DOKEZO Lameck Airo acha kutiririsha maji machafu barabarani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

The wave

JF-Expert Member
Feb 27, 2021
280
312
Wanajamii nimekuwa napita karibu kila siku barabara kuu ya Nyerere inayotoka Mwanza kuelekea Musoma. Ukifika eneo la Kisesa Isangijo kuna kiwanda kinachakata samaki.

Inasemekana mmiliki ni Lameck Airo aliyekuwa mbunge wa Lorya. Kiwanda hiki kinatiririsha maji machafu barabarani tena yanatoa harufu mbaya na kali. Kiasi kwamba hata wanaopita na magari huziba pua zao, ajabu si bwana afya au watu wa mazingira wamefuatilia suala hili.

Wanapita na kujifanya hawaoni sijui kuna nini, watu wanaendelea kuumia. Tafadhali NEMC fuatilieni hii issue msikae tuu ofisini na kupulizwa kiyoyozi.
 
Ungesoma ukawa MKURUGENZI WA NEMC nchi ingekua pazuri saana. Unajituma na una kitu, UTAFIKA MBALI SANA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom