Tahadhari: Lifts(Elevators) zinaweza kuua!

Tahadhari: Lifts(Elevators) zinaweza kuua!

kajamaa kadogo wakati maisha yako yapo hatarini hakuna kingine kitakachoingia akilini mwako na kwenye hisia zako zaidi ya kuomba uokolewe/uokoke na janga hilo tu. Tena utaweka ahadi za kila aina kwa Mungu wako kua ukitoka salama utaacha dhambi zote 😀😀😀
Mda huo kitendea kazi cha Papuchi hakiwezi amka hata kwa dawa, saikolojia ipo ovyo hauwezi hata waza vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitasahau siku ya kwanza kupanda lift.
Sikupata matatizo yoyote wala sikuwa na sehemu yoyote na sababu maalumu ya kwenda huko, ila nilitaka tu kujua inakuaje kuaje ni pale Lumumba jengo la ushirika mwaka 2002. Naenda narudi naenda tena. Hadi kichefu chefu.
 
Sitasahau siku ya kwanza kupanda lift.
Sikupata matatizo yoyote wala sikuwa na sehemu yoyote na sababu maalumu ya kwenda huko, ila nilitaka tu kujua inakuaje kuaje ni pale Lumumba jengo la ushirika mwaka 2002. Naenda narudi naenda tena. Hadi kichefu chefu.
Wakati huo kulikua na ofisi za Wizara ya Viwanda na Biashara, BRELA na Ofisi za Ushirika zenyewe. Ma lift yao mawili yalikua ya kizamani sijui kama wameshayabadilisha. Miaka ya nyuma kidogo ya hapo wakati CTN(Baadae DTV na sasa Chanel Ten) wakiwa ghorofa ya tisa na kumi kuna mtu alikua anakaa ndani ya lift muda wote ili kui oparate kama dereva!
 
Nimependa ulivyomkumbatia huyo dada mpaka kablidi.
Swali langu watu hawajaisi kitu humo kwenye elevetor kinaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaa mkuu, alivyokuja kunikumbatia kweli nilimuona ila akili yangu nadhani pamoja na ya kwake haikua huko unapoelekea wewe, maana dada wa watu alidhani malaika mtoa roho kaja kuchukua roho yake, sasa labda akinisogelea mimi naweza kumfukuza huyo ziraeli mtoa roho. Wakati huo na mimi akili yangu inatoa ahadi kedekede kwa Muumba pindi akiniokoa na janga hilo nitamfanyia nini yeye Mungu wangu. Nilijua dada anataka kupoteza fahamu baada ya kufunguliwa milango
 
Halafu sehemu nyingine lift zinajaa balaa! Kama lile jengo la RITA pale karibu na Bilicanas. Unaomba Mungu lisitokee jambo baya maana inabidi hiyo rescue action isichelewe hata kwa dakika moja amasivyo itakua balaa kwa watu wanavyojazana
Kwa juu inatakiwa waandika maxium users at a time, Mfano 8 people only maanake ni kuwa Ikitokea hitilafu hewa ya humo ita wa accommodate kwa muda mtakao kuwa mnasubiri rescue
 
Hata bongo zipo za vioo ni nzuri sana kwajili ya usalama
Nimefurahinkwelim kweli. Ati milango ya kioo nitauvunja!! Wadhani hicho lkioo ni laini tu kwamba ukipiga chafya tu tiyari kimevunjika?? Hapana. Kioo uzuri wake ni kuwa, wataalam wanawaona mpo wapi hivyo watafanya bidii kuwatoeni. Mlango wa lifti ni madhubuti saana kwa usalama wako pia.
Furaha na masikitiko ni huyo aliyebaki anamkumbatia mdada aliyeingiwa kifafa. Nadhani hata namba zake alikupa umpigie. Hapo ndio wamama mshike adabu mbele ya mwanamume
 
Hizo ndio serikali ingehakikisha zinawekwa sehemu zote wanapotaka kuweka lift
Budget sasa mkuu, Ila watu wa malls wanajitahidi sana Kuweka izo mkuu ila hata mimi huwa nasoma upepo wa jengo afu ndio naamua either lift au Nichape tu mguu ata kama ghorofa ya 15
 
Ndio maana jengo la CCM pale Lumumba St la ghorofa 8 wameachana na lift kabisa kina dada R. Mogela wameshazoea kupanda na kushuka ngazi kila siku!
Meza ya 'Mapokezi' yao iko chini ukiuuliza ofisi fulani gorofa ya sita hata kama hawapo atakwambia "wapo we panda juu" utahenya na ngazi na kukuta hola wamefunga au umekosea namba ya mlango! Inabidi ushuke ukamuone yule resepshenist! Anakuambia "jaribu mlango na. 8 ghorofa ya 8" unamwangalia kwa hasira! Kummeza huwezi! Hapoapo unamuuliza wapi naweza kwenda short call? Anakujibu gorofa ya nne kushoto baada ya ngazi! Ghafla kichefuchefu kinapanda! Chini! Kimya!
Nimecheka Sana, ishawahi nitokea hiyo,Mimi nilidhani wananipima uvumilivu maana yalikuwa Maswala ya kuomba kazi, but where,kukuenjoy tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom