Tahadhari: Siasa isituharibie elimu yetu

kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
5,987
6,646
Kumekuwa na jitihada nyingi wakati wa uchaguzi wanasiasa kutaka kuonesha walivyofanya maajabu, ubaya nipale yanapotengenezwa mambo kinguvu ili kusadifu matakwa ya wanasiasa.

Tunakumbuka 2013 matokeo ya K IV yalinogeshwa ili BRN (big results now) ionekane imeleta output kubwa enzi hiyo.

Hivi sasa niajabu kidogo jinsi shule za serikali nane zimeshika kumi bora matokeo KVI.

Shule za private zimewekeza mmmno natena kadhaa huchukua wanafunzi bora tupu na huwalipa walimu wake vizuri sana,zina vifaa bora kabisa vya kufundishia na kujifunzia sasa leo iweje wazidiwe na shule ambazo wanafunzi hawachujwi, chakula cha wanafunzi ni tabu, walimu hawalipwi vyema, mishahara haiongezeki, madaraja kupanda ni kwashida, wanaidai serikali malimbikizi ya mishahara muda mrefu bila kulipwa,wamepandishiwa kibabe makato ya heslb na wanalalamika awamu ya tano kutokuwajali kama ile ya nne na matatizo mengine mengi.

Bila hata ya utafiti ni dhahiri point tatu zinatafutwa kwabao la mkono nahii ni aibu kuu maana bila elimu bora taifa huishia kusinyaa hata lijengwejengwe vipi. Tunataka elimu bora isiyolongoshewa siasa za ubabe ubabe kulazimisha yasiyoyamkinika.

#ondoa magumashi kwenye elimu.
 
Mkuu sipendi porojo za serikali juu ya elimu, lakini ukweli uliowazi watoto wanaosoma advance kwa shule za serikali wengi ni wazuri kuliko wanoasoma shule binafsi. Kwa o level privates wanafanya vizuri sana....

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Nikweli lkn sidhani kwa kiasi hiko yaani hamna hata seminaries? Labda wengine hatujui vizuri mabadiliko ya kimaajabu yanayofanyika.
 
Nikweli lkn sidhani kwa kiasi hiko yaani hamna hata seminaries?? Labda wengine hatujui vizuri mabadiliko yakimaajabu yanayofanyika
Seminaries bado haziwezi kuwepo hapo mkuu kwanza most of them zipo kwenye category ya below 30 which is siyo rahsi kuoinganisha na shule kama Kibaha yenye watoto mia mbili.

Fatilia hata records za miaka ya nyuma kwa a level out of ten schools government unaweza kuta na zaidi ya tano, huo ni uhalisia.

Kumbuka wale division one unaowajua wengi from private schools o level waanchaguliiwa hizo shule japo wachache wanabaki huku private, sasa wakienda huko hichi ndo kinatokea.

Lakini pia kwa nyongeza tu mwanafunzi anayetoka shule ya kata au let's say day school akachaguliwa kwenda a level boarding school obvious anakuwa na utulivu kwenye kusoma plus anakuwa anajitambua, japo walimu hawafundishi sana kama ambavyo private wanafundisha.

So kujituma na kujitambua kwao ni sababu kubwa kwanini wanafanya vizuri, nadhani wengine wanaweza kuja na maelezo zaidi

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kamanda bhana ndio maana nyie hamuwezi kugusa ikulu hahahahah.
Kwa hiyo wakifeli sana ndio utaratibu
Hahahaa ni tahadhari tuu ili elimuyetu isije chezewa hasa nilipoona best 10 nashule wanazotokea, uwekezaji kwenye elimu bado nimdogo serikali inapaswa kutoridhika kirahisi.
 
Sikubaliani na haya matokeo ni siasa tupu, uwezi kulinganisha ubora wa shule binafsi na za serikali, binafsi zipo juu.

Ndio maana hao wanasiasa watoto zao wanasoma shule m 1.5 kwenda juu ada.wakati govm ni bure.

Sio wanasiasa tu wengi wasomi na watu wenye kipato cha kati na juu watoto zao ni shulu binafsi tu.

Ina maana watoto wa maskini ndio wanasoma best schools?
 
Vyovyote Iwavyo...

Lazima kuna namna hapa.
nimeshtuka sizioni Canosa,Feza boys, Feza girls, St. Mery's mazinde juu nk.
Bila unafiki inabidi tujiulize imetokeaje ghafla shule zenye uwekezaji mkubwa hivi kuzidiwa na shule za kata?!??!!?
 
Mkuu shule advance vijana wako vizuri zaidi Govt, kipindi nipo form 6 pale Azania nilikua nazamia sana Kibaha, watu wanasoma nyie
 
Mkuu shule advance vijana wako vizuri zaidi Govt, kipindi nipo form 6 pale Azania nilikua nazamia sana Kibaha, watu wanasoma note
miaka ya karibuni binafsi zimeongoza sana, iweje mwaka huu matokeo yamebadilika fasta? mbinu gani serikali imetumia?
 
Ni kawaida kwa A level, watoto wengi waliofanya vizuri kwa shule zote za private na government upelekwa government tena vipaji maalumu na ndo mana mara nying A level government hua zinajitokeza nying Top ten
 
Serikali awamu ya tano imefanya ukarabati mkibwa wa miundombinu ya shule kongwe zote na kuziwekea mikakati ya kufaulisha. Mojawapo ni kuwachuja vilaza. Vilaza huwa wanahamishiwa shule nyingine changa.
 
Kama shule ingikuwa ya huko sitimbi sawa

Ila Kama unazungumzia ,kibaha,ilboru,mzumbe,Tabora schools,kilakala,msalato na kisimiri usishangae

Hizi shule hazichukui avarage students

Wanachukua cream tupu

Sina Shaka na ufaulu wa japo huu wa mwaka huu nahisi umenogeshwa kwa namna fulani
 
Ukiwa kilaza shule kama Kibaha au Mzumbe secondary hupati nafasi ng'oooooo.

Usikariri kwamba shule za serikali hakuna mchujo.
 
Mbona ni kawaida tu ,private wajipange msimu ujao wameangushwa na Mimi natamani sana kuona mashindano yakiongezeka mwakani mana sidhan kama private watakubali hali hii ijirudie natarajia kina feza,canossa,st.mary's,ila ndugu zangu govt schools wanasoma nyie acheni na hii coronà ndo iliwaongozea hamu ya kutoboa kabisa mana mwanafunz akifikiria hali shule ilivo walimu hawafundishi alaf nyumban hawakusoma vizuri mwez ulibaki mmoja tu,hata kama n wewe lazima ungekomaa tu
 
Siasa ilishaanza kuharibu elimu kwa njia nyingine tofauti na unavyofikiria.

Huko nyuma nafasi za uongozi wa kisiasa alipata mwenye akili nzuri, elimu na mwadilifu (matendo na maneno yake yalithibitisha).
Siku hizi, lazima ujifanye akili hazipo au ziwe tia maji kweli kweli.

Hapo elimu haijaharibika?
 
Back
Top Bottom