TAHADHARI: Majambazi waunda Task force

Halisi,

Mimi naamini unachosema ni sahihi,sio kwa sababu nina ushahidi bali kwa vile kinawezekana kabisa.Sasa,kuna msemo wa kiswahili kwamba MCHAWI MPE MTOTO AMLEE!Je hudhani kwamba laiti ungewaanika majambazi hao na task force yao hadharani ingewafikishia ujumbe kuwa TUMESHAWANG'AMUA?

kama haoni kuwa inafaa kuwataja sasa hivi ni sawa, ila kama ulivyo sema tuwape watoto wetu watu lele. Hapa halisi ametumia high level language kutuma ujumbe. Kwamba miongoni mwetu kunawatu wamevaa ngozi ya kondo ndio maana kuna upotoshaji mkubwa na wa maksudi taarifa mbali mbali.
 
Katika hali isiyo ya kawaida, majambazi wamejipanga kwa kuunda kikosi kazi (task force) ya kupambana na wenye mali (wananchi) hasa wale wenye kupenda kupiga kelele za "wezi hao!!!! Wezi hao!!!!".

Kazi ya task force hiyo imeanza kwa kasi na tayari baadhi yao wamo humu JF na wanawashughulikia wale wote wanaopiga kelele za mwizi.

Niliwahi kuona pale Kariakoo kibaka anapora simu na anapofukuzwa wenzake wanamsindikiza na kumgeuzia kibao aliyeibiwa na kuanza kumdunda kwamba ndiye mwizi na wakati mwingine mwenye mali huuwawa na kuchomwa moto.

Hali hiyo sasa imeingia kwa majambazi wakuu na sasa kazi imeanza kwa kasi na wale wote wanaopiga kelele za mwizi (akiwamo Mwanakijiji) wajiandae kugeuziwa kibao na kufukuzwa, wakati wao (familia zao) ndio walioibiwa na majambazi wakuu.

Majambazi hao wanakutana usiku na mchana na wana fungu kubwa kwa kazi hiyo ya kujilinda.

Thanks for noting
 
Mkuu Halisi

Heshima mbele.

Hii habari yako ukiisoma kwa makini utagundua vitu viwili muhimu.

Kwanza kuna watu ndani ya jamiiforums.com wamepewa kazi ya kudukuza vyanzo vya maoni nikimaanisha wapi maoni yanayoingia ndani ya tovuti ya jamiiforums yanatoka.

Na pili, vyanzo hivyo ni nani wanaishi wapi na wanafanya nini.

Sasa mimi niliwahi kutoa maoni yangu kuhusu ni kwanini nilijiunga na jamii forums na kama kuna anaependa kurudia kusoma maoni hayo yanapatikana katika unganisho lifuatalo hapo chini:

https://www.jamiiforums.com/habari-...2-why-i-like-jamiiforums-my-thought-week.html

Anyway yote ni maisha yale ya kupigania haki ya yale ya kudhulumu haki na ili upatikane usawa ni lazima vitu hivi vitwangane na apatikane mshindi na lazima mshindi huyo awe mpigania haki.

Nikiwa huku ughaibuni kuna siku nilikutana na moja ya vyanzo vyangu vya habari ambae yeye yupo pale kwenye uwanja wa vita (Tanzania).

Ni very reliable na nnamwamini sana na akaniambia habari ambayo si tu ilinistua bali alinishangaza sana.

Jamaa akaniambia kwamba simu zote ziingiazo nchini Tanzania zinasikilizwa kupata habari ambazo pengine ni "credible" kwa wasikilizaji au kwa "fan" tu.

Mimi nikaelewa kwani mtindo huu ambao kwa kiingereza unaitwa eavesdropping ni ule ambao simu zinasikilizwa na hizo task forces na zikiishachujwa basi wale elements za resistance, magaidi, na wasumbufu wote katika jamii huwa wanafuatiliwa.

Eavesdropping inaweza kufanyika kupitia nyaya za simu au wiretapping, email, njia ya kutuma text kwenye simu au computer, na njia zingine za mawasiliano zinazochukuliwa kuwa ni private. "Eavesdropping" iikinoga inaweza kupelekea kufanya kitu kiitwacho kwa kiingereza snitching njia ambayo mkuu mwenzetu ameeleza ya task force ambapo watu wanatumika kutafuta watu wengine fulanifulani na kuwa-report kwa vyombo vya dola-hususan Police.

Sasa mambo haya hayakatazwi ila yanakiuka haki za msingi ambazo zimo hata kwenye katiba yetu ya pamoja na mengine haki ya kutoa maoni na haki ya kupata habari. Sasa je yamepitishwa na Bunge? au ndio kimefanyika kikao cha dharura na emergence laws zimepitishwa?
 
Last edited:
Wakuu mbona mna wasiwasi..hela za kampeni 2010 ndio zinakusanywa taratibu...kwa makisio zitahitajika kama Dola Milioni 100 na ushee...sio nyingi sana. Ndio zinakusanywa taratibu hivyo...msiwe na wasi utaratibu huu ni wa kawaida kama mtakumbukwa uchaguzi wa 2005 zilitoka moja kwa moja pale BoT ila kwa sasa pameshaonekana kuwa hapafai.
 
Hafi mtu. Ni lazima kieleweke. Ila tahadhari ni lazima tuchukue!!!!
 
Mkuu Halisi

Heshima mbele.

Hii habari yako ukiisoma kwa makini utagundua vitu viwili muhimu.

Kwanza kuna watu ndani ya jamiiforums.com wamepewa kazi ya kudukuza vyanzo vya maoni nikimaanisha wapi maoni yanayoingia ndani ya tovuti ya jamiiforums yanatoka.

Na pili, vyanzo hivyo ni nani wanaishi wapi na wanafanya nini.

Sasa mimi niliwahi kutoa maoni yangu kuhusu ni kwanini nilijiunga na jamii forums na kama kuna anaependa kurudia kusoma maoni hayo yanapatikana katika unganisho lifuatalo hapo chini:

https://www.jamiiforums.com/habari-...2-why-i-like-jamiiforums-my-thought-week.html

Anyway yote ni maisha yale ya kupigania haki ya yale ya kudhulumu haki na ili upatikane usawa ni lazima vitu hivi vitwangane na apatikane mshindi na lazima mshindi huyo awe mpigania haki.

Nikiwa huku ughaibuni kuna siku nilikutana na moja ya vyanzo vyangu vya habari ambae yeye yupo pale kwenye uwanja wa vita (Tanzania).

Ni very reliable na nnamwamini sana na akaniambia habari ambayo si tu ilinistua bali alinishangaza sana.

Jamaa akaniambia kwamba simu zote ziingiazo nchini Tanzania zinasikilizwa kupata habari ambazo pengine ni "credible" kwa wasikilizaji au kwa "fan" tu.

Mimi nikaelewa kwani mtindo huu ambao kwa kiingereza unaitwa eavesdropping ni ule ambao simu zinasikilizwa na hizo task forces na zikiishachujwa basi wale elements za resistance, magaidi, na wasumbufu wote katika jamii huwa wanafuatiliwa.

Eavesdropping inaweza kufanyika kupitia nyaya za simu au wiretapping, email, njia ya kutuma text kwenye simu au computer, na njia zingine za mawasiliano zinazochukuliwa kuwa ni private. "Eavesdropping" iikinoga inaweza kupelekea kufanya kitu kiitwacho kwa kiingereza snitching njia ambayo mkuu mwenzetu ameeleza ya task force ambapo watu wanatumika kutafuta watu wengine fulanifulani na kuwa-report kwa vyombo vya dola-hususan Police.

Sasa mambo haya hayakatazwi ila yanakiuka haki za msingi ambazo zimo hata kwenye katiba yetu ya pamoja na mengine haki ya kutoa maoni na haki ya kupata habari. Sasa je yamepitishwa na Bunge? au ndio kimefanyika kikao cha dharura na emergence laws zimepitishwa?

Utasikiliza simu ngapi bongo. Wana set target na kufuatilia simu hizo tu.
 
Katika hali isiyo ya kawaida, majambazi wamejipanga kwa kuunda kikosi kazi (task force) ya kupambana na wenye mali (wananchi) hasa wale wenye kupenda kupiga kelele za "wezi hao!!!! Wezi hao!!!!".

Kazi ya task force hiyo imeanza kwa kasi na tayari baadhi yao wamo humu JF na wanawashughulikia wale wote wanaopiga kelele za mwizi.

Niliwahi kuona pale Kariakoo kibaka anapora simu na anapofukuzwa wenzake wanamsindikiza na kumgeuzia kibao aliyeibiwa na kuanza kumdunda kwamba ndiye mwizi na wakati mwingine mwenye mali huuwawa na kuchomwa moto.

Hali hiyo sasa imeingia kwa majambazi wakuu na sasa kazi imeanza kwa kasi na wale wote wanaopiga kelele za mwizi (akiwamo Mwanakijiji) wajiandae kugeuziwa kibao na kufukuzwa, wakati wao (familia zao) ndio walioibiwa na majambazi wakuu.

Majambazi hao wanakutana usiku na mchana na wana fungu kubwa kwa kazi hiyo ya kujilinda.

Kwa hiyo wamekutuma wewe uje useme huku siyo? Basi waambie ujumbe umefika...
 
hao mafisadi tunasema sisi na hizo kesi wakishinda itakuwaje ?? yule anayemwita mtu fisadi wakati suala liko mahakani ni sawa na yule anayeita mwizi njiani anapoona watu wanaita mwizi
 
Wana JF kuna jambo lisilo la kawaida.Tumevamiwa.Jinsi mijadala inavyokwenda inaelekea kuna tatizo. Wasafisha mafisadi wamo humu na mashushu wamo humu.

Wamejizatiti kabisa kutuhujumu,kwa hiyo hatuna budi na sisi kuwa more articulate and smart katika kutoa hoja zetu.

Tukumbuke kwamba JF ipo kwa ajili ya kuinua maisha ya watu wetu.
 
Mkuu Halisi, usijishushie hadhi kiasi hicho, kama unajua kuna watu humu JF wameunda Task Force wataje na uweke ni vipi umejua hilo. Nao watajitetea, lakini ukianza hisia ni sawa tu na wale wanaoua vikongwe kule kanda ya ziwa kwa sababu wana macho mekundu.

Eti watu wanaopiga kelele kama Mwanakijiji wajiandae kugeuziwa kibao. Hapa ndio huna points kabisa, unataka sema kuwa watu fulani humu (kama Mwanakijiji) wakiandika kitu hata kama hakifai basi wote tukubali. Hiyo sio mjadala. UNATAKA SASA ANZISHA MAKUNDI, MANAKE IKITOKEA SASA WALE UNAOONA KUWA NDIO WAPIGANAJI WAKIBANWA UTASEMA SI NILISEMA. Mkuu kwa nini usifungue eneo kama Shehe Yahya udanganye watu kwa utabiri.

Kuna watu wanataka wayasemao wao, ama watu wao ndio iwe mwisho wa mjadala. Kutofautiana kulikuwepo, kupo na kutakuwepo. Mtu akifanya jambo jema ataungwa mkono, akikosea atakosolewa bila kuogopa eti kuwa nitaambiwa niko katika hiyo Task Force. Sasa usigeuze kukosoana ni kuwaunga mkono mafisadi. Huo ni mwisho wa kufikiri.

Kama majungu vile??
 
Back
Top Bottom