Tahadhari: Usalama wa Magari Quality Centre shopping Mall Dar

Tahadhari: Usalama wa Magari Quality Centre shopping Mall Dar

whitehorse

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2009
Posts
2,570
Reaction score
4,455
WanaJF wenzangu, napenda kuchukua nafasi hii kuwatahadharisha na usalama wa magari yenu mnapoyapaki pale quality centre hali ya usalama inazidi kupotea. Sasa imekuwa sawa na mlimani city ya zama zile. Wale wezi wa kubomoa vioo na kukomba vilivyomo wamehamia rasmi kule nyerere road kwa sasa. Waambie ndugu jamaa zako na rafiki zako mimi ni muhanga nimeibiwa kabegi kana nguo za mtoto walidhani labda ni vitu vya maana. Nikaenda pale police chang'ombe kureport nikaambiwa kwa sasa kesi kuhusu wizi wa vitu kwenye magari mahali pale zinamwagika kila iitwayo siku. Na sijawahi kuhizi hivyo kutokana na ulinzi kabambe uliopo pale. Naomba mwenye kusoma habari hii awaambie na wengine.

Sent from Samsung tablet
 
Kuna wale wenye vifua vipana mimi sina imani nao hata kidogo tena kazi kubwa pale wanauza sura na siyo kulinda...May be plan ya mlimani City ya kukaa juu kwenye viota inaweza kusaidia kiasi ila wajameni tuwe makini saaaaaaaaaaaaana.
 
Pole sana mkuu. I can assure you wezi wa pale QC ni wale askari wa pale. Nusura nimshone risasi mmoja Jumapili; nilimkuta live!

Kha! Inawezekana I see cause mimi nilipopaki tu alikuja mmoja akajidai kunisalimia lakini mimacho yote iko kule seat za nyuma sikujali cause najua ni mlinzi. Nikabeba handbag yangu nikatokomea wezi kumbe wale.

Sent from Samsung tablet
 
Kha! Inawezekana I see cause mimi nilipopaki tu alikuja mmoja akajidai kunisalimia lakini mimacho yote iko kule seat za nyuma sikujali cause najua ni mlinzi. Nikabeba handbag yangu nikatokomea wezi kumbe wale.

Habari ndo hiyo! Siku nyingine nenda na kamera. Ile ukipaki tu si atakuja? Mwambie "simama hapo hapo", afu umpige picha pamoja na gari. Kisha mwambie "sasa rudia tena ule usenge wa siku ile"!
 
Pole sana mkuu. I can assure you wezi wa pale QC ni wale askari wa pale. Nusura nimshone risasi mmoja Jumapili; nilimkuta live!

Nawe pole sana, nilitaka kusema huo wizi unafanywa kwa ushirikiano na hao askari.
 
Nikaenda pale police chang'ombe kureport nikaambiwa kwa sasa kesi kuhusu wizi wa vitu kwenye magari mahali pale zinamwagika kila iitwayo siku. Na sijawahi kuhizi hivyo kutokana na ulinzi kabambe uliopo pale. Naomba mwenye kusoma habari hii awaambie na wengine.

walinzi wanahusika na wizi ule kwa kushirikiana na vijana wa Gerezani , Ilala . dakika moja tu wanahitaji kuliacha gari likiwa na milango wazi bila alarm kupiga kelele.
 
walinzi wanahusika na wizi ule kwa kushirikiana na vijana wa Gerezani , Ilala . dakika moja tu wanahitaji kuliacha gari likiwa na milango wazi bila alarm kupiga kelele.

Unachosema naweza kusema ni kweli, last 2 weeks walimuibia mama mmjoja na anafanya kazi hapo na kila siku ana paki hapo. walinzi wale ni wajinga maana wakikuona unapaki gari wanakuja na salam kibao huku wanaangalia kilichomo then wanawapigia hao wezi.
 
Back
Top Bottom