Tahadhari unapolipia huduma kupitia MULA!

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
Napenda kutoa taadhari wana JF na kuwaomba TCRA kuwa makini pindi wanapotoa leseni kwa makampuni ya kutoa huduma za malipo kupitia njia ya simu za mkononi.

Awali nilijulishwa huduma hii na watu wa star times niliposhindwa kulipia king'amuzi kwa njia MPESA wao wakanitajia njia nyingine ya Mula(150*78#).

Lakini sasa nimekuja kubaini ni wajanja fulani ambao pindi unapotumia njia hiyo lolote linaweza kukutokea,

1:Hawa jamaa katika MENU yao wameweka mawasiliano yao ya simu kwamba ukikwama au kukosea huweze kuwapigia lakini hiyo namba HAIPOKELEWI kamwe. namba ni 0755400006

2:Hawa jamaa hawana website bali ukurasa wa FB na katika ukurasa wao hawajaweka namna ya kuwapata bali wanakuelekeza tu,kutumia huduma zao,tazama .Mula Tanzania

3:Ukinunua huduma mhamala unaonesha walishachukua fedha lakini huduma hupati na hakuna namna ya kuwapata.

Nilichopata leo.
Asubuhi nilinunua umeme LUKU wa tsh 9150 na mhamala ukasoma kupitia MPESA,sikupata umeme,kwa kuwa namba yao huwa haipokelewi nimejaribu kuwapigia vodacom wanasema fedha walishachukua na mhamala umekamilika hivyo HAWATARUDISHA FEDHA labda niendelee kuwatafuta..

Kwa kuwa hakuna namna ya kuwapata nimeamua kununua umeme kwa njia nyingine lakini nikaona kutoa taadhari humu,ili husije ukapata hasara kama niliyopata.

Mhamala:
4JU7XW77B7 Imethibitishwa. Tsh9,150 imetumwa kwa CELLULANT MULA kwenye accounti namba 1109929 tarehe 30/10/17 saa 7:33 AM. Salio.......

Byabato
0754527358
MULA.png
 
Updates.

Leo vodacom kupitia MPESA wamefuta ule mhamala na kunirudishia fedha zangu..

Hivyo taadhari bado inaendelea

asante.
 
Na mimi nimeibiwa hivyo na Mula wiki jana. TCRA njoo jamani muokoe jahazi. walazimishe hawa jamaa wawe na ofisi,website,namba ya simu na email. hii black market kwa nini
 
Mimi niliwahi kuona namba zao kupitia haohao startimes na azam. Hua siamini katika miamala ya fedha kwa kampuni ambayo haijulikani imeanzaje. Hivyo miamala mikubwa nilikua nikifanya kupitia mpesa direct. Kilichonipa mashaka mapema ni kwamba ukishapiga menu yao tu halafu usikamilishe muamala, wanakupigia simu kukuuliza kwann. Siku moja mpesa kulikua na shida na umeme umeisha, nikaona ndio muda wa kuwajaribu. Nilitaka kununua umeme wa 5000 ila nikasita, hivyo nililipia 1000 kupitia mula (1000=units 8.2). Muamala ukafanikiwa na mpesa wakaruhusu pesa itoke, (shida ilikua ni upande wa luku tu kwa mpesa ila miamala mingine unafanya kama kawaida) siwafichi, nilipiga simu nikachoka, umeme ukakata kabisa. Ilibidi niendelee kujaribu mpesa hadi muamala ulipokubali, chenga za mula ilikua ukikata simu utaona meseji , wapi. Hadi leo hii naandika hivi sijawahi ona tokeb wala nn. Wakajisahau wakaanza kunikumbusha kua kwa huduma za uhakika nitumie mula. Matusi ya mama zao waliyaoga kama mvua hawajawahi kunipigia tena, walitokomea.
Nb: Mula ni wezi tena mchana kweupe, nilitoa taarifa vodacom. Walinishauri kutokubali kufanya muamala ambao hata kwa mpesa unawezekana kufanywa, indirect. Tuwe makini kwasasa kubet kupo kwa aina nyingi
 
Hivi wanapataje leseni na vibali kupitiaTCRA?
 
Napenda kutoa taadhari wana JF na kuwaomba TCRA kuwa makini pindi wanapotoa leseni kwa makampuni ya kutoa huduma za malipo kupitia njia ya simu za mkononi.

Awali nilijulishwa huduma hii na watu wa star times niliposhindwa kulipia king'amuzi kwa njia MPESA wao wakanitajia njia nyingine ya Mula(150*78#).

Lakini sasa nimekuja kubaini ni wajanja fulani ambao pindi unapotumia njia hiyo lolote linaweza kukutokea,

1:Hawa jamaa katika MENU yao wameweka mawasiliano yao ya simu kwamba ukikwama au kukosea huweze kuwapigia lakini hiyo namba HAIPOKELEWI kamwe. namba ni 0755400006

2:Hawa jamaa hawana website bali ukurasa wa FB na katika ukurasa wao hawajaweka namna ya kuwapata bali wanakuelekeza tu,kutumia huduma zao,tazama .Mula Tanzania

3:Ukinunua huduma mhamala unaonesha walishachukua fedha lakini huduma hupati na hakuna namna ya kuwapata.

Nilichopata leo.
Asubuhi nilinunua umeme LUKU wa tsh 9150 na mhamala ukasoma kupitia MPESA,sikupata umeme,kwa kuwa namba yao huwa haipokelewi nimejaribu kuwapigia vodacom wanasema fedha walishachukua na mhamala umekamilika hivyo HAWATARUDISHA FEDHA labda niendelee kuwatafuta..

Kwa kuwa hakuna namna ya kuwapata nimeamua kununua umeme kwa njia nyingine lakini nikaona kutoa taadhari humu,ili husije ukapata hasara kama niliyopata.

Mhamala:
4JU7XW77B7 Imethibitishwa. Tsh9,150 imetumwa kwa CELLULANT MULA kwenye accounti namba 1109929 tarehe 30/10/17 saa 7:33 AM. Salio.......

Byabato
0754527358View attachment 620570
Kumchangia mwenzio 9150 povu linakutoka. Mbona kwenye harusi unachanga lakhi ?
 
Jamaa wamenipiga na mimi muda huu, nimeelekezwa na jamaangu akidai yeye alihudumiwa juzi, nimemwambia jamaa pesa yangu arudishe
 
Nimekuwa nikiwatumia Mula mara kwa mara katika malipo lakini jana wameninyoosha maana naona wamenipiga hela yangu,nimenunua umeme kwa njia ya mpesa na pesa imekatwa lakini hadi muda huu sijapata umeme. Simu yao ukipiga kuwaulizia tatizo nini,inaita tu hakuna majibu
 
Kwañn usinunue kwà m pesa tu,
Na kwa taarifa yako jàmaa juzi wamepata hasara sanaaa kwahyo hyo hela yako wàmeitumia kulipia hasàra walioipata.
 
Napenda kutoa taadhari wana JF na kuwaomba TCRA kuwa makini pindi wanapotoa leseni kwa makampuni ya kutoa huduma za malipo kupitia njia ya simu za mkononi.

Awali nilijulishwa huduma hii na watu wa star times niliposhindwa kulipia king'amuzi kwa njia MPESA wao wakanitajia njia nyingine ya Mula(150*78#).

Lakini sasa nimekuja kubaini ni wajanja fulani ambao pindi unapotumia njia hiyo lolote linaweza kukutokea,

1:Hawa jamaa katika MENU yao wameweka mawasiliano yao ya simu kwamba ukikwama au kukosea huweze kuwapigia lakini hiyo namba HAIPOKELEWI kamwe. namba ni 0755400006

2:Hawa jamaa hawana website bali ukurasa wa FB na katika ukurasa wao hawajaweka namna ya kuwapata bali wanakuelekeza tu,kutumia huduma zao,tazama .Mula Tanzania

3:Ukinunua huduma mhamala unaonesha walishachukua fedha lakini huduma hupati na hakuna namna ya kuwapata.

Nilichopata leo.
Asubuhi nilinunua umeme LUKU wa tsh 9150 na mhamala ukasoma kupitia MPESA,sikupata umeme,kwa kuwa namba yao huwa haipokelewi nimejaribu kuwapigia vodacom wanasema fedha walishachukua na mhamala umekamilika hivyo HAWATARUDISHA FEDHA labda niendelee kuwatafuta..

Kwa kuwa hakuna namna ya kuwapata nimeamua kununua umeme kwa njia nyingine lakini nikaona kutoa taadhari humu,ili husije ukapata hasara kama niliyopata.

Mhamala:
4JU7XW77B7 Imethibitishwa. Tsh9,150 imetumwa kwa CELLULANT MULA kwenye accounti namba 1109929 tarehe 30/10/17 saa 7:33 AM. Salio.......

Byabato
0754527358View attachment 620570
Sio mhamala kaka ni muamala
 
Dah! Ilikuwa jana tar 15.02.2019, baada ya Mula kukata 11,000 yangu ya kifurushi cha king’amuzi X, nikapokea ujumbe kutoka kwa watu wa King’amuzi kuwa ‘Malipo hayajakamilika, piga 0755400006 kwa maelezo.’ ...haipokelewi, mara haipatikani,,, Voda wakasema hawawezi kusitisha muamala, wakanipa namba nyingine nne za Mula 0732981051, 0742466500, 0754400006 na 0787137371,,, hiyo ya kwanza naambiwa nimekosea namba, ya pili haipatikani ya tatu haipokewi mara haipatikani na hiyo ya mwisho Imefungiwa. Nikajaribu kuwatumia Mula email, sikupata majibu yanayoeleweka; nikawa nimekata tamaa...

Ninachoshukuru baada ya saa2 Mulla wakanirudishia pesa yangu,,, “Your Pay Bill transaction 6BF521S0KG3 of Tsh11,000.00 has been reversed by 276655 - CELLULANT MULA. Please contact 100 for more information. Your account balance is now Tsh12,333.00.”

Ingawa nilifurahi kurudishiwa pesa na nikanunua kifurushi kwa njia nyingine, nasikitika kwamba hao Mula bado wako na wanaweza kupokea malipo ambayo hawawezi kutoa huduma. Kiukweli mwanzoni niliwaamini kwa sababu nilipokea ujumbe kutoka kwa Watu wa king’amuzi changu wakinielekeza kutumia Mula,,, Voda na watu wa king’amuzi wameonyesha wazi kuwa hata wao wamechoka na malalamiko ya kuwahusu Mula, lakini nashangaa ni kwa nini Mula bado wapo. Voda waliniambia tutoe maoni kuwahusu, hakuniambia jinsi gani na wapi, tunaweza kufanyaje wadau?
 
Back
Top Bottom