Dreamliner
JF-Expert Member
- Jan 17, 2010
- 2,034
- 215
Wadau.. Mfanyakazi mwenzangu, ameibiwa LAPTOP baada ya kuwapa lift watu watatu, mmoja akiwa ni mwanafunzi FAKE. Alikuwa anatoka maeneo ya MAJOHE asubuhi kuelekea maeneo ya Gongolamboto halafu kibaruani. Alipofika Relini, Watu wawili na mwanafunzi FAKE wakaomba lift. Jamaa alipoona na mwanafunzi yupo. akasimama na kuwapa lift.
Wale watu, walilaza kiti cha nyuma na kupata ACCESS kwenye buti ambako alikuwa ameweka Laptop. Wakaitoa kwenye BAG lake, na kuupitisha chini ya kiti cha abiria aliyeko upande wa kushoto wa gari mbele, (Mwanafunzi fake) kwani alipoingia garini, aliweka madaftari yake chini. Hivyo basi, alipofika Pugu Sec, akatelemka, na kuchukua madaftari (Counters) yake na kuunganisha na laptop ya jamaa.
Jamaa alikuja kushtuka baada ya kufika kibaruani na kuona hana laptop na alijua kaibiwa kwani zile shughuli aliziona zikifanyika, lakini hakuhisi kama ni wizi ulikuwa unaendelea. Wale wezi wawili wakatelemkia Gongo la Mboto..
Hivyo hata nyuma ya BUTI la gari sio salama tena. Dawa ni kutompa mtu yeyote lift.