Hicho kiwanda kinatengeneza nini?
Wengine hatukijui Mkuu samahani lakini
Yaani hao wahusika wanatoa leseni bila masharti ya kulinda afya za watu?
Kweli tuna safari ndefu sana


Sent from my iPhone using Tapatalk
 

wise boi

JF-Expert Member
Aug 9, 2017
296
1,000
Tunalishwa sumu nyingi kwenye mifugo ambazo zinatokana na uchafuzi wa mazingira
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom