ndugu sababu kubwa ya unene ni kula!!! kama umefuatilia watu wanene au ukiwa nao karibu ni watu wanapenda sana kula...hata ukitembea nao mkichelewa kula tu atalalamika kama hajala wiki nzima....leo nilikuwa kituo cha basi nasubiri daladala akashuka jamaa mmoja mnene sana cha kwanza alichofanya ni kununua hindi la kuchoma na kuanza kula! hii ndio tabia ya watu wengi wanene wanapenda sana kula....
kundi lingine ni vijana hawa wanaoanza kazi hawa kabla ya kupata kazi kula ilikuwa shida,sasa mtu anapata kibarua anakuwa na kauwezo ka kuchagua ale nini[most of the time junky] basi ndio utamuona miezi mitatu tu tangu apate kazi mishavu hio,tumbo kule basi wenzie wanamsifia hapo ooh mara shvu dodo,kitambi kimetulia mwenyewe anaona sifa kumbe anafuga magonjwa....najua vibonge watanijia juu ila ndio ukweli,wengi wanakuwa wanene kwa sababu ya kula sana na kutofanya mazoezi.