Tahadhari zote dhidi ya Corona tunachukua ila hili la Distancing Serikali itusaidie, hasa kwenye daladala

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,940
141,915
Leo jijini Dar es Salaam nimeshuhudia watu wengi wakiwa wamevalia barakoa na maeneo mengi kuna maji tiririka.

Hata benki na TRA nimeshuhudia barakoa za kutosha tu kwa watumishi.

Kiufupi wananchi wanajitahidi kuchukua tahadhari dhidi ya Corona ila kwenye vyombo vya usafiri ndio wanakofelishwa.
Ukiingia kwenye daladala au mwendokasi unaisikia kabisa harufu ya yule malaika Gabriel.

Serikali saidieni wananchi katika eneo hili la distancing.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wadudu wa corona hawana nafasi sehemu yenye joto kali lile fukuto la joto la kubanana mwendokasi na daladala kidudu cha corona lazima kinyooshe mikono juu hilo joto ni zaidi ya kujifukiza
 
Inawezekana kwenye hii vita ya kovidi wajomba hawapo upande wa wananchi. Hizo tahadhari mnazochukua ndio wanazidi kukasirika.
 
Magufuli aongee kwa style ipi hadi muelewe. Amesema million times Tanzania haina corona ila iliyopo ni ndogo
 
Kwakuwa watu walieweshwe kuwa hakukuwa na shida,kama ipo shira sasa waeleweshwe tena kama kuna shida,kwa nguvu ile iliyotumika kuwa julisha kuwa hakuna shida.Vinginevyo ni sawa na kupaka upepo rangi.
 
Mwendo kasi na daladala ukiingia kwa ule mbanano unajikuta una tatizo la upumuaji njia nzima ila ukitelemka tatizo unaona limeisha automatic unapumua kawaida
Kama tunakiri kuna shida,ni muda sasa waimba mapambio wote kuingia kazini kwa umoja wetu kuwaelimisha watu kwa manufaa yetu na wote.
 
Askofu Rashidi Gwajima akiwa bungeni amesema mswala ya social distance ni upuuzi na hayana maana. Waziri wa afya alionekana kupendezwa na kauli hii ya huyu mtafuna kondoo kwa kupiga makofi ikiwa inamaanisha ndiyo msimamo wa serikali.
 
Askofu Rashidi Gwajima akiwa bungeni amesema mswala ya social distance ni upuuzi na hayana maana,
Waziri wa afya alionekana kupendezwa na kauli hii ya huyu mtafuna kondoo kwa kupiga makofi ikiwa inamaanisha ndiyo msimamo wa serikali.
Poleni bwashee kwa mitambo ya gongo iliyokamatwa huko Rombo!
 
Leo umejitahidi kuongea UKWELI
Mara nyingi unaefikiri katika mazingira fulani kuwa hana akili sii kweli,ila tu wakati mwingine ni akili za tumboni zinatumika.a.k.a ugali kwani mwingine anasema kwavile mkono unaendakinywani na maisha yanajiendea nisumbuke nini,ila madhara yanayowagusa wote,Yana warejesha kwenye ufahamu wa asili.
 
Mara nyingi unaefikiri katika mazingira fulani kuwa hana akili sii kweli,ila tu wakati mwingine ni akili za tumboni zinatumika.a.k.a ugali kwani mwingine anasema kwavile mkono unaendakinywani na maisha yanajiendea nisumbuke nini,ila madhara yanayowagusa wote,Yana warejesha kwenye ufahamu wa asili.
Hahahaaaa..... Mwenzio anazungumzia ukweli bwashee!

Akili na ukweli ni vitu viwili tofauti!
 
Back
Top Bottom