NEMC yakifunga kiwanda cha A TO Z Arusha,viongozi waingia mitini

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
BARAZA la Taifa la Hifadhi za usimamizi wa Mazingira NEMC , limekifungia kiwanda cha kutengeneza chandarua na Nguo cha A to Z kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha,kwa muda usiojulikana kutokana na kutiririsha maji taka yanayotoka kiwandani hapo kwenda kwenye makazi ya watu kinyume cha sheria.

Uamuzi huu umetolewa jana na mhandisi, Redekta samweli Mkurugenzi wa uzingatiaji na utekelezaji wa sheria za mazingira Nemc baada ya kiwanda hicho kukaidi maelekezo ,maonyo na adhabu ya faini yanayotolewa kiwandani hapo kutokana na uharibifuu wa mazingira unaotokana na utiririshaji

"Tunasitisha shughuli zote za zinazohusiana na uzalishaji wa maji taka ,mpaka hapo kiwanda hicho kitakapofanya marekebisho maelekezo ya mamlaka husika"

Hata hivyo wakati baraza hilo la mazingira likiwa kiwandani hapo na kutembelea mfumo wa maji taka ,viongozi wakuu wa A to Z hawakuwepo ofisini huku taarifa zikidai kwamba wapo nje ya nchi.

Naye Mkurugenzi mkuu wa NEMC, dkt Samwel Gwamaka alisema kuwa kiwanda hicho cha A to Z kwa muda mrefu kimeshindwa kutii na kutekelez maelekezo ya wataalamu juu ya utiririshaji wa maji taka yanayozalishwa kiwandani hapo kwenda kwenye makazi ya watu , licha ya kuwepo maelekezo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa ngazi mbalimbali.

Naye meneja wa NEMC kanda ya Kaskazini, Lewis Nzali alisema kuwa ofisi yake tayari imepeleka Amri halali ya Baraza hilo katika kiwanda hicho cha A to Z ili kuzuia uzalishaji unaotokana na maji maji hadi hapo watakapofanyia marekebisho matakwa ya baraza hilo ili kukidhi mfumo wa maji taka.

"Sisi tumefunga utiririshaji wowote wa maji ambayo machafu, hayajatibiwa, ambayo yanarangi na harufu ,hatutaki watiririshe maji ambayo hayajatibiwa "

Alisisitiza kuwa NEMC imechoka na malalamiko ya wananchi ndio maana leo wamekuja kufunga kwa kuweka utepe na iwapo wataendelea kutiririsha hatua kali zaido zitachukuliwa.

Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya waziri wa mazingira, Suleiman Jaffo ambaye hivi karibuni alitembelea kiwanda hicho na kutoridhishwa na mfumo wa maji taka yanayotoka kiwandani hapo kuelekea kwenye makazi ya watu.

Kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda vikubwa hapa nchini kilichoajiri wafanyakazi zaidi ya 8000 wengi wao wakiwa wanawake.

Hata hivyo uongozi wa kiwanda hicho umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu kutokana na kukiukaa sheria za mazingira kwa kutozingatia athali zinazotokana na uzalishaji wa maji taka yenye kemikali na kuyaelekeza kwenye makazi ya watu.
 
BARAZA la Taifa la Hifadhi za usimamizi wa Mazingira NEMC , limekifungia kiwanda cha kutengeneza chandarua na Nguo cha A to Z kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha,kwa muda usiojulikana kutokana na kutiririsha maji taka yanayotoka kiwandani hapo kwenda kwenye makazi ya watu kinyume cha sheria.

Uamuzi huu umetolewa jana na mhandisi, Redekta samweli Mkurugenzi wa uzingatiaji na utekelezaji wa sheria za mazingira Nemc baada ya kiwanda hicho kukaidi maelekezo ,maonyo na adhabu ya faini yanayotolewa kiwandani hapo kutokana na uharibifuu wa mazingira unaotokana na utiririshaji .

"Tunasitisha shughuli zote za zinazohusiana na uzalishaji wa maji taka ,mpaka hapo kiwanda hicho kitakapofanya marekebisho maelekezo ya mamlaka husika"

Hata hivyo wakati baraza hilo la mazingira likiwa kiwandani hapo na kutembelea mfumo wa maji taka ,viongozi wakuu wa A to Z hawakuwepo ofisini huku taarifa zikidai kwamba wapo nje ya nchi.

Naye Mkurugenzi mkuu wa NEMC, dkt Samwel Gwamaka alisema kuwa kiwanda hicho cha A to Z kwa muda mrefu kimeshindwa kutii na kutekelez maelekezo ya wataalamu juu ya utiririshaji wa maji taka yanayozalishwa kiwandani hapo kwenda kwenye makazi ya watu , licha ya kuwepo maelekezo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa ngazi mbalimbali.

Naye meneja wa NEMC kanda ya Kaskazini, Lewis Nzali alisema kuwa ofisi yake tayari imepeleka Amri halali ya Baraza hilo katika kiwanda hicho cha A to Z ili kuzuia uzalishaji unaotokana na maji maji hadi hapo watakapofanyia marekebisho matakwa ya baraza hilo ili kukidhi mfumo wa maji taka.

"Sisi tumefunga utiririshaji wowote wa maji ambayo machafu, hayajatibiwa,ambayo yanarangi na harufu ,hatutaki watiririshe maji ambayo hayajatibiwa "

Alisisitiza kuwa NEMC imechoka na malalamiko ya wananchi ndio maana leo wamekuja kufunga kwa kuweka utepe na iwapo wataendelea kutiririsha hatua kali zaido zitachukuliwa .

Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya waziri wa mazingira,Suleiman Jaffo ambaye hivi karibuni alitembelea kiwanda hicho na kutoridhishwa na mfumo wa maji taka yanayotoka kiwandani hapo kuelekea kwenye makazi ya watu .

Sawa
 
Hiki kiwanda hakikosi kadhia,Kuna mwaka flan lilikuwa na mgogoro na wafanyakazi wake kuhusiana na maslah yao,inaonekana kinaendeshwa kienyeji sana,haiwezekani kiwanda kikubwa hivyo kikose miundombinu ya kuzuia maji yenye chemicals kwenda kwenye makazi ya watu,huu ni uuwaj
 
BARAZA la Taifa la Hifadhi za usimamizi wa Mazingira NEMC , limekifungia kiwanda cha kutengeneza chandarua na Nguo cha A to Z kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha,kwa muda usiojulikana kutokana na kutiririsha maji taka yanayotoka kiwandani hapo kwenda kwenye makazi ya watu kinyume cha sheria.

Uamuzi huu umetolewa jana na mhandisi, Redekta samweli Mkurugenzi wa uzingatiaji na utekelezaji wa sheria za mazingira Nemc baada ya kiwanda hicho kukaidi maelekezo ,maonyo na adhabu ya faini yanayotolewa kiwandani hapo kutokana na uharibifuu wa mazingira unaotokana na utiririshaji .

"Tunasitisha shughuli zote za zinazohusiana na uzalishaji wa maji taka ,mpaka hapo kiwanda hicho kitakapofanya marekebisho maelekezo ya mamlaka husika"

Hata hivyo wakati baraza hilo la mazingira likiwa kiwandani hapo na kutembelea mfumo wa maji taka ,viongozi wakuu wa A to Z hawakuwepo ofisini huku taarifa zikidai kwamba wapo nje ya nchi.

Naye Mkurugenzi mkuu wa NEMC, dkt Samwel Gwamaka alisema kuwa kiwanda hicho cha A to Z kwa muda mrefu kimeshindwa kutii na kutekelez maelekezo ya wataalamu juu ya utiririshaji wa maji taka yanayozalishwa kiwandani hapo kwenda kwenye makazi ya watu , licha ya kuwepo maelekezo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa ngazi mbalimbali.

Naye meneja wa NEMC kanda ya Kaskazini, Lewis Nzali alisema kuwa ofisi yake tayari imepeleka Amri halali ya Baraza hilo katika kiwanda hicho cha A to Z ili kuzuia uzalishaji unaotokana na maji maji hadi hapo watakapofanyia marekebisho matakwa ya baraza hilo ili kukidhi mfumo wa maji taka.

"Sisi tumefunga utiririshaji wowote wa maji ambayo machafu, hayajatibiwa,ambayo yanarangi na harufu ,hatutaki watiririshe maji ambayo hayajatibiwa "

Alisisitiza kuwa NEMC imechoka na malalamiko ya wananchi ndio maana leo wamekuja kufunga kwa kuweka utepe na iwapo wataendelea kutiririsha hatua kali zaido zitachukuliwa .

Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya waziri wa mazingira,Suleiman Jaffo ambaye hivi karibuni alitembelea kiwanda hicho na kutoridhishwa na mfumo wa maji taka yanayotoka kiwandani hapo kuelekea kwenye makazi ya watu .

Kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda vikubwa hapa nchini kilichoajiri wafanyakazi zaidi ya 8000 wengi wao wakiwa wanawake.

Hata hivyo uongozi wa kiwanda hicho umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu kutokana na kukiukaa sheria za mazingira kwa kutozingatia athali zinazotokana na uzalishaji wa maji taka yenye kemikali na kuyaelekeza kwenye makazi ya watu.
A-Z inanikumbusha moto uliosababishwa na gesi na kuua watu.
 
Ilikuwaje
Mtungi mkubwa wa gesi ulivuja na mioto ikasambaa eneo lote linalozunguka kiwanda ikiwapamba watu na kuwa kama utambi, baadhi yao walijitupa kwenye mto Themi ila ukiibuka unao, ngoma ilikuja baada ya uamuzi wa kijinga kulifunga mnyororo tangi la gesi ili walivute, kilichotokea likalipuka gari lote likaungua na watu waliokuwepo.
 
Back
Top Bottom