TAHADHARI: Mnaotafuta wachumba JamiiForums

TAHADHARI: Mnaotafuta wachumba JamiiForums

Kuna dada nae alipata humu, wakafunga na ndoa. Baada ya ndoa ndio jamaa kaanza kuonyesha makucha, yaani anazisoma namba mpaka za kichina. Ana mpango wa kuikimbia ndoa.
We mwanamke sikuhizi unalea ndoa nini?
 
Upweke mbaya sana! pole mwaya.
Tatizo liko pale pale ulishakosea kwa kutomchunguza vema kabla hujakubali kuhamia kwake au hata baada ya kuhamia kwake usingejiachia mzima mzima, ungekaa kwa akili ukichunguza kama safari ndio imefika au unatakiwa kuinua mabegi kusonga mbele. Uwiii mbaya zaidi ukafungulia mageti yote ya papuchi na mbegu zikaota... una mimba!! Dah!

Sikulaumu lakini naamini umejifunza kitu.... ningekuwa wewe ningeanza kujiwekea akiba kidogo kidogo, nisingekopa tena ili kumfurahisha..... ongea nae kuona kama atajirekebisha na mnaweza kuendelea kuwa pamoja. Kama haiwezekani anza kujipanga upyaaaa... dunduliza visenti kwa kukaba kila kona, tunza mimba yako hadi utakapojifungua na kupata nguvu utachagua moja. Kazi ni kwako!
Pole sana, but don't give a f*ck mpige chini tu huyo kwasab ni muuaji
 
Pole mwaya, ila umerudia kosa ambalo ulishaanza kupona vidonda vyake. Tabia ni ngozi. Kusimanga kupo ndani ya damu huyo, utashinda la nyumba atahamia la kitanda au sofa. Cha msingi na sekondari si una kazi nzuri kwanini usiondoke hapo kwake? Ukapanga binafsi kuonyesha umekomaa. Una watoto wawili huyo baba yao hanihusu. Je Mungu aliyekusaidia ukawakuza sasa hivi atashindwa? Hata umtegemee kiasi hicho huyo mtu. Ukweli ni huu ulikoseaga, ukakosea tena. Labda uniambie ulizae twins. Lakin kwann uendelee kukosea kuleta Uzi huu its means umeshtuka. Hata kama kumekucha toka nje utaambulia hata jua la vitamin D. Unaweza kulea mimba cha msingi be strong. Jipe moyo u can do it. Aliyekukuzia waliotangulia. Atakukuzia na huyo. Mpole mpz. Ondoka hapo nyumabni. Atakutafuta kwa adabu.Wala usijione ndo mdhambii. Ila jifunze kupitia makosa
 
Salaam zenu bandugu.. Naandika uzi huu ili angalau nipunguze msongo wa mawazo maana naweza kupasuka kichwa...

Mimi ni mdada nina kazi yangu nzuri tu Alhamdulihah na niko na watoto wawili (usiiulize baba yao alipo hayakuhusu) mnamo mwaka jana 2016 mwezi wa tisa hivi nilipata mkaka humuhumu JF aliyekua anatafuta mwanamke.

Tukapanga tukaonana na kwa mujibu wake akanipenda na mimi nikaona si mbaya nikaridhia mawasiliano yakawa makubwa tu. Huyu mkaka aliachana na mkewe wa ndoa ingawa bado si rasmi legally.

Ana 2 watoto na mmoja anaishi nae mwingine yupo kwa mama yake. Akanisisitiza mno nihamie kwake na wanangu ili tuishi pamoja na kusaidiana life.

Nikaona ni jambo jema maana sikua na nyumba sababu bado najikongoja mno kwenye ujenzi... Nikahamia na wanangu na watoto walimpenda kweli yani maisha yalikua murua kwakweli.

At that time, nilikua na vihela vyangu kidogo nikamsaidia kulipa ada ya wanae ya term ya kwanza takriban laki saba unusu. Na yeye nikamsaidia kumlipia ada ya open university asome Law maana alikua hapendi degree yake aliyonayo nikamlipia semester ya kwanza laki 4 na sabini.

Akaanza chuo na amefaulu first year na anatakiwa awe second year mwaka huu. Matumizi ya ndani tunashare ananipa mshahara wake ingawa mdogo lakini nina hulka ya kushukuru.

Tatizo kubwa ni kunisimanga kuhusu nyumba yake yani its too much, na pia mtoto wake hata nimpemdaje haoni anadai nambagua yani kiukweli huyu mtoto age 14 simbagui, kila nacholeta nagawa mara 3 sijawahi kumkaripia wala kumpiga wala kumgusa.

Hata yeye mtoto hana shida na mimi tatizo ni baba yake. Jana nilienda nao saluni ili mwanangu anyoe, sasa ikawa bonge la bifu eti why na yeye wa kwake sijamnyoa. Kiukweli hakua na nywele mbaya.

Akarudi jioni amelewa na kunipiga juu huku akidai mkewe alikua better kwamba ameruka mkojo amekanyaga mavi na kama vipi nihame chumba nikalale na watoto.

Huyu anataka sex mara 3 kwa siku. Usiku mara 2 na asubuhi ya saa 12 mara moja hadi huwa nachelewa job. Yani sex yenyewe haoimbi, ananivuta tu, "lete **** " anaingiza kwa lazima. Yani sex ni daily.

Akishalewa ni kunitukana kuniita ****** na mpuuzi. Jamani huyu mtu nimetoka kuchukua loan ya laki 4 kumlipia mwanae anayesema nambagua.......

Kiukweli kama ni kuingizwa chaka basi mimi ni chaka bovu. Hapa nilipo nina mimba ya miezi 3 na kwakweli moyoni nimeshamkinia....mungu anitangulie kwenye mipango yangu ya kujikomboa kutoka kwenye huu utumwa.

Tuna mwaka mmoja na miezi kama miwili tangu tuanze mahusiano last year......

Jamani kina dada na kina kaka pia msikurupuke kwenye haya mambo! Go slowly, mimi nilikurupuka sababu ya upweke niliokua nao kipindi hicho.
Pole dada ila kumbuka huyo sio mumeo kwa hiyo tafakari kwa kina.

Vv
 
Yaan dah kuna mtu bhana nikajuaga hapa si ndio penyewe kumbe hola, hlf muda huo kulikuwa na mkaka mwingine ananifatilia mbaya ila nikawa sina imani nae. Bwana wee kumbe huyu niliekuwa namchukulia poa ndio muoaji kbs na anajali kuliko maelezo.
Nilijuta sana kupoteza muda wangu kwa lile tahira.
Hilo litaahira uliliopoa humu?kweli usione ukadhani...
 
Manyumbu ya jf yalipokutana yakaunga familia yakizan mapenz yanapatikana mtandaoni
 
Back
Top Bottom