TAHAJUDI (Meditation): Mbinu, faida, aina na mambo ya kuzingatia

Ahsante, japo dunia ya leo inaweka suala la miditisha kwenye kukazia fahamu ama kutuliza akili, kwenye tamaduni za muda mrefu katika ujuzi, elimu na nidhamu za kiimani na dini kama Bara Hindi, kuna kupambanua mengi katika sura, muktadha na bidii ya kufungua milango ya fahamu, uwezo na taamuli.

Hapo juu umeweka vitendo nidhamu-mkao kadhaa kama ni tahajudi kwa maana ya miditisha hivyo si miditisha hasa ila kiufasaha wa mambo vinaanguakia kwenye vitu kama 'Dharana' ama 'Tratak' kwa mafundi wa mambo hayo. Hebu tazama 'dhyana' na halafu angalia 'vipassana' ni vitu gani na vinachimbukia wapi... Yoga ina mengi kwa mfano, lakini yenyewe hasa ndiyo hutumia maunganio ya mwili, akili na nafsi roho ili kunasibu mfunguko ama mkunjukuko wa fahamu kuelekeo kwenye utambuzi usio wa kawaida wa maumbo, hisia, misukumo na uhalisia wa nje na ndani wa yote. Unaweza kuwa kwenye nidhamu za kiyoga kwa ajili ya afya ya kimwili na kiakili. Lakini daraja bora kabisa ni Yoga itakayokusaidia kujitambua ulipo kuiingiliana na kosmosi yote. Yoga si dini, ni nidhamu na safari ya kiroho. Miditisha nayo katika daraja la ubora wake wenyewe kabisa si kitendo cha kiimani au dini tu ila ni sayansi kamili ya uzima na fahamu. Yoga daima hutimilizwa na miditisha lakini kwa uhuru kamili, hakuna kutumia namna nyenzo ya kukazia fahamu ili kubadili utumikishi wa akili na uwezo wake wote hata ule wenye kuweza kuleta yale yaliyozaidi ya kawaida kwa maana ya uhusiano wa 'boddhi' na 'siddhi' kwenye maarifa ya Yoga; bali ni kuachana na akili yenye na basi kurudi kwenye asili yenyewe ya uhai na uzima wote. Hiyo ndiyo huwa ni wokovu kamili na taamuli kamili... Kweli ya Mwisho.
 
ahsante mtambuzi ubarikiwe kwa somo zuri nimeipenda zaidi ya mshumaa nitaifanya usiku wa leo naamini naweza hilo
na ya namba ni nzuri zaidi kwa wanafunzi ingawa ni ngumu kidogo nimejaribu hapa
 
Mkuu kidogo niongeze ufafanuzi wa Neno "TAHAJJUD"....Tahajudi ni neno la kiarabu lenye Maana ya kufanya juhudi ya kujilazimisha jambo lisilo la lazima....TAHAJJUDI ni verb ya nown ya "JUHDI" ukiongeza "Tah" ndo inakua Kitendo...Kiswahili itakua kimetohoa hili neno nafikiri.....Katika Uislam Ibada za kujitolea kama sala za usiku, funga za Juma tatu na Alhamis hizi kwa ujumla huitwa Tahajudi....
 
Ndiyo left back gunner nilipoona neno tahajjud linatumika hapa nikapata na hofu tunaanza kutaka kutohoa vibaya lugha, isije kuleta tatizo kwa wanalugha wanaochipukia katika kupata mzizi wa maana ya jambo.

Ninadhani tutohoe tu meditation kuwa miditisha... Halafu kwa nini tusitohoe moja kwa moja kutoka kwenye maneno ya kihindi? Hilo neno tahajudi kwa maana ya kiingereza kutajwa ni namna ya 'concetration' basi tuseme ni 'dharaa/dharana'...

Kitu cha kukaziwa fahamu huitwa 'tratak' na bidii ya yake kuitwa dharana-- ilivyo kimaksudio , jitihada ni kubadili uwezo wa akili kupitia kwenye 'jicho la tatu' ambalo ni lensi ya utambuzi iliyo ni tezi ya Pineli ili hiyo kuanza kudaka habari na taarifa hata zilizo nje ya fahamu ya kuona kwa wakati ama hata nje ya mzingo wa uono wa mahala afanyiapo mwenye kufanya hiyo.
 
asante mheshimiwa.nipo job nimejaribu hii ya namba ila naona najiwa na usingizi.tuelezee zaidi kuhusu haya mambo.na hii ya ardhi inakuwaje mkuu
 
Machale..... ndio maana naona wanaofanya meditation kama wanga.
7. Husaidia kuimarisha nguvu yako ya
machale pamoja na nguvu zako za
ziada.
Kuna jamaa yangu Rodrick Ntepa aliniambia kaanzisha dini yake inaitwa WANAZARAYO. Na yeye ndiye Mungu wa dini hiyo. Akanifundisha ku meditate. Tulimeditate kwa masaa matatu none stop. Yeye akaniambia alishawahi kumeditate hadi akawa kama mfu. Na siku hiyo alikuwa ameenda kwenye mbingu ya saba ambako anakaa Mungu wa Wakristo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom