Tahadhari tusiyoizingatia

Mume wangu alipania safari siku hiyo toka asubuhi anawahi deal lake safari ilitakiwa ianze saa 6, mie nikamuandalia kila kitu, kufika saa 4 nikaanza kupata wooga wa ajab, wasiwasi ikabidi nimwambie usiende hii safari nenda kesho, akaniambia wivu sasa huo mi naenda kikazi, jamanii nilimbembelezaa asiendee hadi chozi ujue hadi nikajishangaa, hee muda umefika wenzake wakaja kumpitia walikua na usafiri binafsi, akawaambia msikieni huyu ananizuia safari wanawake wengine bana maneno kibao akabeba kirago chake huyoo wakaondoka, baada ya nusu saa huyu hapa karudi, heee akaniambia huwezi amini amepaatwa na tumbo ghafla amerudi wenzake wameenda mama miaaa masaa 2 tu simu wamepata ajalii na mmoja kafa palepaleee[emoji24].
 
Duu Mungu wangu
 

Duu...! inasikitisha kwa kweli
 
Nimeisoma habari nikajikuta machozi yanataka kutoka,
2011 baba alipoteza co-owners wenzake wawili ambao tulikua nao kama familia katika ajali ya gari. Usiku aliota ndoto ya ajabu (aliota kaka ake kavunjika mguu halafu anaendesha gari, kwa kua ni mtu wa dini sana alijua nini kinaendelea), akatusimulia mimi na mama, akawapigia na kuwaambia wasisafiri lakini wao walilazimisha ili wawahi kazi (walikua wakitokea Arusha kumzika baba yao wakielekea mbeya). Baba aliumwa ghafla, hakwenda kazini. Saa 6 usiku ilipigwa simu (baba alikua wa mwisho kuongea nao) akaambiwa gari imepata ajali na wote wawili wamefariki.
 
Na vipi zile ishara zinazotokea kimwili mfano wanasema jicho likicheza utaona kitu kibaya, Makalio yakicheza utakaa kwenye msiba, Nywele zikisisimka kuna hatari hapo...Hizi ziko kwenye mlango wa ngapi mshana jr ?
Hizi ziko kiimani zaidi kwenye mila na desturi lakini kiuhalisia ukweli ni mdogo sana...
Ile ni normal muscle twitching lakini kwakuwa maneno huumba basi hiyo hali hutengeneza uhalisia fulani hivi
 
Hizi ziko kiimani zaidi kwenye mila na desturi lakini kiuhalisia ukweli ni mdogo sana...
Ile ni normal muscle twitching lakini kwakuwa maneno huumba basi hiyo hali hutengeneza uhalisia fulani hivi
Kitalaam wanasema mtu ukiwa na msongo wa mawazo ama kuufikirisha sana ubongo basi huchoka na hupelekea macho kucheza, na dawa yake ni kupumzika tu.
 
Umenitoa machozi,leo tar18.06.2016 ni miaka22 tokea tukio hilo!! Mungu awalaze mahali pema daaah, so sad jaman!! Ni mengi nimekumbuka...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…